Mwanadamu sawa na kuku bandani

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
14,376
14,870
Wakuu salamu zenu.

Nimekaa na kutafakari hali ya maisha yetu sisi binadamu nimeona yapo mithili ya maisha ya kuku bandani.

Kuku anafunguliwa asubuhi kutoka bandani hapo anapata "uhuru" wa kuvinjari na kujitafutia riziki, katika kipindi hicho kumswaga ili arudi bandani sio kazi ya kitoto, ni hadi jioni atakaporejea mwenyewe pindi ameshiba kupitia riziki ya jasho lake, akiwa bandani hapo unaweza kumfanya kitu chochote utakacho kwani wahenga walisema; kuku mali yako manati ya nini ?!, wakati huo unaweza hata kulitia moto banda lote na kuku akateketea au ukaamua kumkamata na kumchinja kwa kitoweo kwani huyo si mali yako bwana!!!.

Kipindi huyo kuku anapokuwa vichakani akijitafutia riziki huko anaweza kugongwa na nyoka, akaliwa na mbwa, akaibwa nk na ukamkosa kabisa, si mnajua lakini??!!.

Sisi binadamu hapa duniani tupo mithili ya kuku bandani, banda letu ndio hii dunia, kila kukicha tuna amka kwenda kutafuta riziki na mihangaiko mingine na jioni kurejea majumbani mwetu, tofauti kubwa kati yetu na kuku bandani ni kwamba angalau kuku anao uhuru na nafasi kubwa ya kutoweka moja kwa moja na mwenye kuku asimpate milele kinyume chake sisi binadamu haiwezekani kumuepuka mmiliki wetu kwani maisha na shughuli zetu zote tunazifanyia BANDANI (Duniani), siku mwenye banda akikasirika na kuamua kulitikisa banda japo kidogo tu, looo!! mara tetemeko la ardhi, Tsunami, mara mafuriko, ukame, vimbunga, magonjwa nk hayo ni baadhi ya majanga ambayo mwenye banda akiamua kuyaleta basi hatuna pa kukimbilia wala pa kwenda kushitaki, si mwenye banda kaamua!!😏
Mfano angalia Turkey na Syria hali inatisha sana kuhusu tetemeko la ardhi.

Basi ndugu zangu, tunapoishi duniani (bandani) katika hali ya faraja na mafanikio tuchukue nafasi hizo kumuabudu na kumshukuru mwenye banda ambaye ndiye ametuweka humu bandani, tumshukuru na tumuabudu asije tujaribu kwa mitihani hiyo migumu wanayopitia binadamu wenzetu lau kama.ni adhabu badi atusamehe makosa yetu na atuepushe na adhabu.

Watu watauliza je; huyo.mwenye banda ni nani??, Mwenye banda (dunia) ni MUNGU mtukufu, sisi ni viumbe wake aliyetuweka humu duniani bila ya sisi kutaka tuwepo humu duniani hivyo sisi ni mali yake tutake tusitake, imepita hiyo.

Nawaambia Atheists; Hatuna ujanja aliyetuweka bandani ni MUNGU kama hampendi ondokeni bandani.
 
Ni juzi tu hapo umetoka kuachia uzi ukisema ulimwengu huu ni mzuri kuishi na kushangazwa na Atheists jinsi wasivyokuwa convinced na uzuri huo kiasi cha kuamini uwepo wa Mungu

Leo tena unakuja kuonesha matatizo ya ulimwengu huu tena kwa mifano iliyo hai (Turkey na Syria)

Sasa tushike lipi?
 
Ninapozungumzia uzuri wa dunia ninamaana ya maumbile yake na vilivyomo, maumbile yake.na vilivyomo ni ishara tosha kwamba yupo aliyeiumba hii dunia naye ndiye tunamuita Mungu, au a conscious disciplined being, Super being nk.

Ninapozungumzia mambo yanayotokea duniani (mambo hasa yanayomsibu mtu) ni lazima uyaweke katika mafungu mawili;

1-- Mambo yote ya raha, faraja, mafanikio nk.
2-- Mambo shida, majanga, misiba nk.

Mambo hayo mawili hayaondoi nafasi ya dunia kuumbwa bali mambo hayo ni sehemu ya taratibu za Mungu kuwafanya watu wamjue Mungu, mfano; tuapopata faraja, raha nk huo ni wakati wetu wa kumshukuru na kumkumbuka Mungu tunapofanya hivyo ndivyo Mungu anatuongezea faraja zaidi.

Upande wa.majanga ni kwamba; Watu wskati mwingine tunapokuwa kwenye faraja huwa tunajisahau kumkumbuka Mungu hivyo wakati mwingine Mungu hutumia njia kali au adhabu kali au kutupa mtihani ambao kwao tuweze kumkumbuka kwa faida yetu, hivyo yale unayoyaona majanga, shida nk huwa katika muundo huo kwani Mungu ndiye aliyetuumba hivyo anazijua nafsi zetu kuliko jinsi sisi tunavyozijua nafsi zetu.

Kifupi ndivyo hivyo.
 
Majanga yanayotesa watu hayapaswi kuwepo kwenye kazi iliyofanywa na Mungu mwenye upendo wote
 
Majanga yanayotesa watu hayapaswi kuwepo kwenye kazi iliyofanywa na Mungu mwenye upendo wote

Hayo unayoyaona ni mateso kutoka kwa Mungu yanaweza kuwa ni ama mtihani au adhabu, mtihani ni kuwapima watu je watamtegemea Yeye katika shida, adhabu ni kuwaadhibu wakosefu baada ya wao kumsahau na kutenda maovu nk, mara nyingi Mungu huwa haadhibu (watu) mtu kabla ya kumuonya/kumpa ishara ya onyo na huo ndio upendo wake kwa binadamu, mfano adhabu ni sawa na wewe kumnywesha mwanao dawa chungu ili apone maradhi, huo ni upendo.

Kifupi ni kwamba tumo ndani ya "banda" ni lazima tutii na tufuate sheria za bandani, hatuna njia sisi tunamilikiwa na Mungu.
 
Anavyokupa hiyo mitihani ili akupime anataka kugundua nini ambacho hakijui ilihali yeye ni mjuzi wa yote?
 
Back
Top Bottom