Mwanamke na matumizi ya mwili kama silaha…!

Mwanamke na matumizi ya mwili kama silaha…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
IMG_86651.jpg

Kuna nguo ambazo, mwanamke anapovaa, hawi huru kwani zinamghasi na kumpa hofu na wasiwasi kwa muda wote anapokuwa amezivaa. Kuna nguo za kubana, kuna nguo fupi sana, kuna nguo zenye kuonyesha sana na nyingine ambazo humnyang'anya mvaaji uhuru wake.

Watu wanapozungumzia nguo za namna hiyo, mtu anaweza kukimbilia kwenye dini au kudhani wanaosema hayo wanafikiri kwa mtindo wa mkabala wa zamani sana. Siyo kweli. Nguo hizi fupi sana, za kubana sana na zenye kuonyesha maungo, zinatoa picha kuu moja kuhusu mwanamke.

Kwamba mwanamke ni lazima aonyeshe maungo yake, jamii na hasa wanaume waone alivyoumbika. Kwa hiyo mwanamke ni mwili na mwili huo ni bidhaa, ambayo bila kuoneshwa hadharani jinsi ilivyo, haitapata mnunuzi. Kama siyo kwa kuonesha mwili wake kama bidhaa, basi atauonyesha ili kulipa fidia.

_DSC7195.JPG

Fidia gani?

Anahisi au kuamini kwamba, kuna eneo kwenye maisha yake ambalo haliko barabara, iwe sura, elimu, kipato, uhusiano na mengine. Lakini kwa sababu amesifiwa kwamba, ana mwili mzuri sana, anajaribu kutumia mwili huo kuziba huo udhaifu ambao anao au ambao ameambiwa anao. Kwa mfano, kama anaamini kwamba, ana mwili mzuri na kalio lililotokelezea, bora autumie mwili huo kuziba huo udhaifu wa sura mbaya!

Unakuta mwanamke kavaa kiguo kifupi, ukimtazama unaweza kwa haraka kudhani ni ndege aliyenyonyolewa manyoya. Kuna mwingine unaweza kukuta amevaa nguo za kubana na kama huna macho mazuri unaweza kudhani umekutana na kifurushi fulani.

15.JPG

Kwa kutembea uchi au kwa kuvaa nguo zenye kubana sana, anahisi kwamba, watu wanamsifu kwa mwili ule na hisia hizo humpa nafuu kutoka katika hisia za udhaifu wa yale maeneo aliyoamini kwamba, yana mapungufu.
Nasikitika kusema kwamba, wanawake wote ambao wanatembea nusu uchi au ambao wanavaa nguo zenye kubana hadi inakifu, wana matatizo mahali fulani kwenye maisha yao. Kuna jambo, mambo, matukio au hisia ambazo zinawafanya wajihisi kwamba, wana udhaifu, kwamba hawako kama ilivyotakiwa, kwenye maeneo hayo.

Mwili, ambao waliambiwa ndio kitu pekee kizuri walicho nacho na wakaamini, ndiyo silaha wanayoitumia kujaribu kujilinda na hisia za kutojitosha walizonazo. Kwa sababu ndiyo silaha pekee, huitumia vibaya hadi inawaumiza wenyewe. Ndiyo maana unawakuta wanatembea nusu-uchi wanazomewa, wanashindwa kupanda kwenye gari, wanahangaika wanapokaa chini kwa kujiziba na pengine kubakwa. Lakini bado hawawezi kuacha kuvaa hivyo, kwa sababu, wakiiacha silaha hiyo, wamekwisha.

Wakianza kuvaa nguo ndefu au zisizobana, watashindwa kabisa kufanya chochote kwa sababu hawajiamini katika eneo lingine lolote kwenye maisha yao, isipokuwa miili yao tu. Wanamudu kuendelea kuishi kwa sababu angalau wana huo mwili ambao waliambiwa ni mzuri, basi.

310509_10150333152254586_569519585_7956777_767388538_n.jpg

Hata hivyo, kuna wakati hiyo sifa waliyopewa kwamba miiili yao ni mizuri siyo ya kweli, lakini kwa sababu waliamini, huitumia. Unakuta mwanamke kavaa kiguo kifupi, ukimtazama unaweza kwa haraka kudhani ni ndege aliyenyonyolewa manyoya. Kuna mwingine unaweza kukuta amevaa nguo za kubana na kama huna macho mazuri unaweza kudhani umekutana na kifurushi fulani.

Lengo langu siyo kuwakashifu wanawake kwa mavazi yao ambayo ni uchaguzi wao, hapana. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kuna wanawake wengi ambao huvaa nguo wasizozipenda kwa sababu tu ya kujaribu kuziba mwanya wa hisia za udhaifu walionao dhidi yao.
 
Mbali na mapungufu waliyonayo, kunawengine wanaiga tu kisa flani kavaa amependeza, ngoja na mie nivae.. Mwisho wa siku wajaonekana kituko mbele za watu

kila vazi lina mahala pake pakuvaa, kama ni kwenye masherehe, kanisani sehemu yoyote yenye mjumuiko wa watu kiheshima ni bora mwanamke akavaa mavazi ya kusitiri mwili wake ili asiipoteze heshima yake mbele za watu.
 
