"Mwanamke mzuri akiwa kwa Mwenzio?"

"Mwanamke mzuri akiwa kwa Mwenzio?"

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
Wakati fulani katika umri wa ujana wa kati, pale nilipokuwa sijaoa mara zote nikisikia Baba kagombana na mama hisia zangu siku zote zilinituma nimwone Baba ni mkorofi, yeye ndio chanzo. Lakini pengine mama alikuwa akilalamika hata dada wa mumewe (mashangazi) hawana mahusiano ya karibu, hawampendi. Alieleza hata marehemu Bibi nae alikuwa hawana mahusiano mazuri, walimchukia. Yeye wakati wote hata sasa ambapo hata Baba amefariki anadai ndugu wa ukoo wa Baba hawana upendo nae na hawakupenda aolewe na Baba hivyo sisi watoto wake tusiwasikilize shida zao.
Wakati ule ugomvi wa Baba na mama ukiwa mzito mama alitushawishi tumuone yeye hana hatia labda kwa kutoroka nasi kwenda kwa mjomba au kuja kulala chumbani kwetu huku akilia " siwezi kuondoka niache watoto wangu". Kisaikolojia binafsi niliharibika kabisa na kuona kabisa mama anaonewa.

Kiasi fulani nami nimeanza ku experince maisha yale yale ya Baba na mama. Baada ya kuoa na kukaa katika ndoa kwa takriban miaka kumi sasa mama, dada na mke wangu wamekuwa hawaishi malalamiko kila mmoja kwa wakati wake. Mke wangu anahisi kutopendwa na ndugu akiwemo mama mkwe wake, mawifi na mashemeji. Anadai mama anawafundisha hata ndugu zangu wadogo kumdharau yeye na kumwona takataka tu.Dada zangu wao wanadai mamsapu anawadharau sana hajui mimi ni ndugu yao tumbo moja na bila wao singefika hapa..pengine unakuwa njia panda kama mwanaume. Najiuliza kumbe Baba alikuwa mwanaume mvumilivu sana mpaka sisi tukakuwa. Naona kwa Baba yangu mama hana tofauti na mke wangu, lakini kwangu mke wangu anaonekana kama vile mama anavyoonekana kwa ndugu za Baba yangu. Dada zangu nao wameolewa na wao pia kila mmoja wao haishi kuleta nyumbani matatizo ya familia za waume zao zinavyowafanya.Kama ilivyokuwa kwa mama, wakati fulani nilidhani dada zangu kitabia ni bora na ni wazuri kwa yote na wasingeweza kupata matatizo kwa wanaume zao.. Nahisi ndivyo ndugu wa mke wangu wanavyofikiri kuwa mke wangu hana tatizo ni mzuri wa tabia pia.

Ila kwa full tafakari haya yananifundisha kuwa upendo wa mwanamke yeyote upo zaidi kwa kile kinachoitwa "chake". Naona wanapenda zaidi wa kwao (mume wangu, mwanangu, ndugu zangu nk). Hii ndio inapelekea kutokwisha kwa migogoro ya ndoa itokanayo na wakwe na mawifi.

Dah,kweli mwanamke mzuri akiwa kwa mwanaume mwingine.
 
Hiyo kweli kabisa mkuu,utampenda mke wa mtu kwa kuwa huishi nae humgharamikii humtibu,humvalishi siku akipigwa kibuti na kuhamia kwako kwa kila kitu utaona dunia chungu.kuchukia ndugu huwa ni mechanism yao ili aweze kukutawala vizuri maana anajua ukiwa na ndugu zako karibu hawezi
 
I know wanawake wote. Wana mitihani, ata imesemwa kwa wenye imani ya usilam kwamba mwanamke, mali na watoto vyote ni mitihani.wanawake wenyewe kwa wenyewe wanaanzisha chuki iyo ipo katika familiia nyingi za kiafrika
 
mwanamke kiumbe wa ajabu sana, mama mkwe wangu humpigia mke wangu yaani mwanae mara kibao akimwelekeza kuhusu nyumba yetu! Msiweke vibati wekeni vigae kabisa ntakuja kusimamia lakini leo shangazi yangu kanipigia tu simu kaniuliza mnahamia lini imekuwa nongwa huyo shangazi yako anataka nini? anatulazimisha kuhamia dah nimebaki na maswali mengi sana. Wanawake bwana khaaa!
 
Hiyo kweli kabisa mkuu,utampenda mke wa mtu kwa kuwa huishi nae humgharamikii humtibu,humvalishi siku akipigwa kibuti na kuhamia kwako kwa kila kitu utaona dunia chungu.kuchukia ndugu huwa ni mechanism yao ili aweze kukutawala vizuri maana anajua ukiwa na ndugu zako karibu hawezi

Unajina baya lkn umeongea point wewe! Lkn kuna watu wanabahatika kupata wanawake wa maana mno!
 
