Mwanamke jifunze uvumilivu

Mwanamke jifunze uvumilivu

Nifah i can undestand your point of view lakini hiyo mateso anayoteswa yeye ni yepi? kwanza kilimtuma nini kufungua cm ya mumewe na kupekura? mume hakumwambia kama ana mtoto nje yeye ndio kaenda kuyatafuta na mamake mpaka wakayajua na pia sio sababau he is my bro ndio namtetea lakini na yeye pia wifi yangu ana mapungufu yake as a human
mfano Nifah Being mama mwenye nyumba au mke kweli mumeo anaamka na watoto kwenda kazini wewe umelala?
sio kama una umwa mzima,wewe zako ni Harusi sijui maulidi mara kwenye kufunda mwari upeleke sanduku mda na mume
hunaaaaa yote sawa ameyakubali tulia basi ulee wanao unataka Talaka sijui kama amefikiria sana ila kwangu sitopenda itoke hata kidogo...
My dear,hakuna mateso makubwa kama yale ya moyo.
Huyo ni mtu mzima, mama wa watoto watano anajua nini anafanya.
Nafikiri busara ni kukaa pembeni... Waachie ndoa yao.
Kama angetaka suluhu yapo mabaraza ya usuluhishi na sio wewe.
 
Habari wana MMU,

Kuna jambo linanitatiza,Jana amekuja wifi yangu mke wa Kaka na kilio nikajua amefiwa
kumuliza haya kumezidi nini? anasema anataka kuachwa amesha choka na kuona msg
kwenye cm ya mumewe za mapenzi na hivi karibuni aliona msg na picha za mtoto
kwenye cm ya mumewe akafatilia mpaka akajua kama mumewe ana mtoto mwengine
sasa ame hama nyumba na anataka Talaka yake,hapo alipo yeye ni mkubwa kuliko
bro,ameolewa mwanzo ana watoto wa2 na akazaa wa3 na bro, nilicho mwambia

Astahmili alee watoto wake,hakuna ndoa yenye raha moja kwa moja leo tamu kesho chungu
na istoshe watoto wake anasomeshewa,maisha sio mabaya anayo ishi tatizo la mumewe ajitahidi
kumuomba mwenyezi mungu atatulia,anasema moyo wake hauchukui tena anataka talaka yake
na watoto wake wawili kawachukua lakini mmoja karudi anasema anataka kuishi na ndugu zake
nimemwambia wifi anipe mda bro amesafiri akirejea ntaongea nae lakini ameshikilia Talaka
Bro amesema Talaka sio Tatizo atampa aseme jengine, lakini waungwana mie staki waachane
sababu watoto watapata tabu,mama wa wifi nae nimeongea nae kanichamba utadhani mie ndio
nilomuoa mwanawe
sasa hapa nimebakia njia ya panda hata lakumwambia akanielewa sinaaaa.

Naomba mnisaidie mawazo ili hawa watoto waishi na wazazi wao kwa salama na amani..
Hapo pekundu shida tupu. Juzi niliona documentary ya Crime Investigation ambayo binti alimuua mmewe kwa vile wazazi wa binti hawakupenda aolewe naye-Wamarekani. Hili la akinamama kug'ang'ana kwa kuoverdefend mabinti zao ni shida sana katika mahusiano. Ikitokea kama huyu wako lazima unyoshe mikono. Piga ua talaka ipo mlangoni, cha maana jaribu kufikiria jinsi ya kusaidia hao watoto wa kaka yako ili maisha yaendelee bila baba na mama kuishi wote.
 
Halafu kama mwanamme haja kwambia kama ana mtoto nje na mahitaji yako unapata una mtafutia nini huyo mwanamke
ili iweje? na mama wengine nao mwenyezi mungu atunusuru sio anamwambia mwanawe ondoka isiwe tabu...
Mamy mama Na mwana hapo akili zao zimejaa pumba

Asikwambie mtu maisha unayoyaishi kuna mwenzio anayatamani uondoke Leo ufe Leo akae yeye

