Mwanamke ajifungulia kwenye pantoni muda huu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke ajifungulia kwenye pantoni muda huu!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, May 20, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Hii ndio tz bwana! Ktk hali ya ajabu mwanamke mmoja amejifungulia ndani ya pantoni lile kubwa hapa KIGAMBONI huku likiwa ktkt ya bahari! Mashuhuda tulio kuwepo imetubidi kufumba macho! Hii watz tunakwenda wapi? Yani hakuna cha ambulance wala mkunga yani ni balaa tupu!! Chanzo mm mwenyewe ndani ya pantoni kubwa!!!
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Duu!!Alikuwa anapelekwa muhimbili?
   
 3. duda

  duda Senior Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole yake, Boss wangu pole kwa hilo maana kushuhudia mama akijifungua usiombe ikukute, mie nilishuhudia yn mpaka naogopa hata kumzaa huyo mtoto,
   
 4. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,622
  Likes Received: 12,881
  Trophy Points: 280
  Poleee du hatari lakini usilaumu sirikali
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Yani mpaka hamu ya kupata lunch sina! Sijui alikuwa anapelekwa hosp au laa kwakuwa hakuna ishara yoyote inayoonyesha kuwa alikuwa anakwenda hosp.
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,036
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Huwezi kulaumu mtu kwa hili,anaweza kuwa alichelewa mwenyewe kuwahi hosp au matarajio yalikuwa bado kama alivyoelezwa na daktari.
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Inatisha ila nakuomba usiogoe kwakuwa ndilo agizo la mungu! Nipo tayari kukusaidia uzae, vp upo kwenye himaya au bado?
   
 8. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Du pole zake jamani, hawa manesi na madactari wetu vipimo vyao ni vyakubahatisha.
  Wanawake wengi wanajifungua katika mazingira ya ajabu ajabu na wkati wanahudhuria clinic kutwa.
   
 9. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  teh teh!! yaani ambulance ndani ya pantoni??
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseeeee...hopefully mama na mwana wote wazima!!Hayo mengine utasahau tu!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  kazi kwel kwel
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tunaomba source na picha za tukio!
   
 13. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hawa wakina mama wakati mwingine hawazingatii siku za kujifungua..Ina maana alikuwa hajui kwamba huo ni mwezi wa kujifungua???

  Cha msingi ni mtoto amezaliwa salama...Sijui atamuita jina gani
   
 14. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Siyo kuchelewa mwenyewe tu; siku hizi hata hivyo vipimi vya hospitali zetu haviamini: ni lishashududia my Wife kidogo apate matatizo hivihivi; nilishauriwa hosptalini na Ma-doctor kuwa Wife apige Ultra-sound ili kuangalia mtoto amekaaje tumboni, na muda mufaka wa kujifungua kitendo ambacho nilitekeleza fasta; majibu yaliyopatikana tuliambiwa kwamba mimba ina wiki 36 hivyo bado wiki 4 kujifungua. Tulirudi nyumbani tukakaa siku 1 tu iliyofuata uchungu ilizidi ikabidi nimrudishe hosptali ilikuwa kama saa 7mchana ilipofika saa 9 akajifungua, sasa ningechelewa nami yangenikuta makubwa. Duh tuwe makini na hospitali zetu pia.
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  May 20, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli lakini saa nyingine wamama huwa tunashauriana visivyo. Wapo wanaoshauriwa kuwa ukianza kusikia kitu kama uchungu usikimbilie hospital uache uchanganye kwanza ........sasa kama katika process ya kukuacha uchanganye na hospital iko mbali yanawezakutokea mengine.

  pili huwezi jua pengine hata yeye mwenyewe siku zake zilikuwa hazijatimia (ingawaje huwa tunashauriwa kujiandaa kila mara hasa siku za mwishono) so kimetokea kama shtukizo na mambo yakawa mambo.

  Au pengine kuna kilichomshtua na kumfanya mtoto atamani kuwahi duniani.
  Angekuwa anasafirishwa kwa machela au wheelchair na manesi au dakitari basi tungewezailaumu serikali au manesi kwa kutomsaidia mapema.

  pole mama na mwanao. Mungu awalinde
   
 16. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #16
  May 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Isome vizuri post acha kusoma nusunusu kiongozi! Natumia simu hawezi kupost picha
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sioni ukweli hapo! Unaweza post picha kutumia simu JF
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  nafikiri mama alichelewa kutoka nyumbani au alipoteza muda mwingi kusubiri Kivuko.

  Vipi alijifungua salama?
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  May 20, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Tafadhari naomba msaada wako ili nijue kupost picha kupitia simu, natumia blackberry curve 8520 os v.5! Kiongozi nitakushukuru sana!!
   
 20. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,396
  Trophy Points: 280
  Kigamboni wanahitaji hospitali yenye hadhi ya hospitali ya hospitali ya wilaya
   
Loading...