Mwambieni January Makamba kwamba umeme umeanza kukatika ovyo Dar es Salaam

Jamaa sijui kala maharage ya wapi
 
Matatizo ya umeme tulianza kuyasahau! Automatically watu wameanza kununua generators kujihami shughuli zao! Sometimes naelewa kwanini JPM kuna watu aliwashughulikia bila huruma.
Ukiwa mfanyabiashara au na Nyumba kuwa na standby Generator ni kawaida sana!!...
 
Umeme umekatika toka asubuhi hadi mda huu, zaidi ya masaa sita hakuna umeme...na ni maeneo mengi hapa mjini. Acha upumbavu!
 
Hapa ndio umakini wa JPM unakuja, huu upumbavu haukuwahi kuwepo, binafsi nilisahau kabisa hizi mambo za kukatika kwa umeme ovyo kiasi hiki.

JM ameweka mabeste zake, mama nae yupo tu sasa tutegemee majenereta kufanya kazi yake. Watu wa pwani kuna wakati wanakuwa wa hovyo hovyo tu, hivi JM nae si mtu wa pwani tu, hapo bumbuli si pwani tu..
 
Mgao umerudi tena? Maana si kwa kukatika huku kwa umeme. Kuna shida gani?
 
Mpigie simu au muandikie barua
 
Acha tuuze majenereta mkuu
 
1. Unapotoa mfano uwe halisi, 2015 umeme ulikuwa imara chini ya mwamba Muhongo.
2. Umeme utakatika sana, lengo kumhujuma Makamba.
3. Lazima wamkaribishe kwa kukata umeme, nchi hii ina wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…