Mwanafunzi afia kambini JKT Tabora

Mwanafunzi afia kambini JKT Tabora

So sad,najua uchungu wa huko japo sijawahi na sitakwenda ng'o,my girlfrend(awamu ya kwanza) alikuwa analalamika mda wote,ukiumwa hakuna anaejali na ukifa ndio furaha yao mana wanapandishwa vyeo,I was so worried kila alipougua anapewa panado na siku moja ya kupumzika bila kujali amepona siku ya pili lazima aende mzigoni hata kama amemeza vidonge vikali na drip za ma quinini.
SO SAD HATA KAMBI YAO KIGOMA ALIFARIKI MVULANA MMOJA KWA MALARIA NI WA MOSHI,chanzo ni uzembe alikuwa mgonjwa alipoenda hospitali akapewa panado na usiku akazidiwa na walipomrudisha hospitali akawa ameaga dunia,TAARIFA ZA KIFO ZILIKA MAPEMA NYUMBANI MANA WENZAKE WALIPIGA SIMU,cha kushangaza kifo kile kiliwafurahisha watoa mafunzo,nilipouliza iweje mtu afe wengine washerekee nikaambiwa WATAPANDISHWA VYEO WOTE,whatr a foolish?AFU WALIPOENDA KUZIKA WAKAONGOPA MDA ALIOKUFA KWENYE RISALA MANA HAWAKUJUA KAMA FAMILIA ILIELEZWA KILA KITU.
Pole sana mkuu. Girlfriend wako alirudi salama?
 
Kule kutibiwa ni usiku sana 11 na hupewi mapumziko unaendelea na mafunzo kama kawa, hivi ukikataa kwenda huko inakuwaje? maana mimi mwanangu simpeleki huko.
 
Kule kutibiwa ni usiku sana 11 na hupewi mapumziko unaendelea na mafunzo kama kawa, hivi ukikataa kwenda huko inakuwaje? maana mimi mwanangu simpeleki huko.
Atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kukosa uwezo wa kudahiliwa vyuoni.
 
poleni sana kwa msiba wa ghafla, ila mammbo ya HAPA 6 week kweli yanhitaji ule msemo wa "kazi ya jeshi ugangamale",
jeshi liboreshe mfumo wake wa mafunzo ili kuendana na hali ya maisha ya vijana wetu wa sasa na sio kutumia msuli tuuuu.
 
Hiko chama mwanangu haendi ng'o. Watoto wenyewe wawili tu na nimewapataje kwa mbinde. Nitakaa nao hapa dukani wanangu loh. Innalillahi wainnailayhi rajuun.
 
Hakika jeshini wanacheza sana na afya za binadamu. Nakumbuka miaka yetu ukiumwa kwanza hadi upewe pass ya kwenda hospital hiyo process tu unaweza kufa. Na kama unaumwa kiasi gani hakuna chakula cha wagonjwa. Wenzetu walikufa sana kwa uzembe. Yaani udhaifu, udhaifu kila eneo.
 
Shiittt!! Asije kuwa alibakwa, wazazi/ndugu waombe uchunguzi. R.I.P
Pia wanajeshi huwa hawana muda mtu akiugua mi nadhani huyo marehemu alionesha dalili na wao wakadharau.

yawezekana wewe ni mbakaji ndiyo maana unaweza kuyawaza haya matendo machafu
 
Unaijua malaria vizuri ndugu kifarutz?? Ndio inaongoza kuua mbele ya ukimwi na kansa, sasa wewe unasema inatibika kirahisi. Tupime maneno mengine jamani. Rip halima
 
Hatua zipi mkuu.
Ninaitafuta sheria ya JKT ila hili hapa tangazo lao

TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2013 NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KATIKA MAKAMBI YA RUVU PWANI, MGAMBO TANGA, MSANGE TABORA, BULOMBORA KIGOMA, MARAMBA TANGA, RWAMKOMA MARA, MLALE RUVUMA NA KANEMBWA KIGOMA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI HAYO TAREHE 24 JUNI 2013 KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI.

VIJANA HAO WARIPOTI KATIKA MAKAMBI WALIYOPANGIWA KAMA ILIVYOONYESHA KATIKA TOVUTI YA JKT Jeshi la Kujenga Taifa. ATAKAYERIPOTI KAMBI AMBAYO HAKUPANGIWA HATAPOKELEWA. VIJANA HAO WALIPOTI WAKIWA NA VYETI VYA LEAVING VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA KWA UTHIBITISHO

INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

VIJANA WATUNZE TIKETI ZAO WALIZOTUMIA KWENDA KATIKA MAKAMBI YA JKT. NAULI ZAO ZITAREJESHWA NA JKT WATAKAPORIPOTI KAMBINI.

VIJANA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA PILI NI WALE WALIOFAURU KWA DIVISION I, II NA BAADHI YA DIVISION III MCHEPUO WA SAYANSI.

VIJANA WA KIDATO CHA SITA 2013 AMBAO MAJINA YAO HAYAKUORODHESHWA KATIKA TOVUTI HIYO, WATAJIUNGA NA JKT AWAMU YA TATU MWEZI SEPTEMBA 2013.
 
Tatizo la mafunzo ya jeshi ukisema unaumwa wanajua we unategea, hivyo wanazidi kukupa makaz na mazoez makali hatimae unakufa!!!....inauma sana kwakweli!
 
Mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya sekondari Loyola Halima Kitangila amefariki dunia huko Msange Tabora JKT kwa madai ya kuugua maleria.

My take
Kuna haja ya serikali kuangali utaratibu wa mafunzo hasa kwa watoto wa kike ambao hawaendi JKT kujitolea. RIP Halima.

