Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,786
Nimevutiwa sana kujua Historia ya mwanamke shupavu ambaye alikuwa ni mtawala wa kutoka katika kabila la waha wa Jamii ya kitutsi, ukanda wa Kasulu sehemu za Heru Juu.
Mwami Theresa Ntare (1922 - 1999)
Ambapo zama zile jamii nyingi za Kiafrika zilitajwa kuwaweka nyuma wanawake, Mwanamama huyu aliweza kuwa Kiongozi wa Jamii ya Heru huko Kasulu. Hakuishia hapo, mama huyu aliweza kushika wadhifa mkubwa ambapo alikuwa ni mkuu wa machifu akipokea kijiti kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle mwaka 1958.Makabidhiano yalifanyikia shule ya Mzumbe, na mpaka sasa Mzumbe kuna bweni linaitwa Ntare.
Mwami Theresa Ntare alikuwa ni mmoja ya Wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla hata ya Uhuru wa Tanganyika.
Sina details nyingi za huyu mama, WanaJF kama kuna anayefahamu zaidi kuhusu huyu mama shupavu basi atupe historia yake.
*Mwami ZITTO KABWE sasa hivi ndiye Chifu wa Heru.
------- Nyongeza kutoka kwa wadau--------
IAmShedeOne, anasema
Alipata nafasi ya kwenda kusoma Ulaya enzi ukoloni nafasi maalum za watoto wa machifu.Alihitimu mafunzo ya ya sheria.Alikuwa msaada mkubwa sana wa kisheria wakati wa kudai Uhuru,hasa kwenye mikataba ya kimataifa.
Mengi hayajulikani katika historia ya utoto wa Mwami Theresa Ntare, lakini inaaminika alikuwa mtoto wa kike pekee wa Chifu Ntare. Inaelezwa kwamba Mwami Thereza Ntare alitawazwa uchifu baada baba yake Mwami Ntare kukosa mtoto wa kiume. Baada kutawazwa uchifu ilibidi atafutiwe mchumba kutoka ukoo wa Chifu Lusimbi wa Kalinzi hivyo akawa ameolewa na kijana wa kitutsi kutoka Kalinzi akiitwa Bw. George Shinganya.
Kulingana na mila za Kiha, Mwami haolewi. Akiolewa inabidi ahame milki yake ya Uchifu ili akawe mke wa huyo muoaji. Hivyo basi, Mwami Ntare hakuolewa na Bw. George Shinganya. Bali familia ya Mwami ndiyo iliyolipa mahari kwa familia ya Bw. George Shinganya. Hivyo, Jina la Shinganya likaondolewa na akaitwa George Ntare.
Baadaye ndoa ya Mwami Theresa Ntare na George ilivunjika na Mwami Theresa Ntare akaoana na Mwami Louis Dantes Ngua wa Ufipa(Huyu ana asili ya uchifu wa Ufipa). Kuna nadharia zinazoeleza pia kuwa Mwami Theresa Ntare alipata pia kuwa mke wa Chifu Makwaia wa Usukuma. Lakini hakuna ushahidi wowote juu ya hilo.
Wakati wa zama hizo jamii nyingi za Kiafrika zilitajwa kuwaweka nyuma wanawake hasa katika masuala ya Uongozi. Hilo halikumfanya Mwanamama Mwami Theresa Ntare asiweze kuongoza vizuri na kishupavu jamii yake ya Waha wa Heru huko Kasulu.
Hakuishia hapo, mama huyu aliweza kushika wadhifa mkubwa ambapo alikuwa ni Mkuu wa machifu wote Tanganyika akipokea kijiti kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle mwaka 1958. Makabidhiano yalifanyika shule ya sekondari ya Mzumbe, na mpaka sasa Mzumbe kuna bweni linaitwa Ntare.
Mwani Theresa Ntare aliheshimika kama chifu wa Kasulu yote na sio tu Heru alisimamia vyema msimamo wa Baraza la Machifu mwaka 1958 na kuunga mkono juhudi za TANU katika kudai uhuru.

Aliendelea kuwa Mbunge mpaka miaka ya 1980, lakini kabla ya hapo aliachia uchifu Disemba 9, 1962, Katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam nchini Tanganyika. Hapo alikaribishwa kama Malkia wa Heru kwa Ngoma Maalumu kutoka Ngome ya Malkia wa Heru kwa heshima kubwa.
Inaelezwa alifariki miaka ya 1990 na mara ya mwisho alikuwa akiishi maeneo ya karibu na barabara inayoelekea Munyegera - Kati ya ilipo shule ya msingi na Kahaga Dispensary (kulikuwa na soko hapo kati miaka ya 1985).
Kwa sasa Mwami wa Heru ni Costa Shinganya au Ntare ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mwani Theresa Ntare.
Kuna wanaosema Mbunge wa Kigoma mjini, ndugu Zitto Ruyagwa Kabwe ndiye hasa Mwami wa Waha wote. Lakini hili ieleweke yeye amepewa heshima tu ya Mwami Mpole aliyejulikana kama Ruyagwa.
Huyu ndiye Mwami Theresa Ntare VI, Malkia wa Heru kuanzia 16 Aprili, 1946 mpaka 9 Novemba, 1962.
Matukio mawili yaliyowatokea yeye na Baba wa Taifa ni:
Walizaliwa mwaka mmoja 1922,wamefariki mwaka mmoja1999.
--------------
Mohamed Said, anasema
Tuliyohadithiwa na Wazee wetu Paramount Chief Dantes Ngua na Mkewe Mwami, Theresa Ntare
Ilikuwa mnamo mwezi wa Novemba 1992, mida ya adhuhuri katika mizuguko ya kuwatembelea wakogwe walioshiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingerza.
Safari yetu ilitufikisha nyumbani kwa Alhajj Chief Abdallah Saidi Fundikira eneo la Magomeni Mikumi, Dar es salaam. Tulipata bahati kubwa kwakuwa tulimkuta Chief Fundikira akiwa na rafiki zake Chief Dantes Ngua na Mhe. Joseph Kasella Bantu pamoja na watu wengine wawili, wakiwa katika mazungumzo ya kawaida. Baada ya kuwasalimia, tulikaribishwa tukaketi.
Mohamed Said hakupoteza muda. Aliwachokoza na maswali yahusuyo mambo muhimu wanayoyakumbuka sana katika enzi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Wote walitabasamu huku kila mmoja wao akimuangalia Chief Fundikira kana kwamba wakitaka Mzee Fundikira aanze yeye. Mzee Fundikira akasema kuwa yapo mengi ya kuzungumzwa ila muda ule haukuwa wa kutosha kwa sababu alikuwa ameshauriwa asikae muda mwingi pasipo kupumzika. Masharti hayo alipewa na daktari baada ya kutoka katika mtikisiko wa homa. Na hapo tukatambua kuwa wale wazee walienda kumjulia hali baada ya kupata taarifa ya kuumwa kwake.
Hata hivyo, Mzee Fundikira akanyanyuka huku akisema; “Mohammed, ngoja nikuletee zawadi…” Alipanda ghorofani na kurudi na kitabu kidogo cha kurasa 55 kiitwacho, Ukombozi wa Tanganyika kilichoandikwa na Simon Ngh’waya; na kuchapwa na Chief Printer, CCM Printing Press, Dodoma, 1991. Mzee Fundikira akasema, “huyu mwandishi aliniletea mimi hiki kitabu. Nimekipitia na ninaona kitakufaa.” Mzee akaongeza kusema, “Ni vyema watu waandike watakavyoweza kuandika juu ya yale yaliyotokea wakati wa enzi za kudai uhuru.”
