MwanaHalisi: Njama za Mauaji zafichuka, za kuwauwa Kubenea, Dr. Slaa, Mnyika na Olimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MwanaHalisi: Njama za Mauaji zafichuka, za kuwauwa Kubenea, Dr. Slaa, Mnyika na Olimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 11, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau;

  Baada ya kurudi kwa jembe letu, saed kubenea kutoka masomoni nchini Holland, Mwanahalisi leo limemaliza kazi kabisa. Soma sehemu hii ya stori yake ya leo:


  ___________________________________
  ‘Njama za mauaji' zafichuka
  · Kigogo wa Usalama wa taifa atajwa
  · Ulimboka: Walioniteka ni wa ikulu

  Na Jabir Idrissa

  NAIBU Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS), Jack Zoka ametajwa kuwa miongoni mwa wanaopanga mkakati wa kuangamiza wanaodaiwa kuikosoa serikali, MwanaHALISI limeelezwa.

  Aidha, ametajwa kuwa mmoja wa waliounda mpango wa kutekwa na kuteswa kwa Dk. Steven Ulimboka ambaye hivi sasa anaendelea na matibabu Afrika Kusini.

  Taarifa zilizofikia gazeti hili kutoka vyanzo mbalimbali zinasema, Zoka ni mtuhumiwa Na. 1 katika utekelezaji wa mpango wa siri wa mauaji, utekaji na utesaji ambao umeandaliwa mahususi na kwa watu maalum.

  Miongoni mwa wanaotajwa kutaka kuangamizwa, ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibord Slaa, mbunge wa Ubungo kupitia chama hicho, John Mnyika na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), wachapishaji wa MwanaHALISI, Saed Kubenea.

  Bali Zoka hakupatikana juzi Jumatatu kutoa kauli yake juu ya tuhuma hizi.

  Mwandishi alimwita Zoka tangu saa nane mchana hadi saa 12.55; lakini simu yake iliita bila kupokelewa na wakati mwingine ilijibu kuwa mwenye namba hiyo hapatikani.

  Hatimaye mwandishi alipeleka ujumbe kwa Zoka uliosema: "Natumai umzima wa afya. Mimi mhariri wa MwanaHALISI nataka uzungumzie tuhuma za viongozi wakuu wa Chadema, kuwa TISS na wewe binafsi, mmepanga kuua baadhi yao. Unasemaje?"

  Zoka aliombwa pia kutoa kauli juu ya taarifa katika mitandao, zinazomtaja yeye binafsi kuwa nyuma ya mpango uliofanikisha kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.

  Dk. Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini 30 Juni, kwa michango ya madaktari wenzake, watu mbalimbali na kile kilichoelezwa kuwa "msaada mkubwa wa mfanyabiashara mashuhuri nchini, Dk. Reginald Mengi."

  Kwa mujibu wa mawasiliano ya imeili yaliyotumwa na mmoja wa watoa taarifa wa ndani wa Dk. Slaa na Mnyika, mpango wa kuwateketeza watu hao umeandaliwa mahususi ili "kuwatisha katika harakati za kutetea wananchi wanyonge."

  Mtoa taarifa huyo kutoka ndani ya idara ya usalama ameeleza, katika mawasiliano yake ya 27 Juni 2012, kuwa kuna mpango wa kuteketeza maisha ya Dk. Slaa na Mnyika; na kwamba mpango huo unaratibiwa moja kwa moja na Zoka.

  "…the information I'm giving you is authentic (taarifa ninazokupa ni sahihi na makini). Tayari kuna timu imetumwa kwenda Dodoma kufuatilia mienendo ya Mnyika kwa maana ya mahali alipofikia, mahali anapopendelea kutembea na kula chakula na marafiki anaokuwa nao mara kwa mara, hasa wanawake kama wapo," anaeleza mtoa taarifa.


  Anasema, "Hii timu inafanya kazi moja kwa moja kwa maelekezo ya Zoka na wamepewa kazi ya kutathmini njia bora ya kumdhuru Mnyika bila kuacha trace (unyayo) yoyote. Katika options (njia za kutumia), kuna kuweka sumu kwenye maji, chakula au (kumpiga) sindano. Kuna matumizi ya ajali au ujambazi."