Mtambuzi naona zaidi ya 98% ya maisha yako unatumia kujaribu kuwajua kwa undani hawa viumbe.

kwasababu dunia ndo wanawake na wanawake ndio dunia,,...mabadiliko popote pale hayawezi kutokea kama wanawake hawatojitambua ktk jamii,,....sababu wao ndo walezi wa familia,,,,,jamii na dunia kwa ujumla,,...ivo ata ww fanya ufanyavyo hangaika sana,,..jibidiishe sana ila mwisho wa yote utajikuta jitihada zako zote ni kwa ajili ya sisi wanawake,,...!!
 
Last edited by a moderator:
Mbali na mapungufu waliyonayo, kunawengine wanaiga tu kisa flani kavaa amependeza, ngoja na mie nivae.. Mwisho wa siku wajaonekana kituko mbele za watu

kila vazi lina mahala pake pakuvaa, kama ni kwenye masherehe, kanisani sehemu yoyote yenye mjumuiko wa watu kiheshima ni bora mwanamke akavaa mavazi ya kusitiri mwili wake ili asiipoteze heshima yake mbele za watu.
0011.jpg

Si kama hivi Lady doctor, si unaona wamependeza tu...
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
kwasababu dunia ndo wanawake na wanawake ndio dunia,,...mabadiliko popote pale hayawezi kutokea kama wanawake hawatojitambua ktk jamii,,....sababu wao ndo walezi wa familia,,,,,jamii na dunia kwa ujumla,,...ivo ata ww fanya ufanyavyo hangaika sana,,..jibidiishe sana ila mwisho wa yote utajikuta jitihada zako zote ni kwa ajili ya sisi wanawake,,...!!
1004462_492076340873083_273157534_n.jpg

Bora umemjibu, maana Bujibuji kwa maswali...!
 
Last edited by a moderator:
DSC09743.JPG

Kwa hiyo na hawa wakivaa ndefu wanawashwa eh, si ni hivyo madame B?

Inategemea na wao jinsi wanavyojisikia.
Mimi binafsi nguo ndefu huwa nazitazama kwa jicho la tatu........ndio maana niko radhi kubaki na kujifungia ndani kuliko kutoka nje na nguo ndefu.
Kila mtu na utashi wake kuhusu suala hilo.
Siwezi kulazimisha jambo ambalo najua vyema siliwezi....ni heri uone uhalisia wa maisha yangu kuliko kujifisha na mwisho wa siku nikaonekana kiumbe tofauti. Mtambuzi.....wewe tunange tu bhana, lakini mwisho wa siku itajulukana tu.
 
Sijakutaja lakini Madame B, Mi nimewasema hao kwenye picha na wala wewe hauko kama wao....
Sasa Kesho vipi utakuja pale LTHP au ndio nimekuudhi?
We tupia tu kivazi chako kama kawa kwani hujui ndo ugonjwa wangu...!

Haya maneno yangu hapa yachukulie kama ni maneno ya mkosaji...

Hii maneno yangu hapa asijeona Bujibuji
 
Last edited by a moderator:
sijakutaja lakini madame b, mi nimewasema hao kwenye picha na wala wewe hauko kama wao....
Sasa kesho vipi utakuja pale lthp au ndio nimekuudhi?
We tupia tu kivazi chako kama kawa kwani hujui ndo ugonjwa wangu...!

Haya maneno yangu hapa yachukulie kama ni maneno ya mkosaji...

Hii maneno yangu hapa asijeona bujibuji

hahahahahaha!! Jamani! I'll always luv u jf
 
Last edited by a moderator:
Inategemea na wao jinsi wanavyojisikia.
Mimi binafsi nguo ndefu huwa nazitazama kwa jicho la tatu........ndio maana niko radhi kubaki na kujifungia ndani kuliko kutoka nje na nguo ndefu.
Kila mtu na utashi wake kuhusu suala hilo.
Siwezi kulazimisha jambo ambalo najua vyema siliwezi....ni heri uone uhalisia wa maisha yangu kuliko kujifisha na mwisho wa siku nikaonekana kiumbe tofauti. Mtambuzi.....wewe tunange tu bhana, lakini mwisho wa siku itajulukana tu.

Ni kweli ila kuna mahali panazidi kipimo ....

Kama hao wadada...wanategemea sie tunaowaangalia tunakuwa na hali gani??

Babu DC!!
 
Sijakutaja lakini Madame B, Mi nimewasema hao kwenye picha na wala wewe hauko kama wao....
Sasa Kesho vipi utakuja pale LTHP au ndio nimekuudhi?
We tupia tu kivazi chako kama kawa kwani hujui ndo ugonjwa wangu...!

Haya maneno yangu hapa yachukulie kama ni maneno ya mkosaji...

Hii maneno yangu hapa asijeona Bujibuji

Hahahaha.......... huyo ndio Mtambuzi bhana,.....anakupa kubwa, afu anakupuliza vile vile.
Mie tena,.........lazima nitimbe hapo LTHP!!!
najua mie ndio Daktari wako,.......naja kukupa tibabu.
Nitakuja kaka,usijali.
Huyo Bujibuji sijui anahemea wapi maana tangu tuachane ile kona yetu......mpaka leo.
 
Last edited by a moderator:
kuvaa nguo fupi,zinazobana raha sana hasa zikukae.
Siyo na mchapati wako nyuma mtumbo mkubwa unajipiga kigauni kifupi cha mpira.
Mavazi yanatokana na mazingira,events.
 
Back
Top Bottom