Mwanamke wa kitanzania adakwa na "unga" Indonesia

Mwanamke wa kitanzania adakwa na "unga" Indonesia

Angekamatiwa Philippines angekuwa tayari ni marehem
 
Siungi mkono adhabu ya kunyongwa... Naomba akokotwe na gari uchi mpaka afe
 
Halafu ni kama zile za Masogange ambazo wakuu wenye mamlaka wa hapa Bongo walizivalia njuga hadi kupelekea baadhi kuzama hukohuko bondeni kuhakikisha Masogange anaachiwa Huru haraka sana,Duh!! Na kweli ikafaaa!! Na Mh Mwakyembe akaaibika mno! Kwa sababu yeye ndiye aliyevalia njuga pale nyerere airport hadi alituonyesha footage za Hekaheka wakati wakina maso wakiingiza mzigo wao hapo airport!! Maana presha ili raise ghafla pale uwanjani na kupelekea Polisi kuweka silaha mgongoni na kusaidiana na kina maso kukamilisha shughuli!!! Hatari sana!!
 
Nikiwaona akina chidi,ray c,nando alafu MTU kadakwa inapendeza arududishwe bongo anyongewe huku live pale kinondoni studio kabda wenzie ndio watastuka
 
Mwenye Clip Ile Ya Punda Aliyefanya Mtihani Ili Apate Degree Sasa Baada Ya Mtihani
Kurudi Home Kila Analoulizwa Kakosa
Mmiliki Wa Punda Akakasirika

Swali La Kwanza Akasema Sijaribu Lilikuwa Gumu Sana

Swali La Pili Muda Haukutosha
Kwahiyo Hujajibu Hata Moja Moja
Punda Mpumbavu Sana
 
Halafu ni kama zile za Masogange ambazo wakuu wenye mamlaka wa hapa Bongo walizivalia njuga hadi kupelekea baadhi kuzama hukohuko bondeni kuhakikisha Masogange anaachiwa Huru haraka sana,Duh!! Na kweli ikafaaa!! Na Mh Mwakyembe akaaibika mno! Kwa sababu yeye ndiye aliyevalia njuga pale nyerere airport hadi alituonyesha footage za Hekaheka wakati wakina maso wakiingiza mzigo wao hapo airport!! Maana presha ili raise ghafla pale uwanjani na kupelekea Polisi kuweka silaha mgongoni na kusaidiana na kina maso kukamilisha shughuli!!! Hatari sana!!
Wateje tu mkuuu,uzalendo ni kitu cha msingi sana
 
kwa sheria za huko huyo ajiandae kwa kifo tu maana serikali hiyo aitaki masihara kama walimuua raia wa australia itakuwa yeye mbongo
dunia inakuzawadia unachostahili
si alipenda kuwauwa watoto wa wenzake acha wamuue na yeye sasa
 
Atakuwa Msanii tu huyo.... Maana Show Off nyingi sanaa wakati hela Hakuna
 
Get rich or die trying.

Sad, misfortune caught her!!
 
antarafoto-pengungkapan-jaringan-narkotika-internasional-060117-agr-03-1024x683.jpg

Pichani ni mzigo aliyokutwa nao demu huyo wa Kibongo.

Polisi nchini Indonesia wamemkamata mwanamke wa Kitanzania aliyekuwa anajaribu kuingiza dawa za kulevya aina ya crystal methamphetamine na bangi nchini humo. Mtanzania huyo amekamatwa pamoja na Wanaigeria wawili ambapo mmoja wao ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi alipojaribu kutoroka.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo iliyotolewa jana Ijumaa na kuripotiwa na Jarkata Globe, Mtanzania huyo, ambaye jina lake halikutolewa, alikamatwa Jumatano asubuhi (04/01/2017) katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Soekarno-Hatta uliopo jijini Jakarta akitokea Kuala Lumpur, Malaysia.

Baada ya kukamatwa alikutwa na gramu 138 za crystal methamphetamine alizoficha kwenye kete 20, kete nyingine 66 za crystal methamphetamine alizokuwa amemeza na gramu tatu za bangi alizoficha kwenye chupi.

Mkurugenzi mkuu wa customs and Excise uwanjani hapo Bw. Heru Pambudi ameongeza kwamba mwanamke huyo alisafiri kwenda Indonesia kwa maelekezo ya boyfriend wake raia Uganda anayeishi Malaysia.

Baadae maafisa wa customs waliungana na polisi na kuwakamata Wanaigeria wawili waliokuwa wanaenda kupokea "mzigo" kwa Mtanzania huyo kwenye mgahawa mmoja uliopo katikati ya jiji la Jarkata. Baada ya maafisa hao kutinga ndani ya mhahawa huo, Wanaigeria hao walishtuka na kutaka kuingia mitini, hivyo kusababisha polisi kuwapiga risasi na kumuua mmoja wao hapo hapo. Wanaigeria hao wanatuhumiwa kuwa sehemu ya drug ring huko Malaysia.

Wakati huo huo, polisi nchini Namibia wanadai kukamata watu 135 kati ya Novemba 1 na Disemba 2016 kwa tuhuma za dawa za kulevya aina ya Mandrax, cocaine, crack cocaine, heroin na bangi. Kati ya waliokamatwa na dawa hizo wapo Watanzania watano.
The higher the risk the higher the return ajali kazini
 
Tamaa ya kutaka kuishi maisha ya raha bila kuwajibika ktk MSINGI ya utu!
 
Back
Top Bottom