  Andishi hilo linasema, "Katika ajali, timu hiyo imeelekezwa kuangalia mbinu kama waliyowahi kuijaribu kwa Mwakyembe (Dk. Harrison Mwakyembe mbunge wa Kyela CCM). Hapa kuna vijana wamefundishwa kikamilifu njia hii. Mafunzo yao yaliandaliwa (jina la nchi tunalo) mwishoni mwa mwaka jana."..............


  Habari kamili katika MwanaHalisi la leo.
   
 2. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Katika toleo la tarehe 11/07/2012 gazeti hili limeripoti kwa uwazi bila uwoga njama mahususi zinavyo na zilivyoandaliwa na usalama wa Taifa (TISS) na kuzitekeleza kuuwa upinzani wowote ndani ya vyama vya siasa na makundi mbalimbali ya kijamii.

  Kwa ufupi.

  Kiongozi wa mauwaji na mpangaji ni ZOKA akisaidiwa na muuaji maarufu wa serikali na CCM anayejulikana kama RAMA.

  Na kuna vijana maalumu amabao wamepewa mafunzo maalum ya kuua bila kuacha ushahidi wa mauaji na mauwaji hayo ni kama; kuwawekea sumu kwenye maji au vyakula, kuwatengenezea ajali kama ya Dr. Mwakyembe, kuwavamia kama Dr. Olimboka au kuwatumia kina dada kama vile wanakofikia hotelini na kumaliza kazi.

  Na mtoa taarifa kakili kuwa kwa Dr. Olimboka wahusika ni TISS sio polisi kama wengi wetu tuaminivyo.

  Na zaidi baada ya tukio serikali inatumia nguvu na pesa kuhadaa umma na kuuaminisha kuwa Dr. Olimboka alipigwa na wagonjwa na wafiwa wao lakini ukweli ni kwamba TISS ndo imehusika.
   
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Sasa huu ndio ushahidi, mbona mnakuwa wafinyu wa mawazo? Habari hizo hizo zinageuzwa juu chini halafu mnaziona ni mpya.
   
 4. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Haya sasa,...ngoma bado mbichi
   
 5. Imany John

  Imany John Verified User

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Nasikia upo mbioni kumkana mama yako mzazi kutokana na kipato ukipatacho humu,cha kupinga na kufifisha hoja upate hela.

  Endelea na kazi yako humu jf,aliyekutuma anakuharibia mkeo. Stuka
   
 6. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Safi sana,japo hii habari inanitisha ila tumuombe MUNGU awalinde,atulinde Amen!
   
 7. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  furaha yako kufa kwa watu,je wangekua nduguzo kwa akili zako ungeafiki,use ur brain dont be mad
   
 8. m

  majebere JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Yani nyie mnaweza kusababisha Mnyika apate pressure, kila akichungulia humu anakutana na vitisho vimerudiwa. Acheni kumtisha jamani, sio vizuri.
   
 9. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  toa ukweli wako mbadala
   
 10. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mpiganaji hatishwi na hizi habari kwa sababu anazo kabla hazijafika humu
   
 11. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Mbaya zaidi ni wajumbe wa CCM taifa
   
 12. m

  majebere JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Naona wewe ndio umepitia haya unayo sema, una utaalamu nayo nini?
   
 13. r

  richone Senior Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  watanzania wengi tunajua na tunaamini mambo yote mabaya yanafanywa na serikali kwa kutumia maajent wao TISS. pamoja na baadhi ya mapolisi na nimefurahishwa sana na kitendo s=caha DR slaa kukataa kuhojiwa na Polisi ccm.
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mwanahalisi haliko upande wa serikali kwa muda mrefu ..
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  watu makini tulitegemea mtazamo huo kutoka mwanahalisi.
   
 16. G

  Gene Senior Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakubwa waanze kula kwa mama Ntilie tofaut tofauti...
   
 17. Imany John

  Imany John Verified User

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Lipo kwa wanyonge kwa muda mrefu,nashukuru kama umelitambua ilo.
   
 18. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Thafi thana kubenea!!ccm na kifo kichawi haiwi kutapatapa
   
 19. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Usalama wa taifa - "The killers wa wapenda maendeleo na watetezi wa haki". Sijawahi kuona popote isopokuwa TZ tu. This is too wicked which won't go without punishment from above. People are now crying to GOD hence you will soon pay for your uovu.
   
 20. M

  Mantisa Senior Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama siyo si wakanushe basi? Mbona last timu nakumbuka nilimuona Mkuu wa Usalama wa taifa akikanusha tuhuma

  Kweli nimeamini Serikali imeshapoteza dira
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...