Dkt. Slaa baada ya kuachiwa kwa dhamana, kutoa kauli nyumbani kwake Mbweni

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Muda mchache baada ya Wakili wa Dk. Slaa Dickson Matata kutoa taarifa kuhusu mteja wake kupewa dhamana, Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amesema kuwa akiwa na viongozi wengine wa dini na kisiasa wanatarajia kutoa kauli ya pamoja wakiwa nyumbani kwa Dk. Slaa.

"Sisi Askofu tunaelekea Mbweni, nyumbani kwa Dkt. Slaa muda huu. Tutakuwa na Mheshimiwa James Mbatia pamoja na viongozi wengine wakiwemo viongozi wa dini. Tutatoa kauli ya pamoja mchana huu tukiwa mahali pale." ameeleza Wakili huyo

Ikumbukwe Taarifa liyoripotiwa na kituo cha runinga cha Azam Tv ni kuwa Wakili wa Dk. Slaa, Dickson Matata amethibitisha kuachiwa kwa mteja wake leo Agosti 18, 2023.
 
Niulize tuu kwa upole!! Bado IGP yuko ofisini?

Maana kwa huu ujinga wa polisi hakutakiwa kuendelea kuwa mtumishi wa umma. Ametumia rasilimali zetu vibaya. Amelitia Taifa doa kimataifa, ame nyanyasa watu wasio na hatia. Amekiweka Taifa kwenye taharuki... IGP MUST GO!!!
 
Back
Top Bottom