Source: Tanzania Daima

Mimi siku zote nimeutilia mashaka sana utaratibu wa serikali ya ccm ya kuchukua kila maamuzi kisisasa siasa na kiushabiki shabiki. Sina uhakika na maandalizi yaliyofanywa na serikali ya kuiawalazimisha watoto kwenda jkt, kama maandalizi hayo yaligusa mahitaji yote muhimu ya binadamu.

Kwanza sielewi ulazima huo umekurupushwa na n ini na sina uhakika kama hicho kilichokurupusha mawazo hayo kwamba jibu lake ni jkt ya lazima.

Sina hakika kama hawa maafande kweli wametayarishwa kwa upande wa customer care au ni zile zile akili za kutaka kuona "Ngedere na Binadamu nani ni mstahimilivu kwa maumivu"

Sina hakika na huduma za kibinadamu ikiwa ni pamoja na huduma za afya zipo kwa kiwango gani ikiwa ni pamoja na wataalam. Je viwango bora kama vipo ni kwa makambi yote?

Ikumbukwe pia viwango na aina ya mazoezi ni taaluma ambayo inatakiwa kuendana na afya za watu. Hapo zamani ukakamavu ulianzia majumbani kwa kazi nguvu, mashuleni michezo, mazoezi na kazi za mikono kwa wingi hivyo hata mtu alipofikia kwenda jkt, hapakuwa na utofauti kama ilivyo leo.

Naomba sana serikali iliangalie hili suala kwa undani. Lipua lipua ya serikali ya ccm inayotumaliza watanzania kwa madawa fake, maji machafu, kukosekana kwa huduma za afya, elimu duni, udini, maendeleo duni na uccm, sasa inaonekana kwenda kumaliza watoto wetu kwa janga la jkt. Ni kwa sababu hakuna kitu serikali ya ccm inachofanya kwa sasa ambacho kiko kwenye kiwango ama chenye lengo jema kwa wa Tanzania.

RIP Halima
 
Hili suala la jkt kwa wanafunzi limepitishwa na watu wasio na fikra, kama busara ingetumika kigezo cha mafunzo kisingekuwa kumaliza form six au kupata div 1,2 or 3 wangefuata utaratibu wa kuangalia na kupima afya za candidates wanaofaa kujiunga na mafunzo haya. Tatizo once umeingia huko jeshini huwa hakuna utaratibu wa kupimwa au kuangaliwa una hali gani sana sana ukionekana una C nyingi unapewa adhabu kwamba ni mzembe.

Kwakuwa lengo la mafunzo haya ni kuwafanya wanafunzi wasigome au wasiunge mkono vyama vya upinzani pindi wawapo vyuoni, kilichobaki ni kumuomba Mungu awalinde na maafa ya vifo huko makambini walipo
 
Na inawezekana alireport anaumwa wakaona hataki kufanya mazoezi na makazi yao.....UTII WA SHERIA BILA SHURUTI....Usije ukawa ulitumika hapo

Ni kweli nasikia ali report lakini hawakutilia maanani wakidhani ni mvivu mi nadhani vijana wa kiume tu.ndio waende huko sisemi kwamba hawataumwa at list at list miili yao inaweza vumilia shida..

Imagine wadogo zetu siku zao za mwezi zikifika akihitaji vifaa lazima aombe..

Watoto wengine wamelelewa maadili tofauti wana aibu sana

Serikali iangalie upya kwa dada zetu kwenda huko
 
Wazazi wengi wana wasiwasi na JKT hasa kwa watoto wa kike. Kama hali ikiendelea watoto kupoteza maisha nina mashaka kama huu mpango utaendelea.
 
INNA LILLAH WA INNA ILLAH RAJIUUN!!

Duh!Kumbe mpaka wanakufa kabisa huko?Mimi nilifikiri ni laini laini tu kama ya wale wabunge waliokwenda kipindi kile wakatoka na vitambi vyao.
 
Napenda kuwa shauri CDM huku ndio kuzuri kuwapeleka vijana wao maana wakitoka huko hata jeshi litakuwa upande wa CDM
 
Ninaitafuta sheria ya JKT ila hili hapa tangazo lao

TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2013 NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KATIKA MAKAMBI YA RUVU PWANI, MGAMBO TANGA, MSANGE TABORA, BULOMBORA KIGOMA, MARAMBA TANGA, RWAMKOMA MARA, MLALE RUVUMA NA KANEMBWA KIGOMA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI HAYO TAREHE 24 JUNI 2013 KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI.

VIJANA HAO WARIPOTI KATIKA MAKAMBI WALIYOPANGIWA KAMA ILIVYOONYESHA KATIKA TOVUTI YA JKT Jeshi la Kujenga Taifa. ATAKAYERIPOTI KAMBI AMBAYO HAKUPANGIWA HATAPOKELEWA. VIJANA HAO WALIPOTI WAKIWA NA VYETI VYA LEAVING VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA KWA UTHIBITISHO

INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

VIJANA WATUNZE TIKETI ZAO WALIZOTUMIA KWENDA KATIKA MAKAMBI YA JKT. NAULI ZAO ZITAREJESHWA NA JKT WATAKAPORIPOTI KAMBINI.

VIJANA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA PILI NI WALE WALIOFAURU KWA DIVISION I, II NA BAADHI YA DIVISION III MCHEPUO WA SAYANSI.

VIJANA WA KIDATO CHA SITA 2013 AMBAO MAJINA YAO HAYAKUORODHESHWA KATIKA TOVUTI HIYO, WATAJIUNGA NA JKT AWAMU YA TATU MWEZI SEPTEMBA 2013.

Nasindwa kuelewa kwa nini bunge letu lilipitisha sheria kama hii ya kuwarazimisha vijana wetu kwenda kambini bila kujali hata afya zao.
 
Back
Top Bottom