MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

inategemea singida ipi kaka lakin panamahali pazuri sana tu. unafundisha masomo gan nkupgie kampeni uende mahali pana maji ya kutusho na hakuna ukame kama wanavyokuaminisha.
 
karibu sana ni wilaya iliyobarikiwa kwa kilimo cha mpunga,viazi na kila kitu kiufupi shule nyingi zipo main road ya East Africa yaani kiufupi kufika mjini ni dk chache tu ..ina centres nyingi zilizochangamka sana haya una swali gani wewe na wenzio?
 
Kuna mashamba ya umwagiliaji vitunguu IGOMELO. Jihusishe na kilimo kuongeza kipato.
 
Angalia tangazo la tigo la joti utapajua kyela..jiandae kulogwa kama huna hiriZi
 
Mh kuna wachawi uko balaa tangu nitoke huko kuja dar du hata nikienda huwa ni kwa machale sana mara ya mwisho mwaka 2012 ndo nilienda kuwasabahi wazee babu na bibi, hata hivo hutakiwi kuogopa unatakiwa kujaribu kutotofautiana nao sana ili uwe na amani
 
Kwa walimu ajira mpya aluyepangiwa Msalala dc hasa kwa wale wa secondary uliza hapa upate muongozo usijeenda pangiwa chaka..
 
Umeme utoke wapi kutoka msoma mjini umeishia mgango na lami imeishia kilo meta kama tano tu kutoka mjini
 
But ukilinganisha na maeneo mengine walau ndo kasehemu/ kacenter ambako kapo bomba kisela
 
Kuna mademu sanaaa yaaani huhitaji kutongoza we nunuq baiskeli yako umemaliza utapapatua mpaka uchoke
 
duuuh..sikutishi kiongozi ila omba sana dua mkuu... maeneo mengi ya singida vijijini ni magumu..pakame..maji shida..raia watata watata...
ILA NIJUSHAURI KITU WAHI KURIPOTI MAPEMA KAWE MJANJAMJANJA WAKUPANGIE KARIBU NA TOWN KIDOGO AU KWENYE HUDUMA ...
***kuhusu fursa kule kuna kilimo cha alizeti kinatoa sana
**biashara ya mifugo..hapa namaanisha kuku ..biashara inakuhakikishia faida
**au uje kuchukua bidhaa town ukauze mnadani huko.. bidhaa kama mitumba..yeboyebo..masweta.. mitandio na madera ..
plus...jichanganye na wenyeji na uwe social ..USIJITIE UJUAJI AS I'VE ALREADY SAID RAIA WATATA
 
Mimi pia nimefika Tunduru mara kadhaa na mara ya mwisho ilikuwa ni february mwaka huu. Umeme upo! Zamani ni kweli ilikuwa ni generator lakini siku hizi walishaunganishwa na umeme wa Gesi toka Mtwara. Umeme na maji ya kumwaga. Hiyo karabai mtumie bibi kijijini atashukuru

Ahsante mkuu
 
Back
Top Bottom