Mwananchi: Mtupe vibali tukauze mahindi nje ya nchi

Mwananchi: Mtupe vibali tukauze mahindi nje ya nchi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,292
Reaction score
4,000
Wakulima wa Mahindi Wilayani Ludewa Mkoani Njombe wamesema kutokana na kukabiliwa na hatari ya kupata hasara kutokana na kukosekana kwa maghala ya kuhifadhi mahindi wanaiomba Serikali kuchukua hatua za haraka ili kutatua hali hiyo.

Wamesema hayo baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Antony Mtaka kuomba msaada wa kupata kibali cha kuuza mahindi nje ya nchi, pamoja na kuomba kuongezewa muda wa kurejesha mikopo yao benki hadi watakapopata bei nzuri ya mazao yao.

 
Back
Top Bottom