Uvumulivu huo unaotaka awe nao wifi yako ni wa aina gani?
Wifiyo kasema kachoka kuona message za wanawake katika simu ya mumewe,na kama haitoshi kaka yako kazaa nje kabisa.
Nimeshtuka kaka yako alipokubali kutoa talaka kirahisi.
Ni wazi amemchoka wifi yako ndio maana kashindwa hata kumficha mtoto wake wa nje.
Lengo lake lilikuwa hilo (mkewe aombe talaka) na limeshafanikiwa.
Wifi yako akiendelea kung'ang'ania hiyo ndoa atateseka sana.
Hivi kusomeshewa watoto ni nini?Ndoa maana yake ni makhaba yaliyokomaa yaliyopelekea ndoa.
Kama makhaba hakuna tena ndoa ya nini?
Jamani wanawake tuachane na hii kasumba ya kunga'ang'ania mateso kwa kigezo cha "kulea watoto, watoto watateseka"
Kama hakuna mapenzi tena katika ndoa hakuna cha zaidi ya kuachana.
Ni kweli, lazima apate tabu ya kuishi bila mume na watoto bila ya baba lakini amani ya moyo ni zaidi ya yote,mwisho wa siku maisha lazima yaendelee.
Period