Tatizo la kukatika Umeme ni Dar es Salaam yote au?

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,924
3,904
Wadau hivi hii katikakatika ya umeme inayoendelea ni huku kwetu tu au ni jiji zima la Dar? Huku maeneo ya kawe, mbezi beach, tegeta tunateseka sana. Naamini na maeneo mengine hali ni hiyo hiyo. Kwa muda wa karibu mwezi mmoja kumekua na hii shida kwa kiasi kikubwa sana.

Nakumbuka kipindi cha Waziri Kalemani tatizo la kukatika umeme lilipungua kwa kiasi kikubwa sana. Isije ikawa baadhi ya watumishi TANESCO wanataka kumkwamisha Waziri mpya wa Nishati Mh Makamba.
 
Nashukuru Mungu tangu mgao uanze sisi ulitukumba tu siku moja ya juzi lakini siku zingine umeme upo muda wote
 
Wadau hivi hii katikakatika ya umeme inayoendelea ni huku kwetu tu au ni jiji zima la Dar? Huku maeneo ya kawe, mbezi beach, tegeta tunateseka sana. Naamini na maeneo mengine hali ni hiyo hiyo. Kwa muda wa karibu mwezi mmoja kumekua na hii shida kwa kiasi kikibwa sana.

Nakumbuka kipindi cha Waziri Kalemani tatizo la kukatika umeme lilipungua kwa kiasi kikubwa sana. Isije ikawa baadhi ya watumishi TANESCO wanataka kumkwamisha Waziri mpya wa Nishati Mh Makamba.
Anakwamishwa? Kwa jitihada gani anayofanya?....kwa taarifa yako pambana na hali yako
 
Just imagine katika karne hii ya 21 ambapo kila kitu kinategemea umeme katika nyanja mbalimbali za kiuchumi halfu unakuta katika jiji kubwa linalotegemewa na nchi kiuchumi na nchi yenyewe ina kila aina ya rasilimali za kuzalisha huo umeme na kusambaza unakuta umeme unakatikakatika kila mara kila siku na ni jambo la kawaida tu , then tukiambiwa we are in shithole countries people are going mad...!!?
 
Log! Hizi nchi za Ndabaningi tabu sana.
 
Wadau hivi hii katikakatika ya umeme inayoendelea ni huku kwetu tu au ni jiji zima la Dar? Huku maeneo ya kawe, mbezi beach, tegeta tunateseka sana. Naamini na maeneo mengine hali ni hiyo hiyo. Kwa muda wa karibu mwezi mmoja kumekua na hii shida kwa kiasi kikubwa sana.

Nakumbuka kipindi cha Waziri Kalemani tatizo la kukatika umeme lilipungua kwa kiasi kikubwa sana. Isije ikawa baadhi ya watumishi TANESCO wanataka kumkwamisha Waziri mpya wa Nishati Mh Makamba.
Tatizo hili siyo Dar na viunga vyake pekee, ni la nchi nzima.

Hilo la kusema staff wa Tanesco kumharibia Makamba nalikataa!

Adha kama hii ya kitaifa ukiona waziri hana 'say' elewa kuwa anahusika moja kwa moja na kadhia hiyo.

Wengine hapa sisi ni wasema hovyo hatutaki kusema sana, ila jambo hili lina mnyororo mrefu tena ni wa kimkakati.

Kuanzia kufukuzwa waziri Kalemani na kisha baada ya kukabidhi ofisi tu, umeme ukaanza kukatwa, kuvuta umeme kwa wahitaji waliolipia ni shida, visingizio ni nguzo na vijisababu vingi vidogo vidogo vya kukera!

Matendo haya yote yanatufikirisha sana sisi raia tuliokuwa tumeanza kuona mwangaza wa maendeleo nchini Tz ukitokeza kwa kasi na sasa unafifishwa kwa nguvu kubwa.

Ngojea tuone tunakopelekwa!
 
Back
Top Bottom