Mwanamke anapokupa masharti.

gervase

Member
Jan 23, 2011
41
5
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf
 
Inawezekama ameona mazingira ambayo yamemtatanisha kati yako an huyo mgeni. I believe huyo si mgeni wa kwanza hapo nyumbani kwako. If that is the case, fanya utaratibu huyo mgeni umtafutie mahala pengine pa kulala (Guest house) ili uondoshe rabsha na mkeo!
 
mkuu hebu fafanua maana kuna utata hapo:

huyu dada alipofika ulimtambulilsha kwa mke si ndio?...........na kabla ya kuja huyu dada naamini alitoa taarifa sio?...........je ulimwambia mkeo kuwa kuna mgeni anakuja?

Sikatai yule mwenye kuonyesha wivu ndio mwenye mapenzi ya kweli kwa mwenzi, lakin pia uvumilivu na vitendo vyenye karaha huenda vinamuumiza mkeo, kama wewe ni mtulivu na kuiba mali ya mtu huijafunzwa. . Fikira zake mkeo ziko vibaya kwa kuzani ya kwmba huyo demu unampenda. unless huko nyuma mlikuwa na ugomvi kabla ya huyu dada kuja.......cha kufanya fanya utaratibu huyo dada aende alikopangiwa......

Fuata ushauri wa kwenye post 2. Mkewako ni muhimu kwako kwa sasa kuliko huyu mgeni, hasa unaposema huna mpango naye. Mweleze mgeni wako kinachoendelea kati yako namke wako. Ikiwa ni mwenye kufahamu ataondoka kabla ya kuambiwa aondoke na bado urafiki wenu utaendelea.
 
Wanawake wa aina ya mkeo ni wasumbufu tu....

Subiri mgeni aondoke,huyo mkeo atarudi mwenyewe..

But kwanza mkaipime ukimwi....

Huko aliko anafikiri anakukomoa kwa kutoka nje......

Mwanamke anayejiamini hawezi kukimbia nyumba yake kwa sababu ya mgeni wa kupita...
 
  • Thanks
Reactions: Iza
mke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Kaa kimya mgeni aondoke ukionyesha rabsha basi mkeo kila leo atakuwa anakutisha nyau. Take it from me, am a woman.
 
mke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Kaa kimya mgeni aondoke ukionyesha rabsha basi mkeo kila leo atakuwa anakutisha nyau. Take it from me, am a woman.

Haya mawazio ya kizamani Bi Mkubwa.

Enzi hizi za maradhi ukiyashika hayo watoto yatima watazidi kuongezeka.

Women follow your instincts kama una mume mkware, asiyeeleweka mambo yake/asiyemuwazi. Kama baadhi ya wanaume wanaweza kuwalala binti zao au wasaidizi wa kike wa majumbani, ije kuwa 'mwanamke aliyesoma nae'
 
Umeyataka mwenyewe na wewe.. Mtu umeoa, bado unakaribisha visichana kuja kulala kwako? Acha wema wa kijinga.. Usingekuepo hapo kijijini asingeanza hiyo kazi? Mtafute mkeo umuangukie!
 
Wanawake wa aina ya mkeo ni wasumbufu tu....

Subiri mgeni aondoke,huyo mkeo atarudi mwenyewe..

But kwanza mkaipime ukimwi....

Huko aliko anafikiri anakukomoa kwa kutoka nje......

Mwanamke anayejiamini hawezi kukimbia nyumba yake kwa sababu ya mgeni wa kupita...

Mambo mengine ni kuendekeza ujinga wa mtu. Kwa hiyo kuondoka kwake ndiyo ww utishike? Huyu mwanamke anaonekana ana alergy na wageni. Si akae mpaka mwisho athibitishe kama kweli unatembea naye? Kwa hiyo ndani ya hiyo nyumba mtakuwa hampokei wageni kisa mke ataondoka?? Hii imenisikitisha sana hata kam wivu hii naona imepitiliza.

Sasa Mkuu unamkaribishaje mgeni wako wa jinsia tofauti bila kushauriana na Mkeo ili akupe baraka zake au la!?
 
Fukuza mgeni kamtafute mkeo mimi ni mwanamke pia na imeshawahi kunitokea, ni upuuzi kukaribisha mtu asiye ndugu wa tumbo moja. ten fukuza haraka sana! la sicyo unaharibu ndoa yako.
 
Mambo mengine ni kuendekeza ujinga wa mtu. Kwa hiyo kuondoka kwake ndiyo ww utishike? Huyu mwanamke anaonekana ana alergy na wageni. Si akae mpaka mwisho athibitishe kama kweli unatembea naye? Kwa hiyo ndani ya hiyo nyumba mtakuwa hampokei wageni kisa mke ataondoka?? Hii imenisikitisha sana hata kam wivu hii naona imepitiliza.

Kuna wageni na wageni lakini siyo mgeni wa jinsia tofauti eti kisa wamesoma naye, wema wema mwisho itakuwa balaaa afukuze kabisa huyo geni aende alikopangiwa kama awasingekuwepo hapo huyo mgeni angefanyaje?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mama hajiamini , na huyo mdada inategemea ana behave vipi? Wadada wengne ni wapana kama mapazia majumbani kwa watu. Kosa la mama ni kukimbia nyumba. Tafuta mama mweleweshe vizuri. Na huyo binti akae mbali na wewe. Usije haribu nyumba.
 
Kuna wageni na wageni lakini siyo mgeni wa jinsia tofauti eti kisa wamesoma naye, wema wema mwisho itakuwa balaaa afukuze kabisa huyo geni aende alikopangiwa kama awasingekuwepo hapo huyo mgeni angefanyaje?

Hapa duniani kila kitu hutokea kwa sababu. Kuwa kwako na raha leo usione kwamba umefika na kusahau shida za wenzako. Huyo kaka alisoma na huyo dada na kwa kuwa wanafahamiana aliomba afikie hapo. Na kwa jibu wa Gervace hajatuambia kuwa huyo mgeni alifika bila taarifa au lah!! Jamani kuweni wavumilivu msianze kuhukumu maisha mnayajua hasa mtu anapoenda kuanza kazi. Na pia mwanamke kwa upande mwingine ataondokaje nyumbani alafu atume message kwenye simu? Kama kweli yeye ni genuine kwa nini asikae chini ajadiliane na mumewe? Asije kuwa alikuwa anatafuta sababu siku nyingi ya kuondoka kwa huyo mumewe na hii ndiyo kaipata. Kingine ni rahisi sana kusema fukuza bila kuangalia madhala ya upande wa pili.
 
Simsapoti huyo mama kuondoka, ila makosa ni ya mwanaume. Huwezi kumkaribisha mwanamke mwengine nyumbani hivi hivi tuu alafu utegemee mwenzio achekelee. Na inavyoonekana, hamkujadiliana na kukubaliana na mkeo kabla.
 
Back
Top Bottom