CHADEMA yapoteza ushawishi mitaani. Sare zake hazivaliki

Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
4,056
1,813
Ndugu zangu miaka kadhaa iliyopita hakika chama hiki kilijizolea umaarufu mkubwa Sana hasa kwa kundi la vijana, Vijana walijiona fahari Sana kujiita makamanda, vijana wengi hasa wa vyuo vikuu na vyuo vya Kati walikuwa mtaji mkubwa Sana wa chama hiki, Hakika vijana walikuwa na hamasa kubwa Sana na kuhamasika kujiunga na chadema.

Tulio kuwa CCM na kuweka Imani yetu kwa CCM kutokana na Sera zake na itikadi yake tulionekana Kana kwamba Ni vijana tuliopitwa na wakati, tulionekana Ni vijana wakizamani katika Zama mpya, Tulionekana Ni wazee katika umri wa ujana.

Nguo na magwanda ya Chadema yalivaliwa na vijana hao kwa mbwembwe Sana, Wana CCM wakawa wanaona aibu kuvaa sare na kupita nazo mitaani, Wana CCM waliona uoga kujitambusha UCCM wao katikati ya kundi maana ilikuwa unapata mashambulizi yasiyo ya kawaida.

Wana CCM wakawa Wana vaa tisheti ndani ya mashati ya mikono mirefu na kufunga vifungo Hadi shingoni utazani mtu anayetaka kujinyonga, kofia za chama zikawa hazivaliwi Sana maana wanachama waliogopa kuvuliwa kwa nguvu, kofia zikawa zinakunjwa na kufichwa, wanachama wakawa wanakwenda mikutanoni kupitia vichochoroni Hadi uwanjani na kila mtu kurudi kwa njia yake, Tukawa tunaishi utazani sisi ndio wapinzani na wapinzani ndio chama Tawala.

Asante CCM chama kikongwe chenye kila aina ya mbinu, chenye hadhina ya viongozi, chenye kujuwa historia yake,chenye kujuwa wapi kimetoka na wapi kimejikwaa na chenye kujisahihisha.kikaamua kurejea mezani kuangalia wapi kimejikwaa,wapi kiliwakosea watanzania,wapi kiliwaumiza watanzania,wapi kiliacha misingi yake,wapi hakikutenda haki,wapi kiliteleza,wapi kiliwapa kisogo wananchi, wakina Nani walikiangusha,walikifedhehesha,walikinyima kura,walikisaliti,walikipaka matope,waliokichafua,wakina Nani walikifanya kichukiwe na watanzania, Nini kilikifikisha hapo,mambo gani yalikipa doa chama chetu?

CCM ikajisahihisha na kurejea katika misingi yake, Misingi ya kuwatumikia watanzania wanyonge, misingi yakutokutekwa nyara na wachache, misingi ya kuwa chama kiongozi,misingi ya kutenda haki katika michakato yake ya ndani,misingi ya kutanguliza mbele Taifa letu, misingi ya kusikilizana na kushirikiana,misingi ya kuhakikisha kuwa chama kinakuwa Sauti ya wanyonge,misingi ya kuhakikisha chama kinakuwa masikio na mdomo wa watanzania wanyonge,Misingi ya kuwapa nafasi vijana, misingi ya kukiweka chama mikononi mwa wanachama,Misingi ya kusema kweli na kuondoa ufitini

Hatimaye watanzania wamerejesha matumaini ndani ya CCM, hatimaye watanzania wamesamehe yote yaliyopita, hatimaye watanzania wametambua mzazi Ni mzazi tu ,Hatimaye watanzania wameona namna CCM inavyowatumikia kwa upendo na bidii kubwa, wameona namna CCM na serikali yake inavyogusa maisha yao, hatimaye watanzania wameona namna serikali ya CCM inavyokesha ikifanya kazi, hatimaye wameona namna serikali ya CCM ilivyo sikivu na makini katika kuwatumikia.

Kibao kimegeuka, Sasa chadema haieleweki Wala haisikilizwi, haifuatiliwi Wala haipewi masikio na watanzania, chadema kwa Sasa haina ngome ya aina yoyote Ile, Haina ushawishi kwa watanzania, Haina mizizi yoyote Ile, imebaki imening'inia hewani tu, Haina matumaini ya aina yoyote maana hakuna wa kuipa matumaini.

Wanachama wake wachache waliobakia wanaogopa kuvaa hata Sare zake, wanaogopa hata kusema juu ya chama Chao, wanaogopa hata kutetea chama Chao maana hakuna wa kuwasikiliza na hawaelewi watetee Nini, wenye akili walishawakimibia,walishawapa mkono wa kwa heri, walishabeba akili zao na mikakati yao, walishaondoka na ajenda zao,kimebaki Ni chama kisicho na dira Wala muelekeo, kimebaki Ni chama chenye safu ya uongozi iliyojikatia Tamaa na isiyotoa matumaini hata kwa wanachama wake yenyewe na haina ushawishi kwa watanzania, Hakina viongozi wenye mvuto wa kihoja, hawana maono Wala misimamo ya aina yoyote Ile na hawaeleweki wanasimamia Nini na wanapigania nini.

Chadema kimebaki Ni chama ambacho hakina uwezo wa kuandaa hata ilani ya chama, hakina watu wenye kufanya utafiti wa kisera , Kimebaki Ni chama kilichojaa viongozi wenye mihemuko tu, Kwa heri Chadema wakati si wako Tena na haupo upande wako Tena, Karibuni CCM Tuijenge nchi yetu, Vijana wenye kujitambua wamesharejea ccm na Kuendelea na kazi ya kuijenga nchi yetu.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 

Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
4,056
1,813
Kwa awamu hii kujifunga OWN Goals sidhani hata kama wanahitaji Upinzani kujichimbia Kaburi...

Yaani kuandika kwangu hii post huku natumia mshumaa ni uthibitisho tosha wa kazi yao...
Kuwa mvumilivu wakati maboresho yanafanyika ili tupate umeme wa uhakika wakati wote
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom