Habari wana MMU,
Kuna jambo linanitatiza,Jana amekuja wifi yangu mke wa Kaka na kilio nikajua amefiwa
kumuliza haya kumezidi nini? anasema anataka kuachwa amesha choka na kuona msg
kwenye cm ya mumewe za mapenzi na hivi karibuni aliona msg na picha za mtoto
kwenye cm ya mumewe akafatilia mpaka akajua kama mumewe ana mtoto mwengine
sasa ame hama nyumba na anataka Talaka yake,hapo alipo yeye ni mkubwa kuliko
bro,ameolewa mwanzo ana watoto wa2 na akazaa wa3 na bro, nilicho mwambia
Astahmili alee watoto wake,hakuna ndoa yenye raha moja kwa moja leo tamu kesho chungu
na istoshe watoto wake anasomeshewa,maisha sio mabaya anayo ishi tatizo la mumewe ajitahidi
kumuomba mwenyezi mungu atatulia,anasema moyo wake hauchukui tena anataka talaka yake
na watoto wake wawili kawachukua lakini mmoja karudi anasema anataka kuishi na ndugu zake
nimemwambia wifi anipe mda bro amesafiri akirejea ntaongea nae lakini ameshikilia Talaka
Bro amesema Talaka sio Tatizo atampa aseme jengine, lakini waungwana mie staki waachane
sababu watoto watapata tabu,mama wa wifi nae nimeongea nae kanichamba utadhani mie ndio
nilomuoa mwanawe sasa hapa nimebakia njia ya panda hata lakumwambia akanielewa sinaaaa.
Naomba mnisaidie mawazo ili hawa watoto waishi na wazazi wao kwa salama na amani..