Mwanamke na matumizi ya mwili kama silaha…!

Mwanamke na matumizi ya mwili kama silaha…!

The very same people, kesho wakivaa nguo fupi inamaana mapungufu yanatokea au?
Maana kwa mazingira niliyoyazoea; watu huvaa nguo kutokana na matukio. Kazini, misikitini, kanisani, club, beach, meetings, nguo zinakuwa tofauti.

Haya tufanye nakubaliana na wewe. Na wanaume wanafidia vipi mapungufu yao? Maana naamini mapungufu yapo kwa both sex.

Hizi theories sio 100% correct na some of them sio hata 50% correct. na vipi wenye sura kama angels na umbile baya kama langu na bado wanavaa nguo vupi na za kubana wanafidia nini na kuonesha nini?
Kaunga, hapo kwenye bold ni mada inayojitegemea, siwezi kuchanganya mada, hivi mtachangiaje?
Subiri wiki ijayo, maana mie kwa kawaida nikimsema mwanamke leo kesho namgeukia mwanaume, si ndio ku balance gender kwenyewe huko...!
 
Last edited by a moderator:
Kaunga, hapo kwenye bold ni mada inayojitegemea, siwezi kuchanganya mada, hivi mtachangiaje?
Subiri wiki ijayo, maana mie kwa kawaida nikimsema mwanamke leo kesho namgeukia mwanaume, si ndio ku balance gender kwenyewe huko...!

Na huko ambako hujaweka bold?
 
Hivi wee babu Mtambuzi una kazi ya kufanya leo, au nikupe kazi ya kufanya,
kwani wewe tukivaa nguo hizo zinakuwashia nini si uendelee na mambo yako ya kazi kuliko kusema sema tu
utafikiri umefungiwa morta kwenye mdomo wako yaani asubuhi yote hii badala ya kufanya kazi hapo
unakalia kubwabwaja tu na kushika hako ka ipad kako kutukera hivyo,

kwani ni nani aliyeaniambia mwanzoni kule ............................ niwe hivi jeans.jpgsi ni wewe hapo alaaa!
 
Last edited by a moderator:
Hiyo picha ya 3 imenistimuletisha,zigo la huyo sisterii limetuna balaa.Mood yangu imeharika kbs.Jf mnachangia 100% watu kulack concentration makazini.
 
kwasababu dunia ndo wanawake na wanawake ndio dunia,,...mabadiliko popote pale hayawezi kutokea kama wanawake hawatojitambua ktk jamii,,....sababu wao ndo walezi wa familia,,,,,jamii na dunia kwa ujumla,,...ivo ata ww fanya ufanyavyo hangaika sana,,..jibidiishe sana ila mwisho wa yote utajikuta jitihada zako zote ni kwa ajili ya sisi wanawake,,...!!
And vice versa, naunga mkono hoja.

Na nyinyi nanyi siku hizi kama mmezidi utamu vile.
 
IMG_86651.jpg

Kuna nguo ambazo, mwanamke anapovaa, hawi huru kwani zinamghasi na kumpa hofu na wasiwasi kwa muda wote anapokuwa amezivaa. Kuna nguo za kubana, kuna nguo fupi sana, kuna nguo zenye kuonyesha sana na nyingine ambazo humnyang'anya mvaaji uhuru wake.

Watu wanapozungumzia nguo za namna hiyo, mtu anaweza kukimbilia kwenye dini au kudhani wanaosema hayo wanafikiri kwa mtindo wa mkabala wa zamani sana. Siyo kweli. Nguo hizi fupi sana, za kubana sana na zenye kuonyesha maungo, zinatoa picha kuu moja kuhusu mwanamke.

Kwamba mwanamke ni lazima aonyeshe maungo yake, jamii na hasa wanaume waone alivyoumbika. Kwa hiyo mwanamke ni mwili na mwili huo ni bidhaa, ambayo bila kuoneshwa hadharani jinsi ilivyo, haitapata mnunuzi. Kama siyo kwa kuonesha mwili wake kama bidhaa, basi atauonyesha ili kulipa fidia.

_DSC7195.JPG


Fidia gani?

Anahisi au kuamini kwamba, kuna eneo kwenye maisha yake ambalo haliko barabara, iwe sura, elimu, kipato, uhusiano na mengine. Lakini kwa sababu amesifiwa kwamba, ana mwili mzuri sana, anajaribu kutumia mwili huo kuziba huo udhaifu ambao anao au ambao ameambiwa anao. Kwa mfano, kama anaamini kwamba, ana mwili mzuri na kalio lililotokelezea, bora autumie mwili huo kuziba huo udhaifu wa sura mbaya!



