Mwanamke wa kitanzania adakwa na "unga" Indonesia

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,477
15,320
antarafoto-pengungkapan-jaringan-narkotika-internasional-060117-agr-03-1024x683.jpg

Pichani ni mzigo aliyokutwa nao demu huyo wa Kibongo.

Polisi nchini Indonesia wamemkamata mwanamke wa Kitanzania aliyekuwa anajaribu kuingiza dawa za kulevya aina ya crystal methamphetamine na bangi nchini humo. Mtanzania huyo amekamatwa pamoja na Wanaigeria wawili ambapo mmoja wao ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi alipojaribu kutoroka.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini humo iliyotolewa jana Ijumaa na kuripotiwa na Jarkata Globe, Mtanzania huyo, ambaye jina lake halikutolewa, alikamatwa Jumatano asubuhi (04/01/2017) katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Soekarno-Hatta uliopo jijini Jakarta akitokea Kuala Lumpur, Malaysia.

Baada ya kukamatwa alikutwa na gramu 138 za crystal methamphetamine alizoficha kwenye kete 20, kete nyingine 66 za crystal methamphetamine alizokuwa amemeza na gramu tatu za bangi alizoficha kwenye chupi.

Mkurugenzi mkuu wa customs and Excise uwanjani hapo Bw. Heru Pambudi ameongeza kwamba mwanamke huyo alisafiri kwenda Indonesia kwa maelekezo ya boyfriend wake raia Uganda anayeishi Malaysia.

Baadae maafisa wa customs waliungana na polisi na kuwakamata Wanaigeria wawili waliokuwa wanaenda kupokea "mzigo" kwa Mtanzania huyo kwenye mgahawa mmoja uliopo katikati ya jiji la Jarkata. Baada ya maafisa hao kutinga ndani ya mhahawa huo, Wanaigeria hao walishtuka na kutaka kuingia mitini, hivyo kusababisha polisi kuwapiga risasi na kumuua mmoja wao hapo hapo. Wanaigeria hao wanatuhumiwa kuwa sehemu ya drug ring huko Malaysia.

Wakati huo huo, polisi nchini Namibia wanadai kukamata watu 135 kati ya Novemba 1 na Disemba 2016 kwa tuhuma za dawa za kulevya aina ya Mandrax, cocaine, crack cocaine, heroin na bangi. Kati ya waliokamatwa na dawa hizo wapo Watanzania watano.
 
Ni muendelezo wa vijana kutumika katika mambo maovu. Tunataka maisha ya harakaharaka pasipo kuyatolea jasho. Sasa ona atapigwa miaka kibao gerezani....tamaa mbaya
 
Back
Top Bottom