Wazo Langu
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 1,381
- 842
Katika maisha ya ndoa uzoefu ni muhimu katika kutoa ushauri. Katika mjadala huu unaweza kuhisi ni nani ameoa/kuolewa na ni nani ana ndoa changa (less than 10 years) au ni nani gwiji. Endelea na ushawishi wako ila hiyo ndoa inafika ukingoni. Kuwa na plan B kuhusu maisha ya hao watoto baada ya talaka. Ila akitoa talaka kaka yako ajiandae kwa machungu ya huyo mama na mama yake. Msumari wa moto atakuwa ameubeba. Nasema hivi ni bora mwanamke akakuchoka mwanaume, kwani kama bado anakupenda (kama huyo wifi yako bado anampenda kaka yako ila anatikisa kiberiti), ukimwacha cha moto utakachokipata unaweza hata jiua.
Hapo pa uzoefu napapenda!
Wifi yangu akitibuana na mumewe huwa anakimbilia kwangu na watoto wake.
Halafu anataka mimi nimpigie mume wake kuwasuluhisha. Naanzia wapi sina ndoa mimi.
Akazira eti 'watoto wenu hao hapo nimekuachia nikamwambia mimi sina muda watateseka tu hapa ila nitawapeleka kwa bimkubwa atawalea kama alivyotulea. Mimi na baba yao tutahudumia tusimchoshe mama.
Mbona alienda kunitangaza kwenye magroup yake huko eti nashabikia ndoa ya kakaake kuvunjika nimemnyang'anya na watoto.
Sijawahi kumuelewa alitaka nimshauri nini wakati ndoa yao wanaijua vizuri wenyewe.
Sasa na huyu wa watoto watano namuona walewale tu.