Mwanafunzi Shule ya wasichana Korogwe agonga wenzake kwa gari wakijiandaa kwa mahafali

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,971
10,465
Ndugu wanajamvi,

Poleni kwa majukumu. Leo kulipangwa kufanyika mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wanaohitimu masomo mwaka huu. Habari nilizopata muda huu kutoka kwa wilayani Korogwe ni kwamba, wanafunzi wakiwa wanaendelea na maandalizi ya kuingia ukumbini kuanza sherehe, ikatokea mwenzao akachukua gari ya wazazi wake na kuanza kuiendesha katika viunga vya shule. Katika pilika hizo za kuendesha, amewagonga wenzake , ambao hali zao inasemekana ni mbaya sana, na wamepelekwa katika hospitali ya Magunga ya wilaya hiyo.

Chanzo cha habari hii ni dada yangu aliyepo hapo Korogwe muda huu, alikwenda hapo kuhudhuria mahafali hayo ya wanafunzi wa Korogwe Girls.

Mwenye ndugu yake hapo shuleni aanze kuwasiliana nae muda huu. More updates later.

Nawasilisha..


..¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤¤
Updates....Mwanafunzi aliyegonga wenzake anaitwa 'KIBIBI MMASA BAKARI.'
Waligongwa (hali zao bado zina utata) ni hawa wafuatao:-

1. Wakonta Mapunda
2. Lulu Calisty
3. Vicky Mtwale na
4. Nancy Juma
5. Zahra Jumanne

Nawapa pole sana waliopatwa na mkasa huu.

More updates coming......


11.JPG

Mkuu wa wilaya ya korogwe mwenye suti akiwa amemshika mwanafunzi Kibibi Mmasa (19) aliye weka gia ya kurudi nyuma gari na kusababisha balaa kwenye mahafali ya kidato cha sita shule ya wasichana Korogwe.

12.JPG

Hili ndilo gari lililo haribu mnuso wa Korogwe Girls wazazi na walezi wakaamua kurudi kwa majonzi majumbani na mapilau yao kwenye mahot pot. Hapa likiwa limeegeshwa shuleni hapo baada ya ajari.

Mwanafunzi Zahra Jumanne wa Korogwe Girls afariki dunia tarehe 5 Februari, 2012

Zahra Jumanne, Mmoja wa wanafunzi waliopata ajali ya kugongwa na mwenzao Korogwe katika sherehe za kumaliza shule amefariki dunia leo KCMC..
 
Updates..Inasemekana mwanafunzi alikuwa akiwaonesha wenzake kwamba anajua kuendesha gari, ndipo aliposababisha ajali hiyo katika viunga vya shule.

Polisi wanaendelea na uchunguzi, ila muda huu huyo binti yuko chini ya ulinzi wa polisi pamoja na wazazi. Mahafali hakuna tena baada ya kadhia hiyo. Bado naendelea kusaka jina la huyo denti na waliojeruhiwa, nitatuma majina muda si mrefu
 
ujuaji ni gharama sana kwa watoto wa siku hizi.aliona akimaliza mtihani then akaendeshee kwao walimu hawawezi kujua kama yeye anajua kuendesha ama wanafunzi wenzake hawawezi kutambua uwezo wa wazazi wake na jinsi anavyopendwa.mbaya sana hii kwa watoto wetu.tuwafunze kuridhika wanetu.jambo zuri halihitaji utambulisho wenyewe wataona na kujua mhusika ni nani.
 
More Updates....Mwanafunzi aliyegonga wenzake anaitwa 'KIBIBI MMASA BAKARI.'
Waligongwa (hali zao bado zina utata) ni hawa wafuatao:-

1. Wakonta Kapunda
2. Lulu Calisty
3. Vicky Mtwale na
4. Nancy Juma

Nawapa pole sana waliopatwa na mkasa huu.
More updates coming......
 
Updates..Inasemekana mwanafunzi alikuwa akiwaonesha wenzake kwamba anajua kuendesha gari, ndipo aliposababisha ajali hiyo katika viunga vya shule. Polisi wanaendelea na uchunguzi, ila muda huu huyo binti yuko chini ya ulinzi wa polisi pamoja na wazazi. Mahafali hakuna tena baada ya kadhia hiyo. Bado naendelea kusaka jina la huyo denti na waliojeruhiwa, nitatuma majina muda si mrefu

Polisi bana uchunguzi huo unaweza chukua hata mwaka mzima
 
Updates.. Polisi wanaendelea na uchunguzi, ila muda huu huyo binti yuko chini ya ulinzi wa polisi pamoja na wazazi

Poleni sana wahusika wote.

Sasa katika tukio kama hili POLISI WANAFANYA UCHUNGUZI!!!!!!! kila kitu kipo wazi, mashahidi wapo, mtuhumiwa yupo......


Ni uchunguzi gani kama si kutaka kupeleleza labda mzazi ni mkuu Serikalini au ana pesa za kuwamwagia mchele ili wapoteze ushahidi!!!!!

Mwisho watasema "KOSA LA MAREHEMU"

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
More Updates....Mwanafunzi aliyegonga wenzake anaitwa 'KIBIBI MMASA BAKARI.'
Waligongwa (hali zao bado zina utata) ni hawa wafuatao:-

1. Wakonta Kapunda
2. Lulu Calisty
3. Vicky Mtwale na
4. Nancy Juma

Nawapa pole sana waliopatwa na mkasa huu.
More updates coming......
asante kaka kwa updates
 
Siku zote kujifanya unajua wakati hujui mwisho wake ni aibu.Pole majaruhi nawatakia kila la kheri wapone haraka
 
Back
Top Bottom