Mwanahalisi: CCM wajipanga kumzuia Dr Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanahalisi: CCM wajipanga kumzuia Dr Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 18, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM wajipanga kumzuia Dr Slaa

  • Waandaa mamluki kumdhamini
  • Waomba msaada wa vyama vidogo

  Na Saed Kubenea

  Mkakati umesukwa na viongozi ndani ya CCM ili kuzima safari ya Dk Wilbrod Slaa kwenda Ikulu, Mwanahalizi limeelezwa.

  Taarifa zinasema, kwa kushirikiana na vyama vidogo vya upinzani, CCM imesuka njama za kumkwamisha Dk Slaa katika hatua ya kurejesha fomu za kuwania urais.

  "Kama hatukufanikiwa kumkosesha wadhamini halali, basi tutakwenda mahakamani….lakini hapiti," kimeeleza chanzo cha gazeti hili kikimkariri mmoja wa viongozi waliopewa jukumu la kumzamisha Dr Slaa.

  Mwanahalisi lina taarifa kamili juu ya njama hizo zinazodaiwa kuhusisha baadhi ya viongozi wa CCM, serikali na vyama vya upinzani.

  Dk Slaa aliibuka wiki tatu zilizopita, pale alipotangazwa na Chadema kuwa mgombea urais kwa tiketi hiyo.

  Kuingia kwa Dk Slaa ulingoni kulibadili upepo wa kisiasa nchini, na kuleta kiwewe ndani ya CCM na hata kufanya viongozi wastaafu wa chama hicho kutamka hadharani kuwa "Slaa ni makini…. Hashikiki."

  Hatua ya kwanza ya mkakati wa kumwangamiza Dk Slaa kisiasa inahusisha kumchomekea "wadhamini feki" katika fomu zake za kutaka kuwania urais.

  Hatua hii inahusisha maandalizi ya genge la vijana ambao uraia wao una utata. Hawa watapelekwa mikoa mbali mbali nchini ili watie saini fomu zake za udhamini.

  Kwa mujibu wa mtoa taarifa, wadhamini hao "feki" watafika kwa maofisa wa Chadema wanaoendesha zoezi la kuandikisha wadhamini wakiwa na vitambulisho vyao vya kupiga kura, kwa lengo la kutimiza jukumu walilopewa.

  "Vijana hao wakimaliza kujiandikisha, wataripoti kwa maofisa wa chama xhao (CCM) ambao watarekodi kadi zao. Kwa kutumia kadi hizo za wasio Watanzania, Dk Slaa atawekewa pingamizi," ameeleza mtoa habari.

  "Nakukuhakikishiua, Chadema wasipokuwa makini, Dk Slaa hawezi kuwa mgombea urais. Tayari vijana wametumwa mikoani kutimiza azma ya kumkwamisham" ameeleza kiongozi mmoja wa CCM ambaye hakutaka kutajwa.

  Sheria ya uchaguzi inamtaka kila mgombea wa urais awe na wadhamini 200 kutoka mikoa 10 nchini, ikiwamo miwili ya Visiwani.

  Kwa taarifa za juzi Jumatatu, jukumu la kumwekea pingamizi Dk Slaa litakabidhiwa kwa "wagombea urais wa vyama pinzani." Haijafahamika ni kina nani watapewa jukumu hilo.

  Wadau, stori kamili katika front page ya Mwanahalisi ya leo. Mwenye soft copy yake atuwekee hapa.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  hawataweza coz watanzania tuko macho kipindi hiki. tumechoka na shida za kujitakia.
   
 3. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  hicho ni kiwewe na kutapatapa kwa CCM kwani wanajua kuwa tumeshawawashia moto.

  Mbinu chafu kama hizo ni kuonyesha kuwa Tanzania inaendeshwa na chama cha Mamafia
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Zak Malang twashukuru mkuu. Hi ni taarifa ambayo CHADEMA wanapaswa kifanyia kazi kwa mbele nyuma, nyuma mbele.

  Yawezekana ni kweli huo mpango upo, nina wasi wasi na timing of attack, habari za CCM kutoka nje kirahisi, tena kwenye issue sensitive kama hii uwezekano ni mdogo sana. Kwa hiyo hapa kuna mawili, hii ni primary attack/plan they will come with the secondary plan which will bring and achieve the target/goal, without forgetting contingency plan.

  Ndo maana nawaonya CHADEMA suala hili lichukuliwe kwa uzito, lakini they should work with three dimension alert that something big is coming there way. Be alert.

  Go CHADEMa, go Slaa...
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,859
  Likes Received: 11,978
  Trophy Points: 280
  Tatizo lao hasa ni nini Slaa hafai kuwa rais au wao hawataki awe rais maana haya ni mambo mawili tofauti, maadam mbinu zao zimefahamika mapema i'm very sorry hawatafanikiwa.
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  MS mkuu unanishangaza sana!!!
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehehehe
  hehehehe
  hahahaha
  ccm bana we acha tu
  ni majambazi haswa na wanajua hila zote za kishetani shetani
   
 8. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Jamani hawa CCM waangalieni hivihivi. Unajua Mr Bashe aliyetajwa kuwa si raia Uhamiaji wansema ni raia wa haki tu!
  CCM japo inazidi kupotea na ina wasiwasi kwa matendo yake, Lakini wana mchezo mchafu sana na sometimes wantumia fedha zetu katika kukwamisha wanaharakati wetu.

