Mwanamke anapokupa masharti.

Mambo mengine ni kuendekeza ujinga wa mtu. Kwa hiyo kuondoka kwake ndiyo ww utishike? Huyu mwanamke anaonekana ana alergy na wageni. Si akae mpaka mwisho athibitishe kama kweli unatembea naye? Kwa hiyo ndani ya hiyo nyumba mtakuwa hampokei wageni kisa mke ataondoka?? Hii imenisikitisha sana hata kam wivu hii naona imepitiliza.




hapana
tatizo unalo kaka
ULIMWELEWESHA MAPEMA kuna mgen anakuja/
mazngra mnayoongea na mgen yanaruhusu?
isije ikawa muda woote ulkuwa chumban kwa mgen..wala hamkai seblen...mnakaa kwa raha zenu...mkeo lazima akil imsimame..


nachokiona ;ulimjengea mazngra tata kwa mkeo...mfate mkeo
nb;uenda una kashfa km iz so ulivyomleta demu mkeo akaona yale yale...

mgen mpangie sehemu
 
Inaonekana kwa wakati wote wa ndoa yenu humthamini na kumheshimu mke wako, mara nyingi umekuwa humsikilizi ndiyo maana aliamua kuleta message kwako by action ya kuondoka. Hivyo JIFUNZE kumsikiliza na kumheshimu mke wako, sikiliza hisia zake.

Wanawake na sisi sometimes tuna hila sana bwana, na kosa walifanyalo wababa anaona kabisa hapa mke wangu anakosea ila anaignore tu badala ya kuikataa hiyo hali matokeo yake mwanamke anaona ndio mchezo na anaifanya kuwa tabia yake ya kudumu
 
Hekima ni ki2 muhimu sn kwenye ndoa. Siamini kuwa huyu msichana hakuwa mshikaji wako mkiwa shule. Mgeni wa namna ile ulitakiwa kumtolea maelezo kabla hajafika kwako na uone kama somo linaeleweka kwa mkeo. ukiona halieleweki tafuta njia nyingine sio lazima alale kwako. wanawake pia ni wanadamu. Jiulize ungekuwa wewe ungekubali lijianaume kulala kwako kisa alisoma na mkeo. Mtafute mkeo muombe radhi haraka sana
 
Wanawake huwa wana makusudi sana. Naomba nikwambie kitu kimoja tu, acha mkeo aende mgeni akiondoka atarudi tu mwenyewe.
Nakuhakikishia atarudi mwenyewe, mkarimu mgeni mpaka atakapoondoka.
 
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf


...inaelekea tayari mlishakuwa na tatizo la mkeo kutokukuamini tangia awali.
Hili la Mgeni limekuwa kichocheo tu.

Badala ya kumlaumu Mke, mpangishie mgeni nyumba ya wageni (ni ukarimu tosha,)
kamtafute mkeo arudi Nyumbani.

Jitahidi Uutafute mzizi wa mgogoro huo, uung'oe!
Hayo si maisha!
 
GERVASE

inaonekana hukumshirikisha mkeo kwenye swala la ujio wa mgeni
au kama ulimshirikisha basi hakuafiki.
pia, inawezekana aliondoka baada ya kusense kitu kinaendelea kati yako na huyo mgeni..

lakini jamani twende mbele turudi nyumba ..iweje umlete mgeni wa jinsia tofauti kwako ili hali unafahamu fika sie wanawake tuna wivu hata kama hakuna kinachoendelea baina yenu..je yeye angeleta rafikiye wa kiume wewe ungereact vipi?mambo mengine ya kujitakia tu.
hajafanya vizuri kuondoka huyo mkeo itakuwa ni hasira tu na inategemea pia uliongea nae vipi kuhusu hilo swala.
kwani hakuna guests huko ulipo?ungewaza kumpeleka huko kabla hujamkaribisha kwako.

nenda kamtafute mkeo mpeleke huyo mgeni guest.kutokujua mtu mahali haimaanishi hautosurvive.utaharibu ndoa kwasababu ya kitu kidooogoo.Goodluck
 