Uvumilivu ndio ngao ya msingi

Sasa s kishajua ana watoto Na wanawe wanatunzwa atuliege

Mwambie kaka dini inaruhusu aoe huyo asizini coz zinaaa inaketa ufakiri
 
My dear,hakuna mateso makubwa kama yale ya moyo.
Huyo ni mtu mzima, mama wa watoto watano anajua nini anafanya.
Nafikiri busara ni kukaa pembeni... Waachie ndoa yao.
Kama angetaka suluhu yapo mabaraza ya usuluhishi na sio wewe.
Kama shangazi wa wale watoto lov na amekuja kunielezea niwajibu wangu kumsaidia japo kwa mawazo
huenda ana hasira na kama unavyojua kila binadamu na upeo wake wakufikiri na kuamua anapokua na tatizo...
 
Hapo pekundu shida tupu. Juzi niliona documentary ya Crime Investigation ambayo binti alimuua mmewe kwa vile wazazi wa binti hawakupenda aolewe naye-Wamarekani. Hili la akinamama kug'ang'ana kwa kuoverdefend mabinti zao ni shida sana katika mahusiano. Ikitokea kama huyu wako lazima unyoshe mikono. Piga ua talaka ipo mlangoni, cha maana jaribu kufikiria jinsi ya kusaidia hao watoto wa kaka yako ili maisha yaendelee bila baba na mama kuishi wote.
Ahsante mkuu.....
 
Uvumulivu huo unaotaka awe nao wifi yako ni wa aina gani?
Wifiyo kasema kachoka kuona message za wanawake katika simu ya mumewe,na kama haitoshi kaka yako kazaa nje kabisa.

Nimeshtuka kaka yako alipokubali kutoa talaka kirahisi.
Ni wazi amemchoka wifi yako ndio maana kashindwa hata kumficha mtoto wake wa nje.
Lengo lake lilikuwa hilo (mkewe aombe talaka) na limeshafanikiwa.
Wifi yako akiendelea kung'ang'ania hiyo ndoa atateseka sana.

Hivi kusomeshewa watoto ni nini?Ndoa maana yake ni makhaba yaliyokomaa yaliyopelekea ndoa.
Kama makhaba hakuna tena ndoa ya nini?
Jamani wanawake tuachane na hii kasumba ya kunga'ang'ania mateso kwa kigezo cha "kulea watoto, watoto watateseka"
Kama hakuna mapenzi tena katika ndoa hakuna cha zaidi ya kuachana.

Ni kweli, lazima apate tabu ya kuishi bila mume na watoto bila ya baba lakini amani ya moyo ni zaidi ya yote,mwisho wa siku maisha lazima yaendelee.
Period
Nifah watch your fingers! Watoto hawakutaka uwalete duniani, ni raha zako na huyo 'uliyekuwa' unampenda. Hivyo ni wajibu wako kuwafikiria kwanza baadala ya kujifikiria mwenyewe.
 
Mkuu sio salama lakini watu kugombana ni kawaida na wifi yangu hua akikasirika kidogo tuu niache,kuna siku driver wakupeleka watoto shule alikua anaumwa,sasa bro alikua safarini yeye yupo nyumbani hakupeleka watoto school siku4
mpaka driver amepona alipoja bro anamwambia kwanini usiwapeleke watoto shule? kasema nilikua na usingizi bro akamgombeza basi kafungasha nguo zake anamwambia talaka yangu nilete kwetu,sasa simuelewi mie huyu mwanamke
lakini inabidi tumchukulie nikamwambia bro nenda kamrudishe kwa ajili ya watoto...

Sasa kumbe mwanamke mwenyewe hazimtoshi. We waachie ndoa yao tu, maamuzi ni yao.
 
niwe mkweli tu akiwa finacially okey naishi naye na si kwamba namvumilia no naishi maisha kama vile nipo na business partner ndani .. aniguse asiniguse atajiju .. nitakapo mbana ni matumizi ya home na watoto wasome shule nzuri.. uhuni wanafanya ila akishatakiwa kutoa milioni kumi kwa mwaka akili itamkaa sawa.... sema kama hana uwiii nijiweke pembeni sababu soon ataniletea mizigo yake
Huo ndiyo ukomavu na ukikuta mwanamama aliye na misimamo kama wako, jua mama yake si mshwahili. Mama yake anajaribu kumfunda ili ashikamane na ndoa yake kwa faida ya viumbe ambavyo kwa kukata viuono vyetu na kale kautamu tunavileta hapa duniani masikini ya mungu.
 
