Mwanamke anapokupa masharti.

Hapa duniani kila kitu hutokea kwa sababu. Kuwa kwako na raha leo usione kwamba umefika na kusahau shida za wenzako. Huyo kaka alisoma na huyo dada na kwa kuwa wanafahamiana aliomba afikie hapo. Na kwa jibu wa Gervace hajatuambia kuwa huyo mgeni alifika bila taarifa au lah!! Jamani kuweni wavumilivu msianze kuhukumu maisha mnayajua hasa mtu anapoenda kuanza kazi. Na pia mwanamke kwa upande mwingine ataondokaje nyumbani alafu atume message kwenye simu? Kama kweli yeye ni genuine kwa nini asikae chini ajadiliane na mumewe? Asije kuwa alikuwa anatafuta sababu siku nyingi ya kuondoka kwa huyo mumewe na hii ndiyo kaipata. Kingine ni rahisi sana kusema fukuza bila kuangalia madhala ya upande wa pili.

Wakumwitu wala siyo kwamba tunaraha then tunasahu wengine, Abiria chunga mzigo wako tahadhari kabla ya hatari mwenzangu aka!
 
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf


Fukuza haraka huyo mgeni, nenda katafute mkeo haraka sana!nasisitiza tena haraka sana usilete mchezo na ndoa!
 
Kuondoka sio ufumbuzi. Angepaswa kulaa akaanglia mambo yanAvoenda. Sasa akiondoka na wewe ukabaki namgeni itakuwAje?
Tafuta mtoto Wa kike au ndugu wa Karibu aje alale nae usimuondoe.
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokupata lakini kuwa makini sana na mkeo kitu alicho fanya sio jambola lakawaida kwa mwenye adabu na mafunzo ya wazazi hakika huyo simkemwema hanasababu yoyte yakuacha mji wake kwakufikiwa na mgeni na angekuwa na heshima na mapenzi na wewe asinge kupa mwanya wakuwa na mgeni pekeyenu huyo analake jambo muache akae huko alipo. wala usimfukuze binti nimgeni na hapo ulipo hajui mtu zaidiyako msaidie kiasi unacho weza mkuu dunia hii hujui mbeleni nani atakushika mkono. siumeona mfano mkeo kaona shughuli kubwa kufikiwa na mgeni na anahitaji msada wa muda mfupi. nashangaa jamaa wanvyo kushambulia sijui ni watoto au ni wale walianza maisha kwa kutayarishiwa na mama zao hawajui nini kuanza maisha mmeisha elezwa binti ndo kaanza kazi lakini doo kweli wabongo waleo sio kabisa
 
Peleke mgeni gesti
Mtafuta mkeo
Rudisha familia pamoja
Huyo mgeni ni wa kuja na kuondoka
familia yako wako na we milele..
 
tabia ya mke ni lazima unaijua, mgeni tu aondoke.? kuna jambo labda hujasema, lkn kama ni hivyo tunza uaminifu wako kwake fanya taratibu mgeni aondoke kwa heshima na uungweana wote kisha malizana na mkeo ,
 
Fukuza mgeni kamtafute mkeo mimi ni mwanamke pia na imeshawahi kunitokea, ni upuuzi kukaribisha mtu asiye ndugu wa tumbo moja. ten fukuza haraka sana! la sicyo unaharibu ndoa yako.

Duh! Hayajakutokea the other way round wewe.
 
