imerudiwa sasa mara ya 13 nadhani.....
imerudiwa sasa mara ya 13 nadhani.....
Naona makala yangu wame edit na kuiweka ktk gazeti la mwanaspoti la jana 26/08/2014. Sijapenda kueditiwa ila nimependa ujumbe umewafikia weng.

MWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURII KABLA HUJAOA¡-.
1. Mwanangu!
Mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa mwema kwako, mama mwema kwa wanao na mama kwa familia, tafadhali mwanangu usimuache huyo.
2. Mwanangu!
Majukumu ya nje ni ya kwako na majukumu ya ndani ni ya mke wako. Lakini usimfanye mke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za jikoni peke yake, mtafutie msaidizi kama uwezo uko nao, na kumsaidia mwenyewe kunajenga mapenzi ya ziada.
3. Mwanangu!
Nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa familia!
4. Mwanangu!
Ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo, pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. Wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa.
5. Mwanangu!
Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni.
6. Mwanangu!
Sasa unaamua kuoa, kama bado utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. Ukioa badilika anza kuishi maisha ya mke na mume.
7. Mwanangu!
Zamani tulikuwa na wake wengi na watoto wengi licha ya kwamba tunategemea kilimo mashambani, ingawa kwa sasa maisha yamebadilika, lakini usizuwie kizazi kwa khoff ya rizq!. Pia usimkumbatie mke mmoja peke yake, ongeza wawili au watatu, kama utawafanyia uadilifu.
8. Mwanangu!
Chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu, lakini kumbuka, kitu pekee tulichoweza tunafanya chini ya mwembe ilikuwa ni mazungumzo pekee mbele ya maharimu wake. Nakushauri ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza kufanya nao ni salaam na kama ni mazungumzo, hadharani si vinginevyo.
9. Mwanangu!
Usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio zaidi, na kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.
10. Mwanangu!
Kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au kutimiza wajibu wako.
11. Mwanangu!
Usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanishana na mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.
12. Mwanangu!
Sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa "haki za wanawake", muusie mkeo na mwambie ni miongoni mwa miito ya waovu ajiepushe nayo. Ni Uislamu pekee unaojali heshima, haki na utu wa mwanamke.
13. Mwanangu!
Sikuwapeleka dada zako shule kwa kukhofia utamaduni wa kimagharibi kuwaathiri, kama wazee wengi wa hapa kijiji walivyokuwa. Tafadhali wewe wasomeshe, ingawa, kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa, baada ya kupata elimu ya shule, kimefanya wanaume waonekane ni watu wa kawaida sana na sio muhimu kama enzi zetu. Ukijaliwa watoto watilie mkazo zaidi pia na kwenye elimu ya Uislamu.
14. Mwanangu!
Zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!
15. Mwanangu!
Mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe bila kila
mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa kutatua changamoto zenu
bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.
16. Mwanangu!
Nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza, tafadhali msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako kama ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.
17. Mwanangu!
Usiiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una changamoto nyingi sana na Mwenye-ez-Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako kama baba wa familia
kumbuka pia bado tunaishi na wewe na ni mtoto wetu.
18. Mwanangu!
Swali Swala zako kwa wakati, na hakimisha unaswali, na familia yako, kuna kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!
19. NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA
20. NAKUPENDA SANA MWANANGU
Huyo Mdingi Ni Kilaza na Alikudanganya Sana!
haya mlete dingi yako ambaye ni clim aje atuambie acheni maneno yenu ya shombo nyie ndio wale watoto hamjiu baba zenu mlizaliwa tu mnatumia majina ya wajomba kama ubini wenu nasema haya kwani ungekuwa unajua thamani ya baba usingethubutu mtusi mzazi wa mwenzako kwa kumwambia kilaza
BulldogMWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURII KABLA HUJAOA¡-.

Hata Mimi nimeshangaa hivi aliwasiliana na wewe kabla hajatoa?maana kule yeye anapiga hela