Baada ya hapo yakafuatia mazungumzo machache tena, ya kuagana tu. Mzee Dantes Ngua akatuambia, “karibuni nyumbani, siyo mbali ni hapo jirani huku akituelekeza na kumalizia njooni, mtanikuta.” Mzee Kasella Bantu yeye alituaga akisema yeye atakuwa tayari kwa mazungumzo siku yoyote tutakayopanga na kwamba tukipita kwa Mzee Fundikira itakuwa rahisi kujua alipo na namna ya kuwasiliana nae.
Hivyo wazee wale walipoondoka nasi hatukuwa na haja ya kumchosha Mzee Fundikira ingawa hakuonyesha dalili ya kutaka tuondoke kwa haraka. Tukamuaga na kuelekea kwa Chief Dantes Ngua.
Wakati tukiwa kwa Chief Fundikira, Mohamed Said alimfahamisha Mzee Ngua kwamba alikuwa akiwafahamu baadhi ya vijana wake ambao baadhi yao wakati ule wakiongoza kampuni ya kuingiza magari kupitia Bandari ya Dar es Salaam. Hiyo ilituongezea ukaribu kwa Mzee Ngua.
Mazungumzo yetu kwa Mzee Ngua hayakuchukuwa muda kuanza. Mzee alianza kwa kutufahamisha kuwa yeye kimila ni Paramount Chief wa Ufipa ambako makabila ya Wafipa wakati huo yalienea kutoka maeneo ya Rukwa hadi kaskazini mwa Zambia ambako wakijulikana pia kama Wawemba. Hivyo yeye alikuwa ni Chief Mkuu (Paramount Chief) wa machifu wadogo, wajumbe na wazee wa koo mbalimbali, wakiongoza katika maenneo yao. Alitujulisha pia kuwa na Mkewe Bibi Theresa Ntare alikuwa Mwami, yaani Chief Mkuu wa kabila la Waha wote waliokuwepo maeneo ya Kigoma hadi katika maeneo ya Burundi. Makao yake makuu kiutawala yalikuwa Kasulu.
Jinsi Dantes Ngua na Julius Nyerere Walivyokutana kwa Mara ya Kwanza
Chief Dantes Ngua alituhadithia jinsi walivyokutana na Mwlalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza.
Chief Dantes alisema:
''Wakati huo nilikuwa Mwanafunzi Tabora School mwaka wa pili. Ilikuwa kipindi cha kupokea wanafunzi wapya. Wakati huo pale palikuwa na utaratibu wa kuwathamini watoto wa machifu. Waliorodheshwa na kupewa Head Prefect kiranja wao. Pale shuleni pia wanafunzi walikuwa wakipewa vyakula vya kurutubisha afya; karanga na maziwa. Watoto wa Machfu pia walikuwa wakipata ration (mgao) huo; ila kwao ulikuwa mkubwa kiasi. Hivyo mimi nilikuwa Head Prefect wa wanafunzi ambao ni watoto wa Machifu.
Siku moja wakati wanafunzi wapya wakipokewa pale shule, niliitwa ofisi ya Head Master. Nilipofika nikawakuta wanafunzi wapya wawili. Head Master akaniambia, ‘Hawa ni wanafunzi. Ni watoto wa Machifu.’ Kisha akanitajia majina yao. Mmoja alikuwa ni Julius Nyerere na mwengine Wilbert Chagula.''
Chief Dantes alituambia kuwa yapo matukio mengine muhimu ya kipindi cha mapambano ya kudai uhuru na katika muelekeo wa kupatikana uhuru. Matukio yaliyojaa visa vya wakoloni na vituko vya Nyerere. Mama Theresa alikuwepo pale sebuleni katika yale mazungumzu, bahati mbaya hakuwa akijisikia vizuri. Lakini alikuwa na shauku ya kuzungumza mengi kuhusu jinsi alivyoshiriki mapambano yale ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Aliyotuhadithia Mwami Theresa Ntare Jinsi Alivyoipa Nguvu TANU Buha
Mzee Dantes alitushauri tumsikilize Mama Theresa kisha tumpe nafasi akapumzike. “Mama yenu msimuone hivyo, ana mengi sana,” alisema Chief Ngua, na kuongeza, “Tena yeye uhuru ulipopatikana alipewa uwaziri.” Kwa maneno hayo ya sentensi ya mwisho ya Mzee Dantes Ngua, Mwami Theresa akaitikia; “Ah, nikikumbuka yale niliyokumbana nayo katika mapambano ya kudai uhuru wetu na kitendo nilichofanyiwa na kuondolewa uwaziri, ah, basi tu.”