Msiwainclude wanawake wote hiyo itakuwa overgeneralization kuna wanawake wengine wanateswa mno mpaka habari mama anafikisha kwa mtoto sio ili amchukie baba yake ila ni ili asije kuwa kama baba yake na yapo makabila ambayo kumnyanyasa mwanamke ni kama priveledge so wamama wanavumilia mengi mno
 
Zigo la mwenzio kanda la sufu.
Kitanda usicholalia hujui kunguni wake.
Mie ndo maana nilijiamualia kuwa bonge la wifi kwa wake za kaka zangu. Na dada zake Paw i treat them well (kwa anaeniudhi namtreat well kwa gharama za kaka yake). Nimepania sitakaa nigombane na wifi yangu hata anifanzeje.
 
Wakati fulani katika umri wa ujana wa kati, pale nilipokuwa sijaoa mara zote nikisikia Baba kagombana na mama hisia zangu siku zote zilinituma nimwone Baba ni mkorofi, yeye ndio chanzo. Lakini pengine mama alikuwa akilalamika hata dada wa mumewe (mashangazi) hawana mahusiano ya karibu, hawampendi. Alieleza hata marehemu Bibi nae alikuwa hawana mahusiano mazuri, walimchukia. Yeye wakati wote hata sasa ambapo hata Baba amefariki anadai ndugu wa ukoo wa Baba hawana upendo nae na hawakupenda aolewe na Baba hivyo sisi watoto wake tusiwasikilize shida zao.
Wakati ule ugomvi wa Baba na mama ukiwa mzito mama alitushawishi tumuone yeye hana hatia labda kwa kutoroka nasi kwenda kwa mjomba au kuja kulala chumbani kwetu huku akilia " siwezi kuondoka niache watoto wangu". Kisaikolojia binafsi niliharibika kabisa na kuona kabisa mama anaonewa.

Kiasi fulani nami nimeanza ku experince maisha yale yale ya Baba na mama. Baada ya kuoa na kukaa katika ndoa kwa takriban miaka kumi sasa mama, dada na mke wangu wamekuwa hawaishi malalamiko kila mmoja kwa wakati wake. Mke wangu anahisi kutopendwa na ndugu akiwemo mama mkwe wake, mawifi na mashemeji. Anadai mama anawafundisha hata ndugu zangu wadogo kumdharau yeye na kumwona takataka tu.Dada zangu wao wanadai mamsapu anawadharau sana hajui mimi ni ndugu yao tumbo moja na bila wao singefika hapa..pengine unakuwa njia panda kama mwanaume. Najiuliza kumbe Baba alikuwa mwanaume mvumilivu sana mpaka sisi tukakuwa. Naona kwa Baba yangu mama hana tofauti na mke wangu, lakini kwangu mke wangu anaonekana kama vile mama anavyoonekana kwa ndugu za Baba yangu. Dada zangu nao wameolewa na wao pia kila mmoja wao haishi kuleta nyumbani matatizo ya familia za waume zao zinavyowafanya.Kama ilivyokuwa kwa mama, wakati fulani nilidhani dada zangu kitabia ni bora na ni wazuri kwa yote na wasingeweza kupata matatizo kwa wanaume zao.. Nahisi ndivyo ndugu wa mke wangu wanavyofikiri kuwa mke wangu hana tatizo ni mzuri wa tabia pia.

Ila kwa full tafakari haya yananifundisha kuwa upendo wa mwanamke yeyote upo zaidi kwa kile kinachoitwa "chake". Naona wanapenda zaidi wa kwao (mume wangu, mwanangu, ndugu zangu nk). Hii ndio inapelekea kutokwisha kwa migogoro ya ndoa itokanayo na wakwe na mawifi.

Dah,kweli mwanamke mzuri akiwa kwa mwanaume mwingine.

kaka umeongea issue ambayo inagusa familia nyingi sana, binafsi niliwahi kuufuatilia ugomvi wa mama zangu na mawifi zao, usipokuwa makini utakuwa na maamuzi biased, wanawake wanahitaji uwe na upeo mzuri kubaini hoja zao.
mama anaweza kukulazimisha umuoe binti fulani kisa ana tabua nzuri za kumpendeza lakini ukioa siku chache ataanza kukulalamikia.

nimegundua ugomvi wao huwa ni kwenye mapenzi na umiliki wa wanaume, kwa mfano dada atakupenda kaka yao ukiwa hujaoa coz mapenz na,misaada mingi itakwenda kwao lakini ukioa wanaona misaada inapungua coz unajenga familia yako ila wao wanajua mkeo ndie anakufanya uwasahau na hapo chuki ndipo inaanza kwa mawifi na hata familia nzima ya mume kwa mkeo. wanaume tutumie busara maana ugomvi wa wanawake uhna hila nyingi na sijui kwanin hawapendani.
 
