OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,247
- 103,953
Mwanakondoo katikati ya mbwa mwitu.
_________
Huyu dogo ni miongoni mwa vijana naowakubali sana. Anaitwa Elia F Michael. Kwanza yupo smart sana upstairs, pili ana misimamo isiyoyumba, tatu alishinda udiwani akiwa mwanafunzi chuo kikuu UDSM.
Juzi wakati JPM alipokuwa Kigoma madiwani walialikwa. Na yeye akahudhuria kama madiwani wengine. Madiwani wa CCM wakavaa sare za vyama vyao na yeye akavaa scaff ya chama chake. Wote wakakaa eneo moja. Ajabu ni kuwa Usalama wa taifa wakamshauri avue hiyo scaff, akagoma.
Polisi wakaja na mabavu yao (si unajua hawatumiagi medula) wakataka kumfukuza aondoke eneo hilo. Akagoma. Mwishowe ikabidi madiwani wenzake kupitia CCM wamuombe aondoke ili asiwaudhi wakubwa. Bado akaendelea kugoma maana hakuona sababu ya kufanya hivyo. Kwanini aondoke? Kwa sababu amevaa sare ya chama chake? Absolutely no. Kama ndivyo basi madiwani wa CCM nao waondoke maana wamevaa sare za chama chao.
Baada ya mkutano kumalizika Mhe.Elia Michael alisema "Nikiwa nimeketi kumsikiliza Magufuli mapema leo Kakonko, usalama wa taifa wamenitaka mara tatu nivue skafu yangu na madiwani wenzangu wa CCM nao wamenisaliti wakanitaka nitoke hapo ila wakasahau kama tuna mwaliko wa kufanana kama madiwani. Dawa ya bishoo ni kuwa bishoo zaidi yake." Hongera dogo. Tunahitaji vijana wenye misimamo isiyoyumbishwa kama wewe. Vijana ambao wako tayari kusimamia imani zao hata mbele ya Rais wa nchi. Vijana ambao as long as wanalosimamia ni sahihi, hawako tayari kubadilika for the sake of President or TISS. Wewe ni SHUJAA.!
By Malisa G