  Mimi naona watafanya mengi kumkwamisha Rais Dr. Slaa. Asiingie Ikulu. Tumwombee sana Dr.
  kama utakumbuka walivyowasambaratisha CCJ na kuwafrastrate basi angalieni sana.
  humu wapo Chadema so tafuteni wanachama wa ukweli fanyeni utafiti
  Kwa sababu mnapambana na Mafisadi nyangumi.

  HII HABARI SI YA KUBEZA WANA CHADEMA
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  kama wakija hao vijana ambao sio raia na wakija na kadi zao za Kupigia kura sasa hapo kosa litakuwa la nani?, chadema sio chombo cha kuscreen nani ni raia na nani sio raia, ili mradi mtu akija na kitambulisho GENUINE cha kupigia kura hata kama sio raia hilo chadema hawana habari nalo, hilo ni kosa la Tume ya uchaguzi kutoa kitambiulisho cha kura kwa asiye raia
   
 10. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Sikupingi hata neno moja, Kwasababu najua kwanza unacheka kwa kebehi ya CCM. Kilianza kama chama cha Mapinduzi mema.

  sasa chaweza kuwa na majina kibao. wote waliomo humo wamo kwa sababu ya ulaji uliopo lakini ukwqeli kwamba Mirija ya unyonyaji imo kwa walalahoi wanajua kabisa. Na wale wanaoona ukweli halisi wanakimbia lakini kuna watu ambao wameshakula sana na wana mijikashfa kibao hawawezi kutoka kwasababu wataumbuliwa soon.

  lakini Hawa wote ni mashetani LIVE.
  Maneno yao mazuri sana, matendo madogo yaliyopakwa rangi kibao.

  Tuweni wakweli na siyo wanafiki katika kuhudhuria TAREHE YA KUPIGA KURA,
  Piga kura kuchagua maendeleo siyo kuishia kupiga kelele tu.

  A SIGLE VOTE MEAN A LOT, NA YOTE YANA MWISHO:playball:
   
 11. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haiwezekani kati ya wadhamini zaidi ya 1.3 Mil aliopata Slaa wakosekane 200 tu wa halali ..hilo ni kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano..!
   
 12. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  other way round kumbe mwaka huu hata wageni watapiga kura!!
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hii move yao itashindwa tu. Kwa nini wanaogopa changamoto za kisiasa? You cowards!! mkia m a t a k o n i kama mbwa koko!!
   
 14. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Inabidi kuwa makini sana katika hili,

  Maana hao CCM wana fedha nyingi sana. Wanachokifanya ni kuchonga kadi ambazo ni bandia na si hizi tulizonazo wapiga kura halali, halafu wakija kuhakiki wanaosaport Mgombea hao watu wapo tayari na mishiko imeshakuwa tayri, basi wanawahi kujitokeza.

  Linalofuata anaondolewa kuwa chama kimekosa supporters na kutafuta wa bandia ambao hawakubaliki.
  Mwisho wa siku wale wenyewe mko mbali na watu kama 100 ni bandia na wamefunga msitari basi ndo mpango wao.

  Kumbukeni vizuri lile la CCJ. CCM WAHUNI KULIKO TUNAVOJUA
   
 15. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  wewe acha kabisa, Mamluki ni kitu kingine. Na kuna experts wa umafia hadi maofisa wa makundi mhimu nchini hupandikizwa na mwisho
  Unajua mshiko wake wanaopata. Otherwise si siri itavuja?

  Wanaandaliwa watu special unaweza kukuta hadi mtu wa 500 ni mamluki tu wamejipanga na ni wakali kuliko aliyeanzisha CHADEMA mwenyewe. labda chadema sasa wapite kuscreen na kuwaondoa wenyewe kabla ya kufika kwa anayehakiki pale pale. itakuwa vema mabli na hapo Tusilibeze hili
   
 16. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  These are all challenges which I am sure the task force CHADEMA is working on.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  CCM washaonyesha dalili za kushindwa hoja sasa wanataka kuiba iba tu. Kiufupi tumeshaichoka CCM hata wakimtoa Dr Slaa tutampigia mwakilishi wa Dr. Slaa au Profesa Lipumba but CCM no waende tu wakapumzike hatuwataki
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,117
  Trophy Points: 280
  you can fool some people sometime, but you cant fool all the people all the time, siongezi neno
   
 19. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Dr. Slaa yuko makini kuliko kiongozi yeyote CCM.
  Slaa si mtu wa kukurupuka, naamini kama angekuwa ni mtu wa kukurupuka sasa hivi angekuwa Segerea kwenye sakata ya kutaja majina vigogo wanaoitafuna hii nchi. Subirini mtaona umakini wake zaidi pale atakapokuwa anapakua santuri zile mpya 20 hivi karibuni wakati wa kampeni.

  Wanapoteza muda na fedha, ingekuwa jambo la maana kama wangewatafutia hao vijana kazi za kufanya kuhimili ugumu wa maisha.
   
 20. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi ccm walivyochanganywa na ujio wa dr slaa,lazima watatumia kila mbinu kumkwamisha so nawaomba sana hao maofisa wa CHADEMA wawe makini sana ili hao washenzi ccm wasifanikiwe.
   
Loading...