Changamoto ni nyingi mno mkuu. Kuna wakati unaweza kuona mama yako na mkeo wapo karibu sana lakini kwenye mazungumzo yao utasikia wakimsema wifi wa mama yako (shangazi yako).
Dada yako anaweza kuwa karibu na mkeo lakini dada yako akawa anavujisha taarifa mbaya kuhusu familia ya mumewe. Hawa watu siku wakigombana utayasikia yote hewani.

Ukiona wapo karibu hujue kila mmoja kile anachokitaka anakipata bila tabu.

Pengine mama anaweza kukupigia simu kukuuliza eti unaishije na mwenzio, angalia sie wanawake usituamini sana, usimwachie mwenzio kila kitu akajua, asijue ukoo wenu upoje, asijue mambo yako ya zamani, usimweleze kabisa kama ushawahi kuwa na mwanamke mwingine au umewahi kwenda kwa mganga, usimpe namba ya siri ya benki nk! Haya akijua atakumaliza, jilinde mwenyewe! Utatafakari haya maneno toka kwa mama yako mzazi, mwanamke unayemwona yu bora sana, yeye ni mke wa baba yako anataka usimwambie siri zako mkeo lakini yeye analalamika kuwa baba yako ni msiri sanaaana.
 
Mungu Baba atusaidie, wanawake, wanawake wenyewe twabuluzana na wanaume wanatufanzia acha tu? Sijui itakuwaje.
 
Zigo la mwenzio kanda la sufu.
Kitanda usicholalia hujui kunguni wake.
Mie ndo maana nilijiamualia kuwa bonge la wifi kwa wake za kaka zangu. Na dada zake Paw i treat them well (kwa anaeniudhi namtreat well kwa gharama za kaka yake). Nimepania sitakaa nigombane na wifi yangu hata anifanzeje.

Mmh...huyu ni King'astii? au mwingine. Mbona leo una point sana! Uliamkia mkono gani....
 
Zigo la mwenzio kanda la sufu.
Kitanda usicholalia hujui kunguni wake.
Mie ndo maana nilijiamualia kuwa bonge la wifi kwa wake za kaka zangu. Na dada zake Paw i treat them well (kwa anaeniudhi namtreat well kwa gharama za kaka yake). Nimepania sitakaa nigombane na wifi yangu hata anifanzeje.
Noted for action
 
Binafsi naona kila mwanamke anyelalamika kuumizwa basi mara nyingi chanzo cha maumivu yake ni mwanamke mwenzake. Mama mkwe na mawifi kumchukia mwenzao kisa hazai, hao hao kuanzisha zengwe la mirathi mara mwenzao anapofiwa na mumewe. kwenye daladala mwanamke hana uchungu mwenzake mwenye mtoto kusimama. vimada navyo havijali kumshika mume wa mtu huku mkewe akitaabika.

Kikubwa mambo ya ndoa ni yako na mkeo usipende kuwapa nafasi ndugu zako kuyaingilia. Ulimchagua wewe, umemuoa wewe hivyo wakuache uishi naye wewe.
 
mwanamke kiumbe wa ajabu sana, mama mkwe wangu humpigia mke wangu yaani mwanae mara kibao akimwelekeza kuhusu nyumba yetu! Msiweke vibati wekeni vigae kabisa ntakuja kusimamia lakini leo shangazi yangu kanipigia tu simu kaniuliza mnahamia lini imekuwa nongwa huyo shangazi yako anataka nini? anatulazimisha kuhamia dah nimebaki na maswali mengi sana. Wanawake bwana khaaa!
duh mwambie unaezeka kwa nyasi
 
Mada tulivu sana hii. Kwa haya Inakuwa hivii
Wanaume tunaweza kuwa wakatili sana au tukawa Wakarimu sana. Tunaweza kuwa wapole au wakali.
Kifupi huwa hatuchanganyi sana tabia zetu. Mara nyingi tunaweza kuwa moja ya mafungu hapo juu!

Mwanamke anaweza kuwa mpole sana lakini ndani yake akawa na roho ya ukatili, na huwezi kuiona
kirahisi. Anaweza akahifadhi chuki na usiione kwa miaka kadhaa. Na hapo ndipo sisi sasa tunaitwa Wanaume.
Jina hili lina maana kubwa sana: Kiongozi na Mtawala, na sifa za kiongozi ni kuonyesha njia. Na Mtawala
kuhakikisha kile kilichoamuliwa au kinachotakiwa kufanyika kinasimamiwa ipasavyo.
 
Back
Top Bottom