Mwanamke ajifungulia kwenye pantoni muda huu!!!

Mwanamke ajifungulia kwenye pantoni muda huu!!!

Mkuu wangu mpaka Shehe yahya aongee ndio watapeleka hudma......

BTW karibu Nai

Vipi Naii, wanaongeleaje kifo cha mnabii isti afrika?

Salimia manzii wote..sisi tunasota na serikali yetu!!..
 
Ni fedheha kwa taifa hili lenye miaka 50 baada ya uhuru hatujali afya ya mama na mtoto!

Ukiangalia Demographic Health Survey wanaripoti maternal mortality rate iko 578 kwa akina mama 100,000 na ni 46% tu ya wanawake wanapata uangalizi wakati wa kujifungua, afya ya mama na mtoto bado mgogolo. U know better than I do.


Uko sahihi kabisa Mchungaji...hivi hakuna namna anmbayo tunawezakufanya kuboresha hali hii? Of couze kama kuishinikiza serikali tuishinikize ili iweze kutupatia huduma za kutosha?
 
Yawezekana alikuwa safi kabisa kabla ya kuanza safari, lakini hali ya bahari ilichangia kwani watu wengi maji ya bahari huwatatiza ki-hisia
 
Isome vizuri post acha kusoma nusunusu kiongozi! Natumia simu hawezi kupost picha

Kututmia simu si sababu ya kutoweza kupost picha. Mbona wengi tunatumia simu na tunapost picha kwa kutumia hizo simu. Sema hana tu hizo picha.
 
Inawezekana mtoto ni pre mature, au kawahi kidogo DDE, Haya mambo yanatokea ndo mana wamama wanashauriwa mwezi wa mwisho watulize makalio nyumbani tena karibu na hospital. Hata hvyo huduma zetu za mama na mtoto haziridhish ukute alikuwa anawahi kwa hospital ya wilaya. Pole mama hope baada ya hapo aliwahishwa hospital.
 
hii ndio tz bwana! Ktk hali ya ajabu mwanamke mmoja amejifungulia ndani ya pantoni lile kubwa hapa kigamboni huku likiwa ktkt ya bahari! Mashuhuda tulio kuwepo imetubidi kufumba macho! Hii watz tunakwenda wapi? Yani hakuna cha ambulance wala mkunga yani ni balaa tupu!! Chanzo mm mwenyewe ndani ya pantoni kubwa!!!
hata zile bajaji????
 
usitishe watu wewe, mi ukiacha mwanangu wa mwisho aliyezaliwa nikiwa nje ya nchi, wengine wote walizaliwa huku nikisaidia saidia pale. ni kawaida tu, usitishe watu!

Sijamtisha mtu, we kama unaweza kuangalia si wote kaka !!! mie ndo naogopa!! kama we huogopi si unyamaze. kwanza unasaidia hupush wewe!! so hujui chochote
 
Hii ndio tz bwana! Ktk hali ya ajabu mwanamke mmoja amejifungulia ndani ya pantoni lile kubwa hapa KIGAMBONI huku likiwa ktkt ya bahari! Mashuhuda tulio kuwepo imetubidi kufumba macho! Hii watz tunakwenda wapi? Yani hakuna cha ambulance wala mkunga yani ni balaa tupu!! Chanzo mm mwenyewe ndani ya pantoni kubwa!!!

...miongoni mwa mambo yanayoweza kutokea wakati wowote, na mahala popote ni UHAI na KIFO.
Hii kasumba ya kuilaumu serikali kwa kila kitu ni matokeo ya uvivu wa kufikiri.
Kina dada/kina mama mliokwisha jifungua mnafahamu vizuri Uchungu maana yake nini, na Intervals zake.

Hebu tubadilikeni jamani, Loh? ....Lini tutaacha uvivu wa kujipatia majibu ya maswali rahisi kama haya?
Tumejilemaza kutafuta 'nani mchawi wa kulaumiwa' ilhali matatizo tunayachangia wenyewe (kwa uvivu wa kufikiri.)
 
Lakini katika hili mimi sijaona sehemu ambayo serikali imeingizwa lawamani jamani, hebu tuache siasa kwenye kila kitu.

Kitaalamu, dr. anapogundua una ujauzito, atakuhesabia siku zako za ujauzito 280 na kukupa tarehe ya makisio ya kujifungua (EDD), pia utafanya ultersound kwa ajili ya kuangalia mlalo wa mtoto na ukubwa wake ambayo nayo itatoa makisio ya tarehe ya kujifungua (most of the time kama unakumbuka sahihi tarehe yako ya mwisho ulipoanza siku zako za heshi, tarehe hizi za makisio huwa hazipishani more than a week.

ujauzito wa wiki 37, unatambulika kama full term pregnancy, huku ikumbukwe kwamba ujauzito wote kamili ni wiki 40. hii ina maana kwamba still kuanzia wiki ya 37, mama anaweza kujifungua mtoto salama kabisa na akaishi bila tatizo lolote. still, kuna wale ambao wana overdue date, yaani anaenda hadi wiki ya 42, ambapo most dr. wanalazimika kuwapa dawa za kuwahisha uchungu kama hawana dalili za uchungu.

Kinachotokea ni kwamba, kama mama ni health na hana tatizo lolote, wengi huwa wanajisahau na kuendelea na maisha yao wakisubiri uchungu, na muda wa uchungu kuanza hadi kujifungua unatofautiana kati ya mama na mama, hivyo wengine wanajikuta wanapoata uchungu na ndani ya 1 hour to 2 ameshajifungua, while kabla hajaanza uchungu alikuwa kawaida.

Hii kwangu naichukulia kama ni bahati mbaya ya mama kujisahau tu, au kuwa bize na maisha hadi anajiokuta uchungu unamuanza njiani na sia ajabu ukumuuliza atakuambia alikuwa hana dalili yoyote ya kujifungua alipotoka nyumbani.

All we need to do ni kuwaasa wamama kuwa makini sana once wakiingia wiki ya kuanzia 37 hadi watakapojifungua............. japo still hawawezi ku'control na wala hawawezi kuilazimisha labour (uchungu uanze), it is a natural thing
 
Back
Top Bottom