Mwanangu jifunze haya kuhusu mwanamke

Mwanangu jifunze haya kuhusu mwanamke

Mkuu No. 7 usiifanyie kazi hata kidogo baba neno limemtoka tu, zamani wake zao ndio walikuwa walishaji na wahudimiaji na watunzaji wa familia. Jaribu leo uone kama suruali hujabeba begani.

Mkuu twatofautiana uwezo wa kimaisha na nguvu za kazi. Aliyejaaliwa muache aoe bwana.
 
haya mlete dingi yako ambaye ni clim aje atuambie acheni maneno yenu ya shombo nyie ndio wale watoto hamjiu baba zenu mlizaliwa tu mnatumia majina ya wajomba kama ubini wenu nasema haya kwani ungekuwa unajua thamani ya baba usingethubutu mtusi mzazi wa mwenzako kwa kumwambia kilaza

Ndio Wanadamu weng walivyo ndg. Hajui kumtukana mzazi wa mwenzako ukirejeshewa tusi kama hlo kwa mzazi wako yeye ndio atahesabika amemtukana mzazi wake mwenyewe.
 
Kwanza clim ndiyo nini? Halafu kwani kuwa kilaza ni tusi?
Basi kama ni tusi ngoja nibadilishe!
Huyo Mzee uwezo wake wa kufikiri na kuchambua mambo ni mdogo, sasa kama hapo pia bado nitakuwa nimetukana basi na iwe hivyo, kwa maana nimeishiwa Misamiati ya kuweza kumuelezea huyo mdingi!

Vijana kama nyie ni ambao mmelelewa na single parent au watoto wa zinaa hata elimu ya dini hamna
 
Kwa ujumla baba yako alikushauri vizuri,namba 7 na 9 na sehemu nyingine mzee wako alikushauri kwa mujibu wa dini yake na yako na si vibaya maana hajazijaribu dini nyingine ila ukiangalia vipengere hivyo vinaklinzana soma tena uone:
7. Mwanangu!
Zamani tulikuwa na wake wengi na watoto wengi licha ya kwamba tunategemea kilimo mashambani, ingawa kwa sasa maisha yamebadilika, lakini usizuwie kizazi kwa khoff ya rizq!. Pia usimkumbatie mke mmoja peke yake, ongeza wawili au watatu, kama utawafanyia uadilifu.
9. Mwanangu!
Usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio zaidi, na kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.
My take: Hao utakaooa katika namba 7,maana umeshauriwa usimkumbatie mke mmoja peke yake,hapa nauliza hao utakaowaoa baada ya mali kuongezeka si nao watatumia fedha uliyochuma na mkeo wanatofauti gani na viruka njia/mchepuko?
 
Hapa mbona akina Mamdenyi, badieby, Charminglady Demba na wengine hawasomeki? nini maoni yenu kuhusu ujumbe huu?
 
Ushauri mzuri...anafaa kuwafunda wanaume...
Manake mwingine mke akichelewa kupika tu kesi ishafika nyumbani...Mzee kashasema hana hisa juu ya yanayoendelea...lol...muyamalize wenyewe...!

Ukiyafuata utakuwa best husband kwa mkeo...

Kweli mwari wangu......i wish huyo baba ake angekua babu yangu maana he is was man ever
 
Kwa ujumla baba yako alikushauri vizuri,namba 7 na 9 na sehemu nyingine mzee wako alikushauri kwa mujibu wa dini yake na yako na si vibaya maana hajazijaribu dini nyingine ila ukiangalia vipengere hivyo vinaklinzana soma tena uone:
7. Mwanangu!
Zamani tulikuwa na wake wengi na watoto wengi licha ya kwamba tunategemea kilimo mashambani, ingawa kwa sasa maisha yamebadilika, lakini usizuwie kizazi kwa khoff ya rizq!. Pia usimkumbatie mke mmoja peke yake, ongeza wawili au watatu, kama utawafanyia uadilifu.
9. Mwanangu!
Usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio zaidi, na kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.
My take: Hao utakaooa katika namba 7,maana umeshauriwa usimkumbatie mke mmoja peke yake,hapa nauliza hao utakaowaoa baada ya mali kuongezeka si nao watatumia fedha uliyochuma na mkeo wanatofauti gani na viruka njia/mchepuko?

