Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,676
8,209
Wakuu story ni kwamba huyu jamaa kwenye picha amemuua huyo mkewe usiku wa kuamkia leo huko Mwanza ikidaiwa ni baada ya kumkataza mkewe asiende kwenye show ya Mondi.

Baada ya kumwambia asiende kwenye hiyo show ya Nasib Abdul, mke akakaidi akaenda.

Jamaa amempiga risasi saba za kichwa na inasemekana na yeye kajiua japo maiti yake haijaonekana.

Ila na nyie Wanawake mpunguze visirani. Inaonesha jinsi huyu Marehemu alikuwa mkaidi na hamsikilizi Mme wake.

Mme kakuambia sitaki uende pahala fulani then wewe unakaidi ni nini kama sio dharau na kiburi?

By the way anything else Happen for a reason.

RIP Binti Mzuri


==================================

Baada ya kifo cha Swalha Salum kilichotokea Mei 28, 2022 maeneo ya Busweli Jijini Mwanza, Mama mzazi wa marehemu, Bi Tiba Mohamed anasimulia kilichotokea kuhusu ndoa ya mwanaye na mumewe, Said Oswayo ambapo wahusika hao wamedumu katika ndoa kwa muda wa miezi mitano, kwani walifunga pingu za maisha Desemba 30, 2021.

Anasimulia: “Watoto wangu waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

“Alikuwa akinitania kwa kufurahi kuwafunga Simba akawa anishawishi na mimi nihamie Yanga (Yanga iliifunga Simba bao 1-0 siku hiyo kwenye CCM Kirumba Mei 28, 2022).

“Baadaye baba yake akapiga simu na kusema mume wa Swalha amepiga simu kumjulisha kuwa amefika na hivyo Swalha aende akampokee Igombe.

“Swalha akasema gari yake haina mafuta, hivyo wakakubaliana wakutane nyumbani na mwanaume akasisitiza kuwa ana njaa sana, akamtaka mke wake aende akampikie.

“Nikawasindikiza hadi barabarani mida ya saa moja usiku, muda huohuo mume wake akapiga simu akiwa anafoka, nikamtaka awe na subira mkewe anakuja yupo njiani.

CHANZO CHA UGOMVI
“Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.

“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.

“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.

“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.

“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.

“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.

KUHUSU KUPIGWA RISASI
“Taarifa ni za kweli, pale ndani (wanapoishi Swalha na mumewe) kulikuwa na watoto watatu wametuambia risasi zilipigwa.

“Wanasema huyo baba alikuwa na kawaida ya kuijaribu silaha yake, mara nyingine anapiga hewani, hivyo walivyosikia mlio wa risasi wakaendelea kulala.

“Ni hadi waliposikia Swalha amepiga kelele mara moja tu lakini risasi zikawa zinaendelea kupigwa. Mtoto mmoja akaenda kusikiliza mlangoni kwa Swalha kisha akatoka mbio kwenda kuwataarifu majirani.

“Wakaenda Polisi, kumbe yule mtoto alivyotoka tu yule baba naye (mume wa Swalha) akaondoka. Polisi walivyofika wakauchukua mwili wa Swalha.

“Taarifa za tukio sisi tulianza kuzipata kutoka Kisiwani huko anapofanyia kazi (mume wa Swalha), ndipo majirani wa Swalha na askari wakaja kutoa taarifa wakisema mwanangu ana hali mbaya ameshambuliwa kwa risasi.

“Baba Swalha akaondoka na ndugu zangu kwenda huko maana nilibaki nyumbani, niliishiwa nguvu baada ya taarifa hizo, nikashindwa kwenda, saa tisa usiku wakarejea na ndipo nikajulishwa kuwa Swalha ameshafariki dunia.

“Marehemu hakuwa na mtoto na sijajua nini kinaendelea mpaka sasa.

“Kuhusu huyo mume wake haijulikani yuko wapi, kwani Polisi mara ya mwisho walisema wameangalia simu yake ikaonekana yupo maeneo ya Tunza.”

JESHI LA POLISI LINAMSAKA MTUHUMIWA
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.

Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.


MUME NAYE AKUTWA AKIWA AMEFARIKI
Said Oswayo anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mkewe, Swalha Salum ikidaiwa alimuua kwa kumfyatulia risasi kadhaa amekutwa amefariki na mwili wake kuokotwa kando ya Ziwa Victoria katika Ufukwe wa Rock Jijini Mwanza, leo Mei 30, 2022

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amesema: "Mwili umekutwa kandokando ya ziwa na umetambuliwa na mmoja wa ndugu zake. Umekutwa na tundu kichwani."

"Inavyoonekana hajafia hapa, aliletwa na maji, inasadikika amejiua kwa risasi lakini uchunguzi unafanyika na tutatoa ripoti kamili."


A509D724-CD33-46F7-9CBF-0757E971683A.jpeg

IMG-20220529-WA0146.jpg

IMG-20220529-WA0141.jpg
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
11,122
21,450
Kupata mwanamke anaekusikiliza na kukuheshimu kama baba yake ni baraka kubwa sana ambayo wengi wanaikosa katika kizazi hiki, Asante Mungu.

Muda mwingine sisi wanaume tunashindwa kusimamia uanaume wetu, hivi Mungu kakujalia Pesa na afya ya nini kung'ang'ania mwanamke anaekuumiza akili?? Najua mapenzi yanauma na pengine labda kuna watu wapo humu JF muda huu wanapitia fukuto la mahusiano, nawashauri mfanye maamuzi ya kiume kabla hamjachelewa.

"Every woman in any given reletionship, is taken as the man's project".

Project imekushinda, achia wengine wahangaike nayo kwanini uumie?
 
53 Reactions
Reply
Top Bottom