Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Pole sana mkuu! Ila siku hizi kuna kesi nyingi sana za watoto kupelekana chooni wawapo shuleni na kumaliza michezo michafu hivyo wazazi tuwe makini,ila nakushauri uchunguze wakati ukiendelea na tiba ya mwanao huenda ukagundua kuna wapuuzi wameanza kumfunza mambo hayo mwanao.
 
pole sana mkuu....

binafsi sidhani kama huyo mwanao amepata maambukizi kupitia ngono itanichukua muda sana kuamini katika hilo though dunia imepoteza dira siku hizi.

kutokana na umri wa mwanao me naamini kabisa vitu vyenye ncha kali ndiyo vimepelekea haya maambukizi kwa mwanao, mfano wembe, sindano nk.

usife moyo yote ni mipango ya Mungu atakusaidia.

pole sana mkuu....
 
Ndugu pole sana, lakini kwa sasa hali inaweza ikawa mbaya kwa sababu kuna watoto wanazaliwa wakiwa positive+, transmission from mother to child. Hawa watoto wanaenda kusoma shuleni na watoto wengine, ni vigumu sana kuwatambua na hakuna shule yao peke yao so lazima wewe mixed na watoto wengine. Watoto Hawa wanacheza na kufanya shughuli mbalimbali shuleni pamoja. So possibly inaweza kuwa mtaani au shuleni huko.
 
Siku hizi watoto wadogo wengi sana wapo HIV positive. Na baahati mbaya katika michezo kuna vitu vyenye ncha kali watoto wamekuwa wakichezea na kushirikiana hususani nyembe za kuchongea penseli na nail cutter. Pia ktk kucheza pamoja endapo wana vidonda ni rahisi sana kuambukizana kama mmoja ni HIV+. Kuna mtoto wa shemeji yangu wife alimkuta anashika shika vidonda vya mwenzake ambaye inasemekana ni HIV+. Kwa mazingira kama haya watoto ni rahisi sana kuambukizwa HIV. Hili ni fundisho kuwa tusipende kuwadhania vibaya wenye HIV, wapo wengi wana HIV na hawakupata kwa njia ya uzinzi.

Nakupa scenario ya nyingine; Dada yangu ana ugonjwa wa sukari, kwa hiyo hujipima sukari kila siku na kujichoma sindano. Siku moja katoto kangu kakasema nako kanataka kupima, akakachoma na kukapima. Binafsi hadi leo huwa sielewi dada alitumia sindano mpya kumchoma mwanangu au alitumia aliyotumia yeye kujichoma? Kwa mfano huu nadhani unaweza kuona ni kiasi gani watoto wetu wapo katika mazingira ya hatari wawapo nyumbani na hata shuleni.

Pole sana mkuu, mwenyezi MUNGU awape nguvu. HIV kaipata shule au hapo hapo nyumbani kwa watoto anaoshinda nao na most likely ni vitu vye ncha kali. Kama unatabia ya kuwapeleka wanao kwa kinyozi kunyoa, tafadhali hakikisha hawachongwi. Ktk kuchonga mara nyingi mashine zile huwa zinakata au kukwangua, imagine mashine imetoka kumnyoa mtu mwenye vidonda halafu ije imkwangue mwanao?
 
Kuna vitu viwili au vitatu hapo inaweza kuwa sababu.
1. Mazingira ya shule watoto hushirikiana vitu vingi bila uangalifu, au aliumia ktk bembea au vitu vingine vyenye ncha kali kama compass, nyembe
2. Watoto huchezea vitu hatari vyenye ncha kali hasa mazingira ya nyumbani. Pengine na watoto wenzie walio athirika.
3. Kwenye milango ya mabasi ya daladala au school bus kama anatumia huduma hiyo.
4. Je mliwahi kubadilisha mfanyakazi? Pengine huyo aliye ondoka ndio alikuwa muathirika. Sasa unakuta wana nyembe au sindano za urembo au heleni n.k.
5. Kuna mgeni alikuja na maradhi. Kwwnye miswaki watoto hawako makini.

Kuna watoto wengi tu huko mashuleni na jirani mtaani ambao ni waathirika wa HIV sema wanatumia dawa wanashirikiana na watoto wenzao vitu vingi vya hatari bila tahadhari. Pia wengine hupata mazingira ya hospital.

Jambo la msingi mtoto atumie dawa. Pole sana mkuu maana huo ni mtihani mkubwa sana kwa wazazi na mtoto mwenyewe.
 
sijaongelea mke wake, nmeongelea DNA ya Baba na huyo mtoto...kwani mke hawezi shiriki na dume gonjwa akapata ujauzito? alafu mama akabaki kuwa mzima...mtoto akaathiriwa?. Afanye hilo km ataweza maana kuishi na mwanamke kunahitaji akili ya ziada
mkuu umisha ambiwa mama yake yupo salama!
 
pole sana Mkuu,kuna jamaa ilikuja mtokea hivyo ,source ikawa kuna mgeni alikuja kwake ,mswaki akatumia alafu mtoto wake akaja utumia tena kwa muda mchache uliofuta ,nahisi ulibaki na damu damu labda ya michubuko sijui
 
Pole sana baba
La muhimu sasa ni kumsaidia sana mtoto awe na afya nzuri
Mwangalie sana na usimuonyeshe huzuni yoyote please
Apate furaha sana wala usimfanye ajue ni mwisho wa maisha yake
Nakuombea uwe na subra sana na mama yake pia
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom