TANZIA Mwanadada Azra Ronaldo akutwa amefariki chumbani kwake

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,704
Reaction score
7,409
Mwanadada anayefahamika kama Azra (Maarufu kama Ronaldo) amekutwa amefariki dunia ndani kwake kisarawe huku mwili wake ukiwa umevimba, tukio hilo limetokea leo Jumatano Juni 11, 2025 baada ya majirani kubaini harufu katika chumba chake.

Mdau wa Michezo Seleman Kaniki ambaye alikuwa akimfahamu dada huyo amethibitisha kifo chake baada ya Polisi kufika eneo la tukio.

Azra Ronaldo alikuwa Mwanadada maarufu mitandaoni kwa utashi wake mkubwa wa kucheza mpira mitaani.

Mwanadada huyu amefia Kisarawe na polisi wa kituo cha Chanika walivunja mlango siku ya jumatano na kuukuta mwili wake umevimba na kutoa harufu.

Azra alikuwa mpiga danadana maarufu wa mpira wa miguu kwa kutumia miguu, kichwa, uso, mdomo na shingo.
Majirani walitoa taarifa polisi kuwa wanahisi harufu kali chumbani kwake na pia hawamuoni kwa siku kadhaa.

RIP Azra uliitendea vyema burudani la soka.

View: https://youtube.com/shorts/Cn2en8X4CKw?si=3Wj00z5384oCbf80
 
Marehemu alikuwa hajafika 40? Anaonekana mkubwa
Machache kadhaa niliyosikia kutoka kwa mjumbe ni kwamba huyo dada alikuwa anakaa kwake, peke yake, hajaolewa ila ana mtoto mmoja kama sijakosea. pia alikuwa anasumbuliwa na kifafa. Huyo mjumbe ni fundi ujenzi kwahiyo ni stori tulikuwa tunapiga huku tuko site.
 
Back
Top Bottom