Mama B hiyo mizigo ikisafiri mnaichungaje? na je mnafahamu huwa inakutana na akina nani huko safarini?Ndio maana sisi wengine tuko reluctant kuingia kwenye hii institution ya ndoa kwani imani hamna kabisa. Looks like jamaa ailkuwa na nia nzuri tu ya kumsadia mgeni, jamani huyu mtu kalipoti kituo cha kazi kijijini siwezi kuimagine hali ilivyo huko so alihitaji mwenyeji ambaye ndio huyu kaka Mungu kamtumia. Does this mean tukioa au kuolewa tuache kusupport wale tunaowafahamu simply because ni opposite sex? Kama ndivyo basi kuoa au kuolewa ni bullshit, there is no meaning in it completely. Humu duniani we need each other wandugu kama si leo basi ni kesho.

Haya mambo Bobby yanataka moyo la sivyo waweza kufa na pressure panapowezekana unachukua tahadhari mapema ndg yangu but all in all ni kazi sana inapaswa mtu mwenyewe ajue nini ananachokifanya akiongozwa na hofu ya Mungu.
 
Fukuza haraka huyo mgeni, nenda katafute mkeo haraka sana!nasisitiza tena haraka sana usilete mchezo na ndoa!

Mmm siyo vema kumfukuza mgeni kirahisi namna hiyo.Kwani kosa lake liko wapi?Mimi naona umwambie hali halisi na yeye kama ana busara atahama mwenyewe
 
unatakiwa kufahamu ya kuwa jamii ni ya males & females, kwahiyo wewe hutatakiwa kuwa na wageni wa jinsi yake maishani kama hutasimamia ukweli wako. You are head of a family, make a reasonable decision
 
Huyo ni ubavu wako umpende, umjali, umtunze katika raha na shida, ila muishi nao kwa maarifa kwani mara zote ni kama watoto wenu, pia msiwachokoze, wewe umemchokoza mkeo, jitahidi uyamalize.
 
Jifunze kumshirikisha mkeo kabla ya kufanya maamuzi,unakaribishaje mgeni bila makubaliano na wife? Na huyo mgeni nina wasiwasi haku-behave vizuri mbele ya mwenye nyumba. Mgeni akatafute pa kukaa bwana usingekuwepo wewe huko asingeripoti huko kazini? Hebu kamtafute mkeo umuombe radhi.
 
Huyo mwanamke mcharuko tu, leo anakimbia nyumba yake kwa sababu ya mgeni wako, kesho ataondoka kwa sababu ya mama yako. achana na naye huyo ana bakila wala busara hana. Ana kudhalilisha huyo.
 
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf

Kwa kiasi fulani kwa kufikia kukutext kwa mtazamo wake tu, mke wako ana vituko ila nawe pale pale ulikuwaja umjibu kama hivi "nafurahia uwepo wako ktk ndoa hii".
Lkn subiria mara nyengine. Mtu mzima hatishiwi nyau ujuwe.
 
Unasema mke wako katoweka? na yeye hajakuoga anakwenda wapi! Inawezekana
1. Wewe mke wako hakuamini kwa sababu ya tabia zako,
2. umeleta mgeni wa kike home bila ya kumweleza mke wako ( hayo ni matusi kabisaa kwa mke) je wewe mke akikuletea mwanamume home halafu anakwambia analala hapa hadi apate nyumba, ingekuaje? c vita ni vita muraaaa!
3. Ingetakiwa umweleze mkeo kwamba huna mahusiano na huyo mwanamke sio utueleze sisi, sasa mpigie simu na umweleze hivyo na umwambie huyo mgeni aondoke (kwani wa muhimu ni nani? mgeni au mkeo? tunza nyumba yako dogo acha ujinga
4. Inawezekana wewe huna mazoea au siyo mtu wa kuzungumza na mkeo kwa ustaarabu ndo mana alikutumia sms tu na akaondoka
5. Inawezekana mke wako alishakuvumilia kwa muda mrefu na sasa anataka akuache na huko alikoenda unatakiwa upajua kwa haraka sana
6. inawezekana mke wako anataka akupime je una msimamo gani? hasa la kuhusu familia yako, na je yeye unaweza kumsikiliza?

