Mwami Theresa Ntare (1922 - 1999)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,924
30,273
SIKU YA MWANAMKE DUNIANI 8 MARCH 2024

''Serikali ya kikoloni haikutaka sisi machifu tuwe katika siasa hasa kuisaidia TANU.

Hata hivyo tukiwa wananchi na viongozi wa wanchi wanaotaabika chini ya utawala wa kikoloni, tuliiamua kushiriki siasa kwa siri na kuipa nguvu TANU ili tujitawale. Kuna wakati taarifa zilinifikia kwamba ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulikuwa unakuja kusikiliza maoni ya kudai uhuru.

Utaratibu wa kikoloni ni kuwa chama japo ni cha kitaifa, kilitakiwa kipate pia usajili katika kila jimbo. Hivyo TANU ikidai kuwa inawakilisha wananchi wote, watawala wa mikoa walikuwa wakijiandaa kukisuta kuwa si kweli na kuonesha sehemu ambako hakikuwa na wanachama.

Moja ya sehemu hizo wakoloni waligundua ni katika himaya ya utawala wangu wa Buha.

Waligundua TANU haipo kwa Waha. Taarifa za siri zikanifika kwa wakoloni wataiambia tume hiyo ya UNO juu ya hilo. Nikaamua kuchukua hatua kwa siri na kwa haraka.''
(Mwami Theresa Ntare)



View: https://youtu.be/ayCWG_5UtCQ?si=NVgeGF2WkkufA37D
 
Back
Top Bottom