Kuna tofauti ya viruka njia na mke wewe. Ukioa unakuwa umemuidhinisha kisheria na anahaki sawa. Ukiona ngumu itabidi kuwaoa wote kwa pamoja kisha unatafuta nao mpaka ukipata pia spendi nao wote kwa pamoja.
 
Wewe nadhani utakuwa upande wa pili ndio maana una kataa mwenza. Acha wivu nyie mpo weng sana na kila mmoja anataka kupata mume.

Hujakosea, ukewenza haufai mtu unakufa taratibu, kisa mawazo mahaba yameishia kwa bi mdogo, ukichepuka na akakufuma eti na yeye ana kula tigo ya mchepuko wako, haa!" The world is not fair"
 
1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo,
mwingine anaweza kuwa mama wa watoto
wako, lakini ukipata mwanamke ambae
atakuwa kama mama kwako, mama kwa wanao
na mama kwa familia, tafadhari mwanangu
usimuache huyo!


2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako
kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za
jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata
nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa
majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi
pamoja!


3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha
familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako,
usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama
utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa
sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa
familia!


4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu
na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na
mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha
mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu
mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi
fungu husika hata kama limetokana na
michango yenu wawili. wanawake wanajua sana
kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye
kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa
nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela
zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata
kama utakuwa umeishiwa!


5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo,
maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake
kwa muda mrefu sana na huacha kidonda
ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana
kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!


6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado
utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na
mke wako, sio muda mrefu utakuwa bacheol
tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke
na mume!


7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi
na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na
mashamba makubwa na mavuno yalikuwa
makubwa, lakini kwa sasa maisha
yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke
wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na
mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia
ukubwa wa familia yako!


8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao
nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza
kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini
kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini
ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana
pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike
kikubwa unachotakiwa kukifanya ni salamu
itakuw unatosha


9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza
kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia
hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui
mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na
kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae
aliweza kusimama imara wakati wote wa
mapito yenu magumu.


10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au
kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna
kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha
kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au
kutimiza wajibu wako.


11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au
kumlinganisha mke wako na mwanamke
mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia
sana na hajakufafanisha na mwanaume
mwingine yoyote huko nje na ndio maana
aliamua kuwa na wewe.


12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa
haki za wanawake, sawa,kama mwanamke
anasema ana haki sawa na wewe katika
nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani
kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu
timiza nusu yako na mwambie atimize nusu
iliyobaki.


13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa
bado kigoli (bikra) na nilikuwa naenda sana
kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo
bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa
muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na
wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na
ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo
ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.


14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule
kwa kuwa nilikuwa mjinga kama waze wengi
wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye
ujinga huu, kwani kiwango cha mafanikio ya
wanawake sasa kimefanya wanaume
waonekana ni watu wa kawaida sana na sio
muhimu kama zamani, Ukijaliwa watoto wape
elimu.


15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu,
wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa
siwezi kukudanganya, wengine waliongeza
urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua
na masikio lakini usisahau hawakuonyesha
maumbile yao nyeti hadharani kama sasa.
Hakikisha mkeo analijua hili!


16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna
hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye
maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu
wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba
usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa
kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama
gazeti kwa kila mtu.


17. Mwanangu,nilimnunulia mama yako kifaa
cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa
kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua
cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie
mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na
uwezo wako kama ambavyo unahangaika
kutimiza ndoto zako.


18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na
mama yako, utu uzima una changamoto nyingi
sana na Mungu akikujalia utaziona muda
ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako
kama baba wa familia kumbuka pia bado
tunaishi na wewe ni mtoto wetu.


19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali,
Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui,
ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu
kila siku!

20.mwanangu.....................
 
mmmh ngoja nisubiri watakapo kuwa wanatoa michango yao nami nitaisomea huko hii habari ndefuuuuu!
 
Back
Top Bottom