Mwanafunzi aliyepotea kwa siku 35 adai aliondoka Shuleni baada ya kubakwa na Mwalimu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Mwanafunzi kidato cha tano wa Shule ya Sekondari Panda hill, Esther Noah (18) amesema chanzo cha kutoroka shuleni ni kunyanyaswa kingono na mwalimu wa shule hiyo anayejulikana kwa jina la mwalimu Jimmy.


 
Kwajinsi anavyonyoosha maelezo ni kama Mwl. Jimmy anaangushiwa jumba bovu..
Kwa haiba na muonekano wake na uongeaji wake wa kujiamini huyu sio mtoto wa kuokotwa na kuhisaniwa na mtu baki.
Hivi kweli bint wa kidato cha tano kama alitoroka shuleni kwakukimbia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwanini asikimbilie nyumbani kwao au hata kumpigia simu mama yake na kumweleza.
Pia sitaki kuamini kuwa huyo msamalia mwema kuwa hakuwa na uelewa kuwa kukaa na mtu usiyemfahamu nyumbani kwako bila kutoa taarifa kwa Mjumbe/Mwenyekiti wa kitongoji au hata kuripoti kituo cha polisi.
 
Dogo kapangwa uyo aseme nni, kwa muuza mkaa alikua anafanya nn mpka chanzo kiwe kwa mwalimu??? Tunamsubiri mwl jimmy aongee
 
Siku zote binadamu atakukumbuka na kukupenda kama kuna kitu flani ananufaika kutoka kwako. Hata mwanafunzi pia atampenda sana mwalimu wake kwa sababu anamfundisha lakini akishamaliza shule anamwona mwalimu kama takataka, otherwise he/she will keep on remembering you if you are rich, famous or beautiful
 
Sipo upande wowote lakini huyu dogo, kapangwa!
Kwanza kwa nini basi hayo asingeyasema siku ile ama mapema zaidi, ichukue siku kadhaa ndio aseme hayo?
Je hiyo media iliyomrekodi kabla ya kuongea hayo si walimpa hints za kipi aongee na kipi asiongee( kama ilivyofanyika kwa Feisal), maana bila shaka ni utaratibu wa kawaida, sasa kupangwa hapo ni lazima!
Inavyoonekana huyo mwl ni wale ambao wapo strict sana, ikizingatiwa alikuwa mwl wa nidhamu hivyo pengine baadhi ya wanafunzi walikuwa hawampendi ikiwemo huyu dogo, akaona kwenye hili ndio pa kumnyoosha!
Kuna sehemu niliona kuwa huyo dogo akiwa form 4 aliwahi kutoroka tena, je sababu ilikuwa ni kunyanyaswa kingono?

Btw ngoja tusikilizie upande wa pili!
 
Dogo kapangwa uyo aseme nni, kwa muuza mkaa alikua anafanya nn mpka chanzo kiwe kwa mwalimu??? Tunamsubiri mwl jimmy aongee
Mwalimu Jimmy tutamsemea sisi, kukaa kimya ni busara, uongo ni jambo la muda tu, Bali ukweli usimama daima.

Kwa sasa issue muhimu ni bandari zetu, hawawezi kututowa kwenye mstari kitoto namna hii.
 
Mimi nilichogundua, haka katoto kameamua rasmi kuichafua shule ya Pandahill, lakini pia kujaribu kumharibia kazi yake huyo mwalimu Jimmy!

Ingawa naamini vyote viwili havitafanikiwa. Maana siku zote kwenye ukweli, uongo hujitenga. Huyo mtoto kabla ya kulalamikia kubakwa na huyo mwalimu, angetujibu haya maswali yetu kwanza;

1. Kwanini baada ya kubakwa hakutoa taarifa kwa kiongozi wake wa bweni, Matron, Mkuu wa shule, nk?
2. Kwanini baada ya kutoroka shule, hakutoa taarifa kwa wazazi wake juu ya hilo tukio la ubakaji? Au hata kuwapigia tu simu ili kuomba msaada?
3. Kwanini alipotoroka alikimbilia kwa muuza mkaa (baba Jose), aliyeishi naye kinyumba kwa zaidi ya mwezi mmoja mpaka huyo Baba Jose alipoenda kumuombea hifadhi kwa mama muuza genge? (Na inawezekana ni baada ya Rc wa Mbeya kutangaza lile dau la mil. 5 bila shaka, akaona mambo yatakuwa magumu kwake)
4. Kwa nini alipokuwa kwa mama muuza genge alidanganya taarifa zake muhimu kama majina yake, mahali anapotokea, shughuli anayofanya, nk?

Ajibu kwanza haya maswali yetu, ili tuone ukweli ulipo.
 
Kesi ilikuwa simple sana
Baada ya kubakwa angeenda polisi kabla hata ya kuoga. Sasa yeye kaenda kukaa kimya ndio anaongea baada ya mwezi na zaidi
 
Mwanafunzi kidato cha tano wa Shule ya Sekondari Panda hill, Esther Noah (18) amesema chanzo cha kutoroka shuleni ni kunyanyaswa kingono na mwalimu wa shule hiyo anayejulikana kwa jina la mwalimu Jimmy.


View attachment 2675660
Najiuliza maswali;
1. Baba Jose ni nani kwake?
2. Kwanini hakwenda kutoa taarifa kwa mkuu wa shule?
3. Wakati mwalimu anamfuata bwenini alikuwa peke ake?
 
Back
Top Bottom