pole sana,
1-Ila naamini umemkaribisha huyo mgeni pasipo kukubaliana na mkeo,jambo ambalo kama wana ndoa haupaswi kufanya hivyo USIRUDIE TENA KULETA UGENI PASIPO BARAKA ZA MKEO,ksb maamuzi ya kupokea wageni lazima mkubaliane wanandoa wote ukizingatia pia kuwa hata bajeti hua inabadilika pindi mgeni anapokuwepo.
2-Pia huyu mgeni alipofika hapo nyumbani alibehave vipi kwa mkeo, manake kuna wageni wangine japo siyo GFriend kama ulivyosema lakin anaweza kuwa ameonesha dharau kwa mkeo au amejishaua weee kiasi ambacho kimemkera mkeo,manake wageni wengine wakiingia majumbani mwa watu hayo mashauzi yao mmmhh ni karaha tupu.
3- Wala usimfiche huyo mgeni wako mwambie kinachoendelea kati yako na mkeo kama ni mstaarabu basi ataondoka/ kama siyo mstaarabu wewe mwondoe kwa ustaarabu aende Gest HSE akafikie huko mpaka apate hapo atakapopata pa kuishi.
4- Huyu mkeo SIMUUNGI MKONO KUONDOKA HAPO HOME japo kakereka na huo ugeni,ksb kuondoka kwake HAKUTATUI TATIZO BALI NI KUONGEZA TATIZO, lakin kwa vile kaondoka na ili na wewe kuonesha kuwa kweli UNAMPENDA,UNAMTHAMINI,UNAMJALI,UNAMHITAJI, KUONESHA KUWA MKEO NI MUHIMU NA BORA ZAIDI KULIKO huyoooo mgeni wako basi MTAFUTE MKEO ,MWOMBE MSAMAHA ILI MAISHA YENU YAENDELEE VIZURI KAMA WANANDOA. Mgeni asiwe chanzo ya KUVUNJIKA KWA NDOA YENU. Ila pia jaribu kumsoma mkeo je ni mke anayependa wageni??, na kama ndiyo anapenda je wageni wa aina gani??,na kama ni kati ya wale wasiopenda wageni basi kama unampenda pia una uamuzi wa kuishi naye hivyohivyo kwa kutopokea wageni au laa. Ila kama hapendi wageni basi HAKIKISHENI NA NYIE MSIWE WAGENI MAJUMBANI MWA WATU,lol.
 
ulizungumza na mkeo kuhusu ujio wa mgeni au ndo ulijiamulia tu? maana kama mkeo angekua na taarifa na kufahamu uhusiano wako na huyo "mgeni" asingeondoka unless kama mlikua na magomvi yenu nae akapata sababu:bored:
 
Mama hajiamini , na huyo mdada inategemea ana behave vipi? Wadada wengne ni wapana kama mapazia majumbani kwa watu. Kosa la mama ni kukimbia nyumba. Tafuta mama mweleweshe vizuri. Na huyo binti akae mbali na wewe. Usije haribu nyumba.
Nimependa avatar yako, hiyo mimba bado kujifungua ?
 
Huyo mkeo mpe siku 3 asiporudi nyumbani OA mgeni. Kwishney.

Kha jamani ushauri huu kiboko mwe! utajuaje kama huyo utakaemuoa sasa atakuwa mstaarabu pengine akawa mbogo mara 3 ya mkeo.

Huyo mdada amefanya makosa makubwa sana kukimbia nyumba yake, sa kama anatembea nae si ndio umewaachia uhuru jama? ningekuwa mimi siondoki na kama nawahisi ndio nazidisha mapenzi kwa mume wangu mpaka ataondoka bila kuaga yaani siwaachii hata sekunde ya kuwa pamoja labda wakutane huko barabarani
 
Wakumwitu wala siyo kwamba tunaraha then tunasahu wengine, Abiria chunga mzigo wako tahadhari kabla ya hatari mwenzangu aka!

Mama B hiyo mizigo ikisafiri mnaichungaje? na je mnafahamu huwa inakutana na akina nani huko safarini?Ndio maana sisi wengine tuko reluctant kuingia kwenye hii institution ya ndoa kwani imani hamna kabisa. Looks like jamaa ailkuwa na nia nzuri tu ya kumsadia mgeni, jamani huyu mtu kalipoti kituo cha kazi kijijini siwezi kuimagine hali ilivyo huko so alihitaji mwenyeji ambaye ndio huyu kaka Mungu kamtumia. Does this mean tukioa au kuolewa tuache kusupport wale tunaowafahamu simply because ni opposite sex? Kama ndivyo basi kuoa au kuolewa ni bullshit, there is no meaning in it completely. Humu duniani we need each other wandugu kama si leo basi ni kesho.
 
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf

Inaonekana kwa wakati wote wa ndoa yenu humthamini na kumheshimu mke wako, mara nyingi umekuwa humsikilizi ndiyo maana aliamua kuleta message kwako by action ya kuondoka. Hivyo JIFUNZE kumsikiliza na kumheshimu mke wako, sikiliza hisia zake.
 
Back
Top Bottom