Mwami Theresa hakutaka kuzungumzia kilichomtoa katika uwaziri. Aliamua kutuhadithia kisa cha mpambano wake na maafisa Wazungu wa serikali ya kikoloni kwa ajili ya kuipa nguvu TANU ili nchi hii iwe huru:
''Serikali ya kikoloni haikutaka sisi machifu tuwe katika siasa hasa kuisaidia TANU. Hata hivyo tukiwa wananchi na viongozi wa wanchi wanaotaabika chini ya utawala wa kikoloni, tuliiamua kushiriki siasa kwa siri na kuipa nguvu Tanu ili tujitawale. Kuna wakati taarifa zilinifikia kwamba ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikuwa unakuja kusikiliza maoni ya kudai uhuru. Utaratibu wa kikoloni ni kuwa chama japo ni cha kitaifa, kilitakiwa kipate pia usajili katika kila jimbo. Hivyo TANU ikidai kuwa inawakilisha wananchi wote, watawala wa mikoa walikuwa wajiandaa kukisuta kuwa si kweli na kuonesha sehemu ambako hakikuwa na wanachama. Moja ya sehemu hizo wakoloni waligundua ni katika himaya ya utawala wangu wa Buha. Waligundua TANU haipo kwa Waha. Taarifa za siri zikanifika kwa wakoloni wataiambia tume hiyo ya UNO juu ya hilo. Nikaamua kuchukua hatua kwa siri na kwa haraka.
Nilitoa pesa zangu binafsi na kuagiza haraka kadi za TANU elfu tatu. Zikaletwa kwenye vikapu. Nikaweka mkakati wa siri na watu wangu jinsi ya kuzigawa kadi hizo kwa haraka kwa wananchi wa maeneo ya Buha. Majira ya saa tatu za usiku lilipigwa baragumu la wito wa dharura watu waje kwa Mwami. Wito ulifikishwa kwa haraka kila eneo. Wananchi wakamiminika. Eneo la makazi yangu lilikuwa na uwanja mkubwa sana. Niliwapanga watu wangu katika lango la kuingilia wakiwa na vikapo vilivyokuwa na kadi za TANU na karatasi zake za risiti.
Kila mtu alipoingia alipewa kadi na risiti isiyoandikwa. Kisha akaambiwa aifikiche kadi na hiyo risiti pasipo kuichana. Na asiongee chochote hadi afike lango la nyuma ambalo ni la kutokea. Hapo palikuwepo watu wamejipanga katika meza. Walipofika hapo walimpa huyo aliyekuwepo katika meza hiyo kadi na risiti kisha kumtajia majina yake, anakoishi nk.
Yule karani aliiiandika ile kadi na risiti kwa tarehe za miezi ya nyuma, meza nyingine ilipiga muhuri. Mwisho mwenye kadi aliambiwa kuwamba ameisha kuwa mwanachama wa TANU wa muda mrefu. Akiulizwa atoe kadi na aitetee TANU pasipo kumtaja Mwami wala kilichotokea usiku ule; kwake hicho ni kiapo cha utiifu kwa Mwami. Aliruhusiwa na kusisitizwa kuitunza hiyo kadi na risiti yake.''
Mwami Theresa alitufahamisha kuwa zoezi lile lilikamilika mnamo saa tisa za usiku. Meza zikaondolewa na wafanyakazi wakatawanyika na kwenda kulala. Mzee Ngua akasema, “Sisi machifu tulikuwa na utiifu mkubwa toka kwa wananchi. Hata hili tatizo la Ukimwi, kama ingelikuwa enzi zile, tungetoa tamko la muongozo wa kuacha zinaa, Ukimwi ungeishatokomezwa.”
Mwami akaendelea kutuhadithia:
''Ilipofika alfajiri karibu ya saa kumi na mbili za asubuhi, nikaambiwa kuna msafara wa magari ya polisi unaelekea kwenye makazi yangu. Niliyategemea hayo, maana vibaraka wapelelezi walikuwepo enzi hizo. Hata hivyo, kwa tukio lile walikuwa wameshachelewa. Mimi siku ile sikuwa nimelala wala kupata usingizi. Nilikuwa katika nguo zangu za kawaida. Nilipoletewa taarifa ile, nikaingia chumbani na kuwaambia walinzi wangu kuwa wakifika, kwanza kuweni imara kuhusu siri ya kilichotokea usiku.
Pili waambieni kuwa Mwami hajamka. Ngoja tukamwamshe. Kisha mje kunigongea. Na kwamba nitakapotoka na kufokeana nao, nyiye onesheni utiifu kwangu na kuwakasirikia wao; wala msioneshe kuwahofu. Mkakati huo ukaeleweka.''
Mwami Theresa akatueleza kuwa wakaingia maofisa wa polisi akiwemo mmoja Mzungu na DC (District Commissioner) Mzungu pia. Wakauliza kama Mwami yupo. Wakaambiwa amelala, na kwamba wanaenda kumuamsha. Walinzi wa Mwami wakaenda kungonga mlango wake. Baada ya muda akaitikia na kuuliza kwa sauti ya juu, “kunanini mnanigongea usiku huu?” wakamjibu, “kuna Bwana DC na mkubwa wa polisi.” Mwami akajibu kwa sauti kali, “wanataka nini wakati hakujakucha ngoja nije.”
Akatuambia kuwa alijiandaa kwa kuvaa “night dress” akatimua nywele zake kisha akajiviringisha shuka na blanketi akatoka akiwa ameshikilia na alipofika sebuleni na kuwaona hakuwa salimia wala kusubiri salam zao. Alianza kwa kuwafokea kwa lugha ya Kiingereza:
“How dare you wake me up at this time of the hour? Can you do this to the Queen of the UK? Don’t you know I am the the Queen of Buha? Is it because I’m an African that’s why you are doing this to me? I will file my complaints and report you to the Governor for this.”
Mwami akatuhadithia kuwa wale maofisa wa kikoloni walichanganyikiwa na kuanza kujitetea kuwa walipata taarifa kwamba alikuwa akigawa kadi za TANU usiku. Akawajibu, “Je, mmkuja na ‘’search warrant?” Kisha akaongeza kwa kuwaambia, “Nyiye askari wanaume watupu pamoja na DC mmekuja kunipekua mimi mwanamke? Nitamlalamikia Gavana.
Hawakuwa na ‘’search warrant.’’ Mwami akawageukia walinzi wake na kuwataka wawaambie wale DC na mapolisi wake watoke mara moja au wapige baragumu kuashiria Mwami amevamiwa ili waje wamhami. Yule DC na watu wake waliomba radhi haraka na kuondoka.''
Baada ya kutuhadithia kisa hicho Mwami Theresa Ntare alituambia bora turudi pale siku ya Jumamosi iliyofuata kwa mazungumzo na mahojiano zaidi. “Jumamosi mtapata mengi. Maana kuna waandishi Wamarekani watakuja kunihoji kuhusu harakati za wanawake kuhusu kupigania uhuru wa Tanganyika.” Bahati mbaya hatukuweza kupata fursa ya kwenda siku hiyo. Mwami akasafiri. Na hatukuonana nae tena.