Natumaini mu-wenye afya njema. Poleni na mapambano ya kila siku. Ni mara yangu ya kwanza kuandika katika jukwaa hili hasa baada ya kuwa nasoma maandiko mengi tu ya wadau mbalimbali yanayohusu mambo mengi katika jamii zetu.
Ni jukwaa pendwa pia kuwazungumzia watanzania wenzetu ambao wanashindwa kupaza sauti pale wanapokuwa wanapitia masahibu katika maeneo yao ya kazi.
Kuna shule ipo Mkuranga, umbali tu kidogo kutoka Kongowe Mbagala, inaitwa St. Matthew's. Ni shule ya sekondari japo pia wana msingi. Shule hii ni shule dada na St. Mark's- Mbagala, Ujenzi sec.-Vikindu na Imagevosa-iringa.
Ni shule kubwa yenye wastani wa wanafunzi 680-700 kwa kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwa muda sasa mrefu sasa, walimu wanahangaika kwa kutokulipwa mishahara. Ndugu yangu wa karibu anaefanya kazi pale ameniambia "kwa ushahidi" kwamba ni zaidi ya miezi saba na hajalipwa mahahara wake.
Kila anaesimama kuhoji mshahara wake anaondolewa kazi bila hata notice. Walimu wanaishi kwa shida sana. Wamewahi kuchukua hatua na kuripoti katika halmashauri ya mkuranga. Waliobanika kufikisha taarifa hizo walifukuzwa kazi na tena bila kulipwa stahiki zao na bado halmashauri ya mkuranga haikushughulika na suala hilo. Mwezi huu wa tisa baada ya likizo fupi kuisha, kuna walimu wengine wanne wameondoshwa.
Sababu ni kwamba watoto wapatao asilimia kumi katika masomo yao hawajafikisha wastani. Lakini hawa ni walimu wapya, wameajiliwa miezi mitatu tu iliyopita kabla ya kufanya mitihani ya midterm. Wanawazungusha kuwalipa stahiki zao.. Uongozi unawazungusha kuwalipa stahiki zao hasa baada ya kuachishwa kazi.
Naziomba mamlaka zinazohusika, kufuatilia suala hili hasa kwa kuzingatia kwamba vijana wengi wanaofanya kazi katika taasisi za binafsi wana malengo wanataka kuyafikia pia. Tukemee vitendo vya unyanyasaji katika sehemu za kazi.
Ikiwa kuna mtu yeyote mwenye details za wapi pa kuanzia ili kuwasaidia kwa ngazi za kiserikali tafadhali toa maoni.
Asanteni sana.