Mwanamke wangu alinidharau baada ya kupata Kijana mwenye gari! Sasa anatamani kuwa na mimi tena

Niimemaliza Chuo mwaka 2018 nikaoetea dili kadhaa za pesa na kabla sijafanyia pesa jambo lolote nilikuwa na ndoto ya magari kwanza.
Ndio ununue magari yote hayo? Idadi hiyo ya magari ni kwa mtu mwenye familia sio aliyeko single. Jitafakari ndugu yangu unaonekana huyo binti amekutesa sana na huoni mbele bila yeye. Ingawa umetudanganya kwenye hayo magari naomba nikupe scenario nyingine je tuseme huyo dada ukamchukua halafu akakutana na mtu ana LC 300 VXR si atakumwaga na hivyo vi-baby walker vyako. Demu hakutaki tafuta mwanamke sahihi u-move on

Nimeandika mengi kukusaidia dogo
 
Nilikuwa na mwanamke ambaye nilikuwa nampenda mnoo, naye akasema ananipenda sana, Tukiwa chuo mimi nilikuwa nina kipindi 6 hadi 10 na yeye alikuwa anaingia saa 10 hadi saa 2 nikawa namsubiri atoke kisha namsindikiza kwao kwa daladala. Siku moja akanambie we nenda tu nikasema sawa sasa kuna mshikaji wangu alinichelewesha muda natoka naona pisi yangu inaingia kwenye IST (Vigari visnichi) shwaaa, akaondoka, nikapotezea siku nyingine tupo kwenye daladala akapigiwa simu alipomaliza kuongea akanambia mi nashuka kituo cha mbele, nikwamuuliza amekuja kukufata tena? akanijibi ni rafiki tu. tukateremka wote, jamaa akaja nikamuuliza manzi yangu huyu ni nani yako akanijibu nin mpenzi wangu, dah! niliumia sanaa sikujibu kitu baada yake nikaondoka badaye akanitafuta akanambia alinitania tu.

Tukaendelea ila nilitamani siku ifike ajue kuwa IST sio kitu ya kudharau upendo wangu, Mwenyezi Mungu sio Athumani, saivi nina Magari matatu BMW M5, CROWN, na VANGUARD na huwa napita kumsalimia anapofanyia kazi kuonesha kuwa Wakati wa mungu ni sahihi zaidi. Ila mapenzi bhana, saivi nina Magari anapaparika mnoo.

Tujifunze kuheshimu watu, Maana hatujui nani atakuja kuwa mlango wa Mafanikio Yetu

Acha kulalama, tafuta hela
 
Mtu mwenye magari matatu hawezi kuumizwa na hili. Badala yake anafurahi kupunguziwa zigo. Mtu mwenye magari matatu anakuwa busy na biashara au kazi.
Mkongwe huyu jamaa anatupiga uongo mchana kweupe. Idadi hiyo ya magari ni ya watu wenye familia ambayo anatumia say mme, mke na nyingine inakuwa reserve. Pia mtu kama huyo hawezi kuwa na mawazo ya kama mtoa mada lazima awe ameshajipata. Hapo ukute anaandika kalala kitandani anapigwa na joto umeme umekatika kajichanua anakuna fangasi za pumbuni
 
Umenunua kwa pupa sana,bado unmpenda na unataka mrudiane,kwa kifupu huwezi muacha.
 
Wanaume tunaojielewa hatuko hivyo,wewe utakua ni tule tuvulana,
Ukiachwa achika,eti naenda kumsalimia,demu alikuacha kwenye kituo cha Daladala akaondoka na ndinga ya mshikaji ukabaki unatoa macho tu kama fundi saa ila bado tu wewe unajipendekeza kwake!

Huo muda wa kwenda kumsalimia demu aliyekuacha kituoni unaupata wapi? punguza ujinga kua mtu anayejielewa na kujiamini,hayo ni maisha yako wala hayamuhusu huyo demu tena.
 
mambo ya kitoto hata haya magari ya BMW M5, CROWN, na VANGUARD ni ya kuringishia ..... so mkawa mnashare na jamaa wa IST tundu

kama mwenzio anaishi kwa tamaa tamaaa ... ina maana ni alert tu bado hajakupendaaa ......
 
Nilikuwa na mwanamke ambaye nilikuwa nampenda mnoo, naye akasema ananipenda sana, Tukiwa chuo mimi nilikuwa nina kipindi 6 hadi 10 na yeye alikuwa anaingia saa 10 hadi saa 2 nikawa namsubiri atoke kisha namsindikiza kwao kwa daladala. Siku moja akanambie we nenda tu nikasema sawa sasa kuna mshikaji wangu alinichelewesha muda natoka naona pisi yangu inaingia kwenye IST (Vigari visnichi) shwaaa, akaondoka, nikapotezea siku nyingine tupo kwenye daladala akapigiwa simu alipomaliza kuongea akanambia mi nashuka kituo cha mbele, nikwamuuliza amekuja kukufata tena? akanijibi ni rafiki tu. tukateremka wote, jamaa akaja nikamuuliza manzi yangu huyu ni nani yako akanijibu nin mpenzi wangu, dah! niliumia sanaa sikujibu kitu baada yake nikaondoka badaye akanitafuta akanambia alinitania tu.

Tukaendelea ila nilitamani siku ifike ajue kuwa IST sio kitu ya kudharau upendo wangu, Mwenyezi Mungu sio Athumani, saivi nina Magari matatu BMW M5, CROWN, na VANGUARD na huwa napita kumsalimia anapofanyia kazi kuonesha kuwa Wakati wa mungu ni sahihi zaidi. Ila mapenzi bhana, saivi nina Magari anapaparika mnoo.

Tujifunze kuheshimu watu, Maana hatujui nani atakuja kuwa mlango wa Mafanikio Yetu
Bado alikuathiri sana. Hapo bado pia huna magari ya maana labda hiyo BMW hukuwa unalazimika kupita kumwonesha kama ulipona. Ungesonga mbele na maisha yako.
 
Back
Top Bottom