Mwana JF anusurika kifo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,833
Mwana Jamii Forum mwenzetu anayejulikana kwa jina la Azikiwe, jana asubuhi alinusurika kifo baada ya kukumbwa na ajali mbaya.

Alikuwa akiendesha pikipiki ndipo alipogongwa na gari na kumsababishia majeraha makubwa mwilini mwake.

Azikiwe alipata ajali jana asubuhi alipokuwa akiendesha pikipiki yake kwenda kazini akitokea nyumbani kwake maeneo ya Ukonga.

Azikiwe amevunjika mguu na mkono na amelazwa kitengo cha mifupa MOI.

Tumuombee ili aweze kupona mapema.
 
Azikiwe,
Get Well Soon!
Lakini pia hizi pikipiki, barabara zetu na madereva wetu!
Wee acha tuu!.
 
Mwana JF anusurika kifo.
Pole sana, twakuombea upone haraka. Lakini Mikela ungesema Mwana JF apata ajali mbaya, hilo la kutaja kifo huwa sipendi sana kulisikia hata kama amenusurika, otherwise tunashukuru kwa taarifa na tuliopo Dar tukamuone (ila sasa anatumia ID !)
 
mwana jamii forum mwenzetu anayejulikana kwa jina la azikiwe, jana asubuhi alinusurika kifo baada ya kukumbwa na ajali mbaya.
Alikuwa akiendesha pikipiki ndipo alipogongwa na gari na kumsababishia majeraha makubwa mwilini mwake.
Azikiwe alipata ajali jana asubuhi alipokuwa akiendesha pikipiki yake kwenda kazini akitokea nyumbani kwake maeneo ya ukonga.
Azikiwe amevunjika mguu na mkono na amelazwa kitengo cha mifupa moi.
Tumuombee ili aweze kupona mapema.

my fingers xsd for the lad...get well soon!!
 
Praise the Lord!
Pole sana broda, una kundi kubwa la watu hapa wanakuombea salama!
U wll be sound and out soon!
 
Pole sana mkuu Azikiwe,

Mi niko huku ughaibuni maeneo ya Asia, usafiri wa pikipiki ni moja ya usafiri unaotumiwa na karibu kila nchi na kwa kila mwananchi huku, kuna piki piki nyingi sana huku, lakini ajali za mara kwa mara kama Dar hazipo. Watu wanaheshimiana, wanajaliana lakini kwetu bwana madereva wenye magari ndo wenye barabara. Na mwenye gari akiwa nalo kubwa zaidi ndo mwenye bara bara haswa, i hate this basi tu!. Hii inatokana na mfumo mbovu wa utozwaji faini ya makosa barabarani, leseni nazo zinatolewa kiholela kama wauza michicha.

Nachotaka kusema hapa ni kuwa, kuna haja ya kuangalia upya mifumo na sheria za nenda kwa usalama barabarani ili watu tuheshimiane na tuweze kuwa na amani barabarani.

Once again, Get well soon brother!! hakika mungu yupo, utapona mkuu.
 
Pole sana Azikiwe!... Pasco pia najua una-recover kutoka kwenye ajali uliyoipata Dodoma... Pikipiki sooo! Haswa hapa Dar...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom