Mwami Theresa Ntare anaeleza alivyoiingiza TANU Buha

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
MWAMI THERESA NTARE CHIFU MWANAMKE ANAELEZA ALIVYOIINGIZA TANU BUHA

''Serikali ya kikoloni haikutaka sisi machifu tuwe katika siasa hasa kuisaidia TANU.

Hata hivyo tukiwa wananchi na viongozi wa wanchi wanaotaabika chini ya utawala wa kikoloni, tuliiamua kushiriki siasa kwa siri na kuipa nguvu TANU ili tujitawale.

Kuna wakati taarifa zilinifikia kwamba ujumbe wa Umoja wa Mataifa (UNO) ulikuwa unakuja kusikiliza maoni ya kudai uhuru.

Utaratibu wa kikoloni ni kuwa chama japo ni cha kitaifa, kilitakiwa kipate pia usajili katika kila jimbo.

Hivyo TANU ikidai kuwa inawakilisha wananchi wote, watawala wa mikoa walikuwa wakijiandaa kukisuta kuwa si kweli na kuonesha sehemu ambako hakikuwa na wanachama.

Moja ya sehemu hizo wakoloni waligundua ni katika himaya ya utawala wangu wa Buha.
Waligundua TANU haipo kwa Waha.

Taarifa za siri zikanifika kwa wakoloni wataiambia tume hiyo ya UNO juu ya hilo.
Nikaamua kuchukua hatua kwa siri na kwa haraka.

Nilitoa pesa zangu binafsi na kuagiza haraka kadi za TANU elfu tatu.
Zikaletwa kwenye vikapu.

Nikaweka mkakati wa siri na watu wangu jinsi ya kuzigawa kadi hizo kwa haraka kwa wananchi wa maeneo ya Buha.

Majira ya saa tatu za usiku lilipigwa baragumu la wito wa dharura watu waje kwa Mwami.

Wito ulifikishwa kwa haraka kila eneo.
Wananchi wakamiminika.

Eneo la makazi yangu lilikuwa na uwanja mkubwa sana.

Niliwapanga watu wangu katika lango la kuingilia wakiwa na vikapo vilivyokuwa na kadi za TANU na karatasi zake za risiti.

Kila mtu alipoingia alipewa kadi na risiti isiyoandikwa.
Kisha akaambiwa aifikiche kadi na hiyo risiti pasipo kuichana.

Na asiongee chochote hadi afike lango la nyuma ambalo ni la kutokea.

Hapo palikuwepo watu wamejipanga katika meza. Walipofika hapo walimpa huyo aliyekuwepo katika meza hiyo kadi na risiti kisha kumtajia majina yake, anakoishi nk.

Yule karani aliiiandika ile kadi na risiti kwa tarehe za miezi ya nyuma, meza nyingine ilipiga muhuri.

Mwisho mwenye kadi aliambiwa kuwamba ameisha kuwa mwanachama wa TANU wa muda mrefu.

Akiulizwa atoe kadi na aitetee TANU pasipo kumtaja Mwami wala kilichotokea usiku ule; kwake hicho ni kiapo cha utiifu kwa Mwami.

Aliruhusiwa na kusisitizwa kuitunza hiyo kadi na risiti yake.
Mwami Theresa alitufahamisha kuwa zoezi lile lilikamilika mnamo saa tisa za usiku.

Meza zikaondolewa na wafanyakazi wakatawanyika na kwenda kulala.

Ilipofika alfajiri karibu ya saa kumi na mbili za asubuhi, nikaambiwa kuna msafara wa magari ya polisi unaelekea kwenye makazi yangu.

Niliyategemea hayo, maana vibaraka wapelelezi walikuwepo enzi hizo.
Hata hivyo, kwa tukio lile walikuwa wameshachelewa.

Mimi siku ile sikuwa nimelala wala kupata usingizi.
Nilikuwa katika nguo zangu za kawaida.

Nilipoletewa taarifa ile, nikaingia chumbani na kuwaambia walinzi wangu kuwa wakifika, kwanza kuweni imara kuhusu siri ya kilichotokea usiku.

Pili waambieni kuwa Mwami hajamka. Ngoja tukamwamshe. Kisha mje kunigongea.

Na kwamba nitakapotoka na kufokeana nao, nyiye onesheni utiifu kwangu na kuwakasirikia wao; wala msioneshe kuwahofu. Mkakati huo ukaeleweka.

Mwami Theresa akatueleza kuwa wakaingia maofisa wa polisi akiwemo mmoja Mzungu na DC (District Commissioner) Mzungu pia.

Wakauliza kama Mwami yupo.
Wakaambiwa amelala, na kwamba wanaenda kumuamsha.

Walinzi wa Mwami wakaenda kugonga mlango wake.
Baada ya muda akaitikia na kuuliza kwa sauti ya juu, “Kuna nini mnanigongea usiku huu?”

Wakamjibu, “Kuna Bwana DC na mkubwa wa polisi.”
Mwami akajibu kwa sauti kali, “Wanataka nini wakati hakujakucha ngoja nije.”

Akatuambia kuwa alijiandaa kwa kuvaa “night dress” akatimua nywele zake kisha akajiviringisha shuka na blanketi akatoka akiwa ameshikilia na alipofika sebuleni na kuwaona hakuwa salimia wala kusubiri salam zao.

Alianza kwa kuwafokea kwa lugha ya Kiingereza:

“How dare you wake me up at this time of the hour?
Can you do this to the Queen of the UK?

Don’t you know I am the the Queen of Buha?
Is it because I’m an African that’s why you are doing this to me?

I will file my complaints and report you to the Governor for this.”

Mwami akatuhadithia kuwa wale maofisa wa kikoloni walichanganyikiwa na kuanza kujitetea kuwa walipata taarifa kwamba alikuwa akigawa kadi za TANU usiku.

Akawajibu, “Je, mmekuja na ‘’Search Warrant?”

Kisha akaongeza kwa kuwaambia, “Nyiye askari wanaume watupu pamoja na DC mmekuja kunipekua mimi mwanamke?

Nitamlalamikia Gavana.''
Hawakuwa na ‘’Search Warrant.’’

Mwami akawageukia walinzi wake na kuwataka wawaambie wale DC na mapolisi wake watoke mara moja au wapige baragumu kuashiria Mwami amevamiwa ili waje wamhami.

Yule DC na watu wake waliomba radhi haraka na kuondoka."


1653540913428.png
1653541046821.png
 

Attachments

  • 1653540998314.png
    1653540998314.png
    130.3 KB · Views: 25
Sio chai iliyokolea tangawizi kweli! Unaiweza kumfokea mkuu wa wilaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
Joseph...
Umepata kumsikia Schneider Abdillahi Plantan katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Alikuwa mtu shujaa aliyepambana na Waingereza kwa silaha akiwa askari katika jeshi la Wajerumani WWI.

Akapambana na Waingereza WWII kwa maneno wakamkamata na kumweka kizuizini.

Akapambana na Waingereza uso kwa macho 1950 akipigania kuutoa uongozi wa TAA wa Wazee kana yeye uliokuwa madarakani ili awaingize vijana Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes wa kudai uhuru wa Tanganyika.

Schneider Plantan baada ya uhuru akapambana na Julius Nyerere nyumbani kwa Nyerere kwa maneno makali sana baada ya kutolewa kizuizini alikowekwa na serikali.

Schneider Abdillahi Plantan alikuwa Secretary wa Daawat Islamiyya iliyokuwa ikiongozwa na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.

Unapokutana na mambo kama haya tafuta lugha ya kistaarabu kutaka kujua ukweli.

Kuna watu hawakuwa wanawaogopa Wazungu.

Tafuta hotuba ya Suleiman Mamba kwa Wajerumani kabla hajanyongwa kwa kunyanyanyua silaha dhdi yao baada ya Vita Vya Maji Maji.
1653595023336.jpeg


Kufoka na kunyanyanyua silaha na kutangaza vita uuwe au uuliwe lipi kubwa zaidi?
1653595022941.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom