Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,554
- 2,160
Ana kaka yake anaitwa Adam Malimbwi ana Albinism ni Mhasibu Wa UNDER THE SAME SUN huyu pia ana msongo mkubwa Wa Mawazo kwani akipokea salary lazima afunge bar mpaka uishe.
Taarifa ya polisi ni muhimu sana kuliko maisha, badala ta tiba kwanza wanahangaika toka kituo kimoja cha polisi kwenda kingine! Sasa, hiyo taarifa itamsaidiaje huyo binti?View attachment 213331
Binti mbichi aliyejulikana kwa jina la Neema Malimbwi (pichani) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Kodi Tanzania (ITA) ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kilichopo Mikocheni jijini Dar amefariki dunia kwa madai ya kulishwa sumu kwenye kinywaji.
Marehemu Neema alikuwa binti wa profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (Sua), Rogers Malimbwi.
Tukio hilo la kusikitisha linatajwa kutokea usiku wa Alhamisi, Desemba 18, mwaka huu wakati Neema anarudi hosteli maeneo ya Kijitonyama, Dar ambapo alikuwa akiishi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku ya tukio, Neema alikuwa na marafiki zake wavulana kwa wasichana kwenye onesho la muziki wa B Band inayomilikiwa na Banana Zorro ambapo akiwa huko saa 7 usiku aliendelea kuchati na marafiki zake waliokuwa hosteli akitumia ukurasa wake wa Facebook akiwaambia kuwa alikuwa ‘kiwanja' akiponda raha.
Habari zinadai kuwa, marehemu Neema usiku huo alikuwa akihama maeneo mbalimbali akiwa na vijana ambao baadhi ya marafiki zake wanadai huenda walihusika na kumtilia sumu kwenye bia alizokuwa akinywa.
View attachment 213332
Habari zaidi zinasema kuwa, Neema akiwa na wenzake wakirudi hosteli, njiani alianza kulalamikia kutojisikia vizuri.
"Alikuwa njiani na wenzake wakirudi kulala, akaanza kulalamika kwamba hajisikii sawasawa, ikabidi wenzake wamkimbize Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Palestina, Sinza, Dar ambako waliambiwa kuwa kutokana na hali yake kuwa mbaya wampeleke kwanza Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini' jijini Dar ili kupata hati ya matibabu (PF3)," kilisema chanzo kimoja.Chanzo hicho kikaendelea kudai kwamba, walipofika Mabatini waliambiwa waende Kituo cha Polisi Oysterbay.
Ikazidi kudaiwa kuwa, Polisi Oysterbay walitoa msaada kwa haraka ambapo sasa ikabidi Neema akimbizwe Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala ambako alifariki dunia.
Mwili wa Neema ulihifadhiwa kwenye mochwari ya Mwananyamala kabla ya kusafirishwa juzi kwenda Morogoro kwa mazishi yaliyofanyika jana.
Kumbukumbu zilizopo kwenye makabrasha ya gazeti hili zinaonesha kuwa, Juni Mosi, mwaka jana, mama mzazi wa Neema, Elizabeth Malimbwi alifariki dunia kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar na mwili wake kwenda kuzikwa Morogoro.
Tangu kifo cha mama yake, baadhi ya madenti wenzake wanasema, Neema amekuwa akiishi maisha ya mawazo sana na muda mwingi alikuwa akiutumia kunywa pombe kiasi kwamba, darasani ilikuwa mara chache sana kuhudhuria.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura alikiri kuwa na taarifa hizo."Ni kweli taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo ninazo, mpaka sasa jeshi la polisi linasubiri ripoti kamili ya uchunguzi wa madaktari kuhusiana na kifo chake," alisema Kamanda Wambura.
Chanzo: GlobalPublishers
---Gone too soon, Poleni wafiwa....
Mapendo,
TANMO.
Yule kaka yake adam alishafariki kwaniNimekukumbuka sana Neema (Londai), najua mama na kaka yakk pia wametangulia sisi tu nyuma yako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huu utaratibu wa PF3 inabidi upitiwe upya,mtu yuko taabani unaulizia PF3 utazani ndo chanjo ya kumponya.Isingekuwa mlolongo wa PF3 labda wangeweza kumuokoa!
Kwa nini wasi control hali ya mgonjwa kwanza?
Hapana kaka yake Adam yupo tulimuozesha mwezi uliopita ila Joshua ndiyo alifariki alizikwa kwao huko Lushoto Vuga
Acheni Hii familia itulie jamani mwacheni prof malimbwi atulie familiar imeondokewa na mama mzazi Joshua malimbwi na huyo binti yao bado mnataka Kuisimanga plz stop that acheni wapumzikeHapana kaka yake Adam yupo tulimuozesha mwezi uliopita ila Joshua ndiyo alifariki alizikwa kwao huko Lushoto Vuga
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii thread ni ya 2014.Acheni Hii familia itulie jamani mwacheni prof malimbwi atulie familiar imeondokewa na mama mzazi Joshua malimbwi na huyo binti yao bado mnataka Kuisimanga plz stop that acheni wapumzike
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo masimango yako wapi aiseeeAcheni Hii familia itulie jamani mwacheni prof malimbwi atulie familiar imeondokewa na mama mzazi Joshua malimbwi na huyo binti yao bado mnataka Kuisimanga plz stop that acheni wapumzike
Sent using Jamii Forums mobile app
Acheni kufukua makaburi. Thread ya mwaka 2014 nashangaa imefukuliwa tena kwa mtu aliyepumzika. Acheni dada wa watu apumzikeHapo masimango yako wapi aiseee
Kwani watu kama nyie ambao bado nyeupe mnaona ni nyeupe mpo wapi??nlidhani mmeashaisha kumbe mpo...BIG UP .Mtu anasemwa kapewa sumu, badala ya kukimbizwa hospitali awahishwe tiba, anatakiwa apelekwe polisi kwanza apewe PF3, ndio arudishwe hospitali.
What a bunch of bloody bollocks and vogon verses!
Somebody ought to sue whoever instituted this shitty bureaucratic procedure.