Maeneo ya Dar es Salaam kukosa umeme Oktoba 24 & 25, 2022, TANESCO yasema kuna maboresho ya mitambo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kukosekana kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kutokana na uwepo wa matengenezo kadhaa, leo Jumatatu Oktoba 24, 2022 kuanzia saa moja asubuhi hadi saa nane mchana.

Matengenezo yanayofanyika katika mtambo namba mbili wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Songas uliopata hitilafu.

Taarifa ya TANESCO imeeleza kuwa iwapo matengenezo kwenye mtambo huo yatachelewa kufanyika kunaweza kutokea madhara makubwa kwenye mtambo husika.

Aidha, Shirika limesema matengenezo mengine yanatarajiwa kufanyika katika njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa Kilovoti 220 kutoka Ubungo hadi Kinyerezi, Jumanne, Oktoba 25, 2022 kuanzia saa 11 Alfajiri hadi Saa 5 Asubuhi.

Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam yataathirika kwa kukosa umeme pia.

“Wateja wa maeneo yote yatakayoathirika watatumiwa SMS kwenye simu zao,” imeeleza taaarifa ya TANESCO.

Tanesco.jpg


Tanesco 2.jpg
 
Leo mnamo majira ya saa 11/40 alfajiri umeme umakatika maeneo mengiya TBT sijui maeneo mengine,
naona sasa imekua rasmi ,ila haya hatukuyaona enzi za mwamba yule. hatukatai matengenezo ila sasa too much.huko uswazi tunategemema sana huu umeme kama siku nzima hufanyi kazi unategemea nini?
 
Wale mbwa wanaobweka "mama anaupiga mwingi" nasikia mgao wa maji na umeme hauwahusu. K_mamae zao.
 
Back
Top Bottom