Mwanamke huyu utamlaumu?

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,712
Kumbe wakati mwingine unaweza ukamsababisha mwenzi wako akakucheat!Sikia hii,.Mke ni mhasibu wa shirika la umeme tanzania Tanesco,mkoa wa Tabora(sio jina sahihi).Mumemi mwajiriwa serikalini,mume huyu amekua bize sana kiasi kwamba kumpata nyumbuni ni bahati labda usiku kuanzia saa 6 usiku.Kwa maelezo ya mkewe ni kwamba mumewe akifika huwa amechoka sana na wakati mwingine hali chakula ambacho mkewe hujitahidi kukipika hata kama nae huwa bize kiasi gani,amejiwekea utaratibu chakula cha usiku lazima apike yeye.Siku ya tukio mumewe alikua amesafiri kwa muda mwezi na nusu kikazi Dar,siku aliyotakiwa kurudi alimpigia mkewe simu kuwa atapitia Shinyanga kwenye semina itakayochukua siku mbili,lakini alipofika Shinyanga akapewa taarifa kuwa semina imeahirishwa,ikabidi ageuze kurudi Tabora,alipofika Nzega akakumbuka hajamjulisha mkewe dharula iliyojitokeza,akaamua kumpigia mkewe simu,lakini ikawa haipatikani,alifanya hivyo mara kadhaa bila mafanikio,akaamua aende tu,kabla ya kufika nyumbani akamkuta mkewe akifanya ngono na kijana ambae anaishi jirani na pale.Ulitokea mtafaruku watu wenye busara wakalizima zogo lile.Yule bwana akasema hamuitaji mkewe,ila wakashauriwa waende kanisani kutatua mzozo kwani walikua ni watu wazima!Kweli walienda ndipo mkewe yule bwana alipofunguka na kudai mumewe amekua hampi haki ya ndoa na kama akimpa ni mara moja kwa wiki mbili na hata hiyo mara moja siyo ya kuridhisha,alipoulizwa mumewe alikubali lakini akadai ni ubize kazini ndo chanzo!Bahati nzuri padri aliwaelesha makosa yao wakaombana msamaha yakaisha.Sasa huyu mwanamke ana makosa?Inawezekana alikosea kufanyia home lakini chanzo cha tatizo ni mumewe!So kucheat kwingine kuna mashiko!
 
Hivi ndugu yangu mtoa mada hebu fikiria angekuwa mkeo ingekuwaje?kama hujaoa huwezi kujua uchungu wa mke,uzinzi wa aina yeyote haufai kabisa!
 
Hilo alilofanya ni kosa hata kama mumewe hamridhishi au hamfikishi anapotaka, wameowana mda gani mpaka leo awe hafikishwi? kwanini asikae na mumewe akamueleza nini anataka afanyiwe kwenye mapenzi.
 
Huyo mama haikuwa mara ya kwanza kufanya hivyo. Ilikuwa ni kawaida yake tena kwa watu mbalimbali hapo tu ilikuwa ni arobaini. Dawa ni kumtosa moja kwa moja maana hawezi kuacha uzinzi tena ataendelea tu. Hata kama ataacha bwana ataamini vipi tena.
 
Wote wana makosa,
Ila kwa hili namlaum zaidi mke,
Tunaamin siku no matter wat hata km wanaume ndio vichwa vya familia but lzm kichwa kishikiliwe na shingo,
Km mke ameona hapewi haki ya ndoa suluhisho sio kutafuta bwana,
Kwann hakuenda japo kushitaki kwa hao viongozi wa dini kuliko kwenda kujiabisha kwa kujielezea 7bu za uzinzi wake?
KM imetokea amejua mapungufu ya mumewe angetafuta njia halali kurekebisha sio kufanya jambo akidhan anamkomoa kumbe anajidhalilisha mwenyewe.
 
So kwa kuamua kumeguliwa kando ndiyo alikua anaziba viraka ili ndoa iendelee kudumu au ?
 
Cheating haina justification.

Unaweza kuamua kujiziba macho yako na kuamua kuacha kuangalia upande wa pili,usiseme tu kuwa cheating haina uhalali na kuamua kuamini hivyo,angalia tatizo lilipoanzia kwanza!
 
Hivi ndugu yangu mtoa mada hebu fikiria angekuwa mkeo ingekuwaje?kama hujaoa huwezi kujua uchungu wa mke,uzinzi wa aina yeyote haufai kabisa!

Suala sio mke wangu ama la,hata mtu anapoua,mahakama inatazama mazingira yaliyosababisha mauaji yakatokea!Wakati mwingine watuhumiwa huachiwa huru!
 
Hilo ni pepo la ngono tu. Kwani aliwahi kuchukua juhudi gani kupata suluhu ikashindikana hadi aamue kumegwa tena home? Kimeo hiko!!
 
Canta,fine mke alifanya kosa sijakataa,lakini linapotokea tatizo kumbuka namna ya kulitatua kwa usahihi huwa anajua yule ambae hajapata tatizo,huyu mama ni sawa na mtu mwenye njaa anaangalia chakula kitakachokua karibu nae,suala la usalama wa hicho chakula linakuja baadae!Lakini kama chakula hicho kama kina madhara yatampata tu,haijalishi kama ilikua no way out,lakini linapokuja suala la chanzo mwenye kujibu ni yule ambae hakumpa chakula mhusika ikapelekea akapata njaa kali iliyomfanya atafute chakula chochote!
 
Kuna mengi hayajulikani hapo. kwa mtizamo na uzoefu wangu, wanawake haswa wale wanaoitwa mavuvuzela kwa sababu they speak their minds out, huwa wanatoa warnings za kutosha kabla ya kufanya lolote. ataanza kumuambia mumewe kwa mapenzi, ikishindikana atamuonya kwa upole. kusipokuwa na mabadiliko ataongea kwa ukali (vuvuzela stage), ikishindikana ananyamaza kimyaa na mhusika anadhani yameisha kumbe yamepamba moto.
wanaume: kati ya maneno meengi anayoongea mkeo, between the lines kuna lugha. jitahidi uielewe, itakusaidia sana. ukiambiwa kitu leo, kesho na keshokutwa anza kujistua basi! hata kama ni kuhusu viatu vya shule, onyesha ushirikiano!:A S embarassed::A S embarassed:
 
King'st,nakubaliana na wewe,ila faham kuwa mwanamke alishalalamika lakini si unajua sisi wanaume ubabe mpaka kwenye mambo yasiyohitaji ubabe.Anakugusa unaropoka"we nawe hakuna kingine unachofikiria?Mi nimechoka niache nipumzike"!
 
Watu wana huruma sana duniani ingekua mimi hata angekuja papa john wa ii(rip) na papa benedicto wa 16 asingeweza suruhisha huo mgogoro,yani hapo hapo ni kwao namrudisha
 
Back
Top Bottom