Mkuu
ngoswe umeongea point aisee ya vitu vinavyotokea katika familia zetu haswa maisha haya ya extended families ukizingatia katika familia moja ya watoto saba unakuta wamechomoka watoto wanne wengine wanaishi kwa kutegemea wakubwa zao na mwisho wa siku migogoro kwenye nyumba haiishi kwa kuwa unakuta binti ameolewa na ndio kwanza wengine wanaanzia maisha kwa mume anajikuta anajichanganya na watu wazima wengine (ndugu za mume) ambao hawajui background yao hivyo katika situation kama hii hata kama itatokea wamekwazana ndugu wa mume lazima watasema huyu anajifanya mjuaji sana kwa kuwa ameolewa na ndugu yetu na mke nae hawa wananifanya hivi kwa kuwa ni ndugu wa mume (kumbe ugomvi the same kama huo ungetokea kwa watu ambao hawana u-wifi au u-mama ukwe usingekuwa mkubwa)
Yote yanatokea kwa kuwa wasichana wengi katika mazungumzo kwa maeneo ambayo nimekuwa nikipitapita (mazungumzo baada ya habari, yale kiujumla), mara nyingi kuna kamsemo wanacho dada zetu yaani ukiolewa mama mkwe na wifi zako sio wa kuwachekea kabisa watakuharibia nyumba, kwa mtaji huu kama mtu atakuwa ameingia kichwani na wazo kama hili na wengi ndivyo wanaingia na mawazo haya lazima kitawaka tu hata kama mkwaruzano utakuwa wa kawaida kwani kila wanapoishi watu wazima hapakosi mikwaruzano ya hapa na pale.
Suruhisho: Ni kujenga familia zetu hasa watoto kuhakikisha kila mmoja akifikia umri wa 18 na kuendelea apende kuishi maisha ya kujitegemea ili wakati anakuwa awe anatambua kuwa ni jukumu lake kuhakikisha anakuwa na maisha yake mwenyewe pasipokumtemea mtu maana tumefika hapa kwenye magomvi ya mawifi na mama mkwe kwa kuwa na hizi extend families and of course sio kosa letu bali ndio mfumo wa maisha wa wazee wetu ambao wamekuwa wakiishi maana unakuta mdingi alipokuwa kijana ameanza kazi tu badala ya kujenga familia yake anajikuta anawatoa wadogo zake na wazazi wake kwa kuwajengea nyumba ya bati kutoka ya nyasi, at the time watoto wake wamekuwa wanahitaji support yake mdingi unakuta amechoka na wazee wetu enzi hizo akizaa watoto wachache watano na kati ya hao unakuta wawili ama watatu ndio ameweza kuwapatia full support wengine unakuta amechoka na amestaafu hivyo hiyo kazi anachiwa kaka mkubwa wa familia na ndio chanzo cha matatizo kinaendelea hapa (vicious cirle of poverty at family level).