Mwalimu Nyerere na ukabila

Mkuu usiye na matatizo ya kuelewa, nimekubaliana na wewe kuwa ANGEWEKA KUANZISHA TV KWENYE VIPAUMBELE VYAKE ILI WABONGO TUFAIDI, hutaki tena??? Halafu punguza hasira ili uone vizuri, hakuna mahali nimesema kajenga reli ya kati... Mimi ni mmoja wa watu ambao hawaungi mkono hiyo 'mila' ya mwenge, pia sitegemei kwamba nipendezwe na misimamo yake %100, lkn hiyo hainifanyi nimuone mwenye mawazo finyu .
 
 
Last edited by a moderator:
wewe ni mwongo mkubwa, kwanza toka lini mtu akalazimishwa kupendwa na watu wakampenda? haina mantiki kabisa, ila walikuwepo wasiompenda kwa sababu zao binafsi au kwa kutofautiana mitazamo na walikuwa wachache na uache uongo wako kusema walikuwa wengi, nadhani ulishuhudia kipindi cha kung'atuka kwake jinsi watu wengi walivyomuaga kwa zawadi mbalimbali, je walilazimishwa? na vipi alipofariki uliona umati wa watu waliojawa na majonzi? taifa lilizizima, je walilazimishwa? acha hizo ndugu yangu hicho ni kisokolokwinyo chako tu! halafu una uhakika hao waliotaka kumpindua ndo waliokuwa wanapendwa na wengi au ni tamaa zao za madaraka!?
 
sijakutukana babu najaribu kukuelewesha...the realities most of us we are fully of incorrect facts

Unapozungumzia historia ya nchi hii kila mmoja anaitazama kutokea katika "angle" tofauti na mwenzake, ndio maana tunajadili ili tufike mahali tukubaliane kukubaliana ama tukubaliane kutokubaliana.

Sasa ndugu yangu unajua hapa tunajaribu kueleweshana na vilevile kubadilishana uzoefu wa historia ya nchi yetu, sioni mantiki ya kutumia maneno ya dharau wakati tumekuwa tukijadiliana kiungwana tangu mwanzo.
 

I wouldn't be surprised if u have never seen the speech. I can feel how light u are and if u are a Manchurian candidate, there is nothing i can do 2 help. About Mobutu's visit to USA, that is a rhetorical question, as well as Idd Amin. Who put Mobutu in power? Who killed P.Lumumba?
 
acha hasira babu neno uduanzi siyo baya namna hiyoo niite mie basi...
 
Mwalimu Nyerere kama kiongozi alikuwa na mazuri pamoja na mapungufu, ni kweli alipendwa na watu wengi kwa sababu mbali mbali,hivyo hivyo alichukiwa na watu kwa sababu mbali mbali.Kama kiongozi alikuwa mstari wa mbele wakati wa mapambano ya uhuru wa nchi kusini mwa afrika,na wakati huo huo anataka kujenga ujamaa,vile vile vita vya Kagera,Alijikuta njia panda baada wafadhiri wa IMF,World Bank wakamtema kwa kutofautiana nae.
 

for the records hiyo hotuba ya nyerere south africa
imeonyeshwa sana na tbc1
nimeiona mara nyingi sana...

tatizo lako unaitazama south afrika kama nchi muhimu sana kwa
kum validate mtu...
sijui umefuatilia jacob zuma anavyojaribu kumuokoa gadafi na anashindwa????????
 
Naona unajitahidi kujinasibisha na geza ulole kwa kasi sana.

Rudi kule ukatetee utumbo wako, achana na geza ulole tunakwenda naye vizuri ili kufahamisha na kubadilishana uzoefu na uelewa sio wewe kila saa kurukia ncha ya mkuki wa geza ulole!!

una tatizo kubwa sana
kuthibitisha nyerere alikuwa mkabila hukuti mtu mwenye jina
la mwita akimpinga nyerere

soma vizuri mwanzo wa thread
alieanzisha topic ya vyama vya ushirika hapa ni mimi
gezaulole alikuja kuongezea data
sasa usijiabishe kwa kuropoka ropoka
 
Mwita Maranya said:
Tukumbuke kwamba shule hizi tunazozitaja zimejengwa na wakoloni hata kama tutawaita wamishenari, lengo alo kubwa lilikuwa ni moja tu, kutafuta mbinu bora ya kututawala na kwa msaada wa sisi wenyewe weusi.