15.JPG


Kwa kutembea uchi au kwa kuvaa nguo zenye kubana sana, anahisi kwamba, watu wanamsifu kwa mwili ule na hisia hizo humpa nafuu kutoka katika hisia za udhaifu wa yale maeneo aliyoamini kwamba, yana mapungufu.
Nasikitika kusema kwamba, wanawake wote ambao wanatembea nusu uchi au ambao wanavaa nguo zenye kubana hadi inakifu, wana matatizo mahali fulani kwenye maisha yao. Kuna jambo, mambo, matukio au hisia ambazo zinawafanya wajihisi kwamba, wana udhaifu, kwamba hawako kama ilivyotakiwa, kwenye maeneo hayo.

Mwili, ambao waliambiwa ndio kitu pekee kizuri walicho nacho na wakaamini, ndiyo silaha wanayoitumia kujaribu kujilinda na hisia za kutojitosha walizonazo. Kwa sababu ndiyo silaha pekee, huitumia vibaya hadi inawaumiza wenyewe. Ndiyo maana unawakuta wanatembea nusu-uchi wanazomewa, wanashindwa kupanda kwenye gari, wanahangaika wanapokaa chini kwa kujiziba na pengine kubakwa. Lakini bado hawawezi kuacha kuvaa hivyo, kwa sababu, wakiiacha silaha hiyo, wamekwisha.

Wakianza kuvaa nguo ndefu au zisizobana, watashindwa kabisa kufanya chochote kwa sababu hawajiamini katika eneo lingine lolote kwenye maisha yao, isipokuwa miili yao tu. Wanamudu kuendelea kuishi kwa sababu angalau wana huo mwili ambao waliambiwa ni mzuri, basi.

310509_10150333152254586_569519585_7956777_767388538_n.jpg


Hata hivyo, kuna wakati hiyo sifa waliyopewa kwamba miiili yao ni mizuri siyo ya kweli, lakini kwa sababu waliamini, huitumia. Unakuta mwanamke kavaa kiguo kifupi, ukimtazama unaweza kwa haraka kudhani ni ndege aliyenyonyolewa manyoya. Kuna mwingine unaweza kukuta amevaa nguo za kubana na kama huna macho mazuri unaweza kudhani umekutana na kifurushi fulani.

Lengo langu siyo kuwakashifu wanawake kwa mavazi yao ambayo ni uchaguzi wao, hapana. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kuna wanawake wengi ambao huvaa nguo wasizozipenda kwa sababu tu ya kujaribu kuziba mwanya wa hisia za udhaifu walionao dhidi yao.
Kajala siku hizi ana kitunguu kikubwa hivyo!
 
Hivi wee babu Mtambuzi una kazi ya kufanya leo, au nikupe kazi ya kufanya,
kwani wewe tukivaa nguo hizo zinakuwashia nini si uendelee na mambo yako ya kazi kuliko kusema sema tu
utafikiri umefungiwa morta kwenye mdomo wako yaani asubuhi yote hii badala ya kufanya kazi hapo
unakalia kubwabwaja tu na kushika hako ka ipad kako kutukera hivyo,

kwani ni nani aliyeaniambia mwanzoni kule ............................ niwe hivi View attachment 102982si ni wewe hapo alaaa!

Mtambuzi kasema ukweli, na ukweli siku zote unauma
 
Biashara ni matangazo.

Hao wanauza miili yao, bila kuionesha watapataje wateja?
 
Kaka mkubwa kuna wengine hata vivazi vya kwenye avatar zao mmmh...wengine twabaki kuzikodolea macho kodo kodo!!!
 
Wewe mwanamke wewe,........ngoja tuendelee.
Sasa ndugu yangu mpaka ukisubiri wowowo ndio uvae nguo za kubana,......litakuja leo?
Unajilipua tu.

nani kasema kusubiri wox3??!?!?

mwenio siku moja navaa skini jinz yniende lthp.....sasa katika kuivuta ikachanika kabisa kwenye mshono wa katikati ya paja.....yani roho imeniuma jinz yangu manake haishoneki hapo!!!!
 
Mhhhhhhhh Mtambuzi..... naona leo umetuamkia asubuhi asubuhi.
Sasa sie wengine tukivaa nguo ndefu tunawashwa sana na ndio maana tunatumia nguo fupi.
CC: amu.
Kuna wanawake wengine huikwepa hii mentality ya Mtambuzi , hawajaenda shule, wana sura mbaya, hawana pesa, wana mishepu ya kufa mtu na hawavai nguo fupi wala za kubana, advantage yao kubwa ni kuitwa WIFE MATERIAL na huwekwa ndani haraka sana.
 
Back
Top Bottom