Mamy mama Na mwana hapo akili zao zimejaa pumba

Asikwambie mtu maisha unayoyaishi kuna mwenzio anayatamani uondoke Leo ufe Leo akae yeye

Uvumilivu ndio ngao ya msingi

Sasa s kishajua ana watoto Na wanawe wanatunzwa atuliege

Mwambie kaka dini inaruhusu aoe huyo asizini coz zinaaa inaketa ufakiri
Kwa mujibu wa huyu wifi anasema mtoto ni wa bro ila bro anasema mtoto sio wake
na kama ana shikilia mtoto ni wake yeye sasa mpaka hapo bado tuuu?
yani sijui ana tatizo gani lakini akikazania atajua mwenyewe...
 
Huo ndiyo ukomavu na ukikuta mwanamama aliye na misimamo kama wako, jua mama yake si mshwahili. Mama yake anajaribu kumfunda ili ashikamane na ndoa yake kwa faida ya viumbe ambavyo kwa kukata viuono vyetu na kale kautamu tunavileta hapa duniani masikini ya mungu.
nakubaliana na wewe,, tumekuwa wabinafsi mnoo any way marriage as a project
 
Kwa mujibu wa huyu wifi anasema mtoto ni wa bro ila bro anasema mtoto sio wake
na kama ana shikilia mtoto ni wake yeye sasa mpaka hapo bado tuuu?
yani sijui ana tatizo gani lakini akikazania atajua mwenyewe...
Mama ndio hujuaga mtoto baba yake Nani

Tena simamia hiyo ndoa isivunjike fungu lako utalikuta Kwa Allah
 
Kwa mujibu wa huyu wifi anasema mtoto ni wa bro ila bro anasema mtoto sio wake
na kama ana shikilia mtoto ni wake yeye sasa mpaka hapo bado tuuu?
yani sijui ana tatizo gani lakini akikazania atajua mwenyewe...
kwani huyo mtoto kaletwa home? kuna matumizi yamepungua hapo nyumbani? je anamdharau?
 
Tatizo hana mshauri mzuri,Mama yake ana mwambia ondoka atakuja kukupigia magoti mwenyewe kwani mwanamme yeye peke yake njooo nyumbani kwetu wakati nyumba wanayokaa ni ya Bro simuelewi huyu mama hata kidogo..
Mama wakwe wengine sijui!!!!!! ni janga
 
Tulia apewe talaka yake, ikifika episode 8 njoo utuambia kama hajarud analia au vip maana anaiga maisha ya tamthilia bila kujua wenzake wanaigiza tu.
 
kwani huyo mtoto kaletwa home? kuna matumizi yamepungua hapo nyumbani? je anamdharau?
Yani shosti kama ulikuwepo nimeuliza samethings kasema no yeye ameona msg kwenye cm ya mumewe na picha
za huyo mtoto ndio akachukua number ya cm na kuanza kumfatilia mpaka wamempata na still mumewe kamwambia sio mwanangu lakini yeye anasema ni mwanao hapo ndio yule bwana akamwambia usinichanganye niko safarini,mke nae akasema ukirudi Talaka yangu utaileta kwetu,ndio akaja kwangu kunielezwa.
 
Tulia apewe talaka yake, ikifika episode 8 njoo utuambia kama hajarud analia au vip maana anaiga maisha ya tamthilia bila kujua wenzake wanaigiza tu.
Inshallah asipewe atulie na mumewe..
 
Yani shosti kama ulikuwepo nimeuliza samethings kasema no yeye ameona msg kwenye cm ya mumewe na picha
za huyo mtoto ndio akachukua number ya cm na kuanza kumfatilia mpaka wamempata na still mumewe kamwambia sio mwanangu lakini yeye anasema ni mwanao hapo ndio yule bwana akamwambia usinichanganye niko safarini,mke nae akasema ukirudi Talaka yangu utaileta kwetu,ndio akaja kwangu kunielezwa.
ha hahaa any way mwache tu
 
Back
Top Bottom