Cha msingi mpigie simu mkeo, mwombe arudi nyumbani na umkalishe na huyo mgeni wako! mweleze haya uliyotueleza halafu mwombe mkeo ruhusa ya mgeni kukaa hapo nyumbani. Inawezekana alishaona dalili mbaya kati yako na huyo mgeni wako! Kama hataki basi mwambie mgeni akunje viroba vyake atambae. Wanseama between two evils choose the lesser kaka! Tumia akili kama za mbayu wayu ooh!
 
hapa tatizo sio mgeni au mgeni kuwa jinsia nyingine.. tatizo alimpa mkewe taarifa kama kutakuwa na mgeni wa aina hiyo???
Hapa duniani kila kitu hutokea kwa sababu. Kuwa kwako na raha leo usione kwamba umefika na kusahau shida za wenzako. Huyo kaka alisoma na huyo dada na kwa kuwa wanafahamiana aliomba afikie hapo. Na kwa jibu wa Gervace hajatuambia kuwa huyo mgeni alifika bila taarifa au lah!! Jamani kuweni wavumilivu msianze kuhukumu maisha mnayajua hasa mtu anapoenda kuanza kazi. Na pia mwanamke kwa upande mwingine ataondokaje nyumbani alafu atume message kwenye simu? Kama kweli yeye ni genuine kwa nini asikae chini ajadiliane na mumewe? Asije kuwa alikuwa anatafuta sababu siku nyingi ya kuondoka kwa huyo mumewe na hii ndiyo kaipata. Kingine ni rahisi sana kusema fukuza bila kuangalia madhala ya upande wa pili.
 
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf

Kipimo kizuri....jaribu kunagalia mazingira ya kuja kwa/kumleta huyo 'mgeni' halafu fikiria kama ingalikuwa ni mkeo ndio kafanya kama ulivyofanya wewe (i.e. kuleta mgeni wa kiume kwa utaratibu uliofanya wewe), je unadhani ungajisikia poa tu? Kama jawabu ni la, then fanya hima kumtafutia mgeni wako mahala pengine ili uponye ndoa yako. Mwenyewe ushasema huna 'mpango nae', sasa usitake aharibu nyumba yako!
 
Mke asingeondoka nyumbani kuna mazingira fulani yameleta hofu...pia amefikiria mbele zaidi kuwa uwezekano wa huyu jamaa kumfanya mgeni nyumba ndogo upo ukizingatia alishaona dalili za kuwepo harafu ya uhusiano..sidhan kama mke aliridhia kuja kwa mgeni huyu wa kike...nadhan jamaa alitumia ubabe kumleta mgeni na kumlaza pale..mambo mengine ni ya kuepuka yanaleta usumbufu usiotarajiwa..kama ilikuwa siku moja tuu kwani hapo kijijin kwenu hakuna hata nyumba za wageni?...guest house? au ungemuombea hata kwa jirani ambaye ni bachela nadhan ungeepusha hayo yote yaliyotokea..mkeo ameona humheshimu pia huheshimu ndoa mpaka umefikia hatua ya kumleta mgeni ya kike asiemfahamu vizuri hana hata undugu na wewe na kumlaza nyumbani.
 
Dada hajiamni sasa kwanini kaondoka ndio nini ama ndio anatoa picha gani?.kwasababu kama mtu anataka kufanya lake ndio umempa nafasi kwanini aonyeshe udhaifu hivyo,na kingine wanaweke huwa tuna tabia mbaya ukiona mwenzio amekuzidi kila Idara tunajinusha bila sababu na kutafuta visa vitu vingine vina hitaji uwe na busara sana sio kukurupa tu.
 
mimi kwakweli sikubaliani na hili swala we baba hebu fanya mpango huyo mgeni atimue haraka sana mbona sisi wanawake wa ndoa mnatuonea sana jamani, mimi ilishawahi kutokea nilimkaribisha vizuri na chakula cha usiku nikapika msosi wa nguvu huyo mgeni alikuwa anaingia jioni kweli nilimkarimu,sasa baada ya two day's nilikuta msg ya ushenzi kwenye cm ya husband jamani kilichoendelea naona yule dada atanisahau maisha yake yoye maana,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mh!
 
Back
Top Bottom