Mwita Maranya,

..kuna maeneo Wamishionari walifundisha useremala, ufundi uashi, etc etc. pia yapo maeneo walianzisha zahanati.

..pia yapo maeneo ambayo wazazi walishiriki ktk ujenzi wa shule za misioni haswa za msingi.

..binafsi siyaelewi-elewi haya madai kwamba Wamishionari walitoa elimu ili Watanganyika watawalike kwa urahisi. nasema hivyo kwa kuzingatia kwamba yapo maeneo walikuwa wanatoa elimu ya nadharia na vitendo kama kufundisha useremala, etc etc.
 
Sweke,
Nyerere hakuwa na runinga ikulu. Siku hizo hata ungekuwa na tv ungekuwa unatizama nini? TV Zanzibar? Ila mwaka 1977 baada ya ziara yake rasmi Marekani kuzungumzia harakati za ukombozi Rhodesia, Mzee Bomani alimnunulia video player pamoja na TV yake ili aweze kuona video mbalimbali ambazo ubalozi wa Tanzania Washington DC uliweza kumtumia. Nadhani hiyo ndiyo imepelekea watu kusema Nyerere alikuwa na tv ikulu. Ilikuwa ni TV ya kuangalia video. That is a fact.
 
Reactions: 911
Your might have a point but I don't think this is Mwl Nyerere we know for all these years. Ndio mwalimu sio mtu sahii na kuna vitu vingi vya kumkosoa lakini katika kuishi kwake na maisha yake yalionyesha wazi kwamba yeye sio mkabila. This issue unayoizungumzia hapa really it's not relevant katika maisha yetu ya Watanzania kwa sasa. Why I am saying this, Tanzania sasa kila Mtanzania anayetoka kabila lolote lile anayonafasi ya ku-archive anything they want na opportunities are there. Tatizo lilipo sio maneno ya Nyerere ila ni ccm iliopo ambayo tunaona uozo, wizi, violations za human rights tunazoziona, kikwete na majangiri wenzio ndio wanaharibu Taifa sasa. Yes some of it Nyerere is to blame, Mtanzania yeyote anayehamu politics tunajua wazi kwamba political figure kama Nyerere alikuwa na opportunity kubwa ya kuweka foundation ya true democracy na kwa hili he did come short. Nyerere ange-focus kwenye constitution inayolenga true democratic society and not favouring ccm only, tunajua Nyerere alikuwa na influence kubwa katika kutengeneza hii constitution but he didn't. Tunaona matokeo yake ccm na kikwete wanatumia hii hii constitution to oppress Wananchi na oppositions. In short, Nyerere did a lot for Tanzania and he was largely good political figure but he has many many short comings. Thats Nyerere for you, yes he is human and he had at least leadership integrity compare to Mwinyi, Mkapa and huyu fisadi kikwete.

'One thing to remember Nyerere's short falls can be summarized this way, he did want to protect his legacy and he though ccm will continue and flourish and not deminizing Tanzania this way'


 
Hapo pia umeteleza. Katika njama za mapinduzi za mwaka 1970 alikuwemo mwanajeshi Marwa aliyehusishwa na njama hizo. Jaribu kingine.
 
hakuna kitu kama hicho aliweka Wakurya kumlinda madarakani ukiangalia vizuri kabola Wazanaki ni la kufikirika yaani ni sehemu ya Wakurya!
Geza Ulole,
Hapana. Wazanaki si sehemu ya Wakurya. Wazanaki walitoka Rwanda/ Burundi wakati Wakurya inasemekana wametokea Ethiopia. Lakini hii ya kuwa na Wakurya wengi jeshini na Wanyakyusa haikutengenezwa na Mwalimu. Ilianzia enzi za KAR.
 
ina maana unataka kusema ikulu nzima haikuwa na Dish kuangalia newz kama BBC? siamini! alikuwa anapata wapi habari za nje?
 
well nakuelewa sasa baada ya kuyapinga, then kwanini aliua vyama vyao vya ushirika through nationalization ambavyo ni jasho lao yaani KNCU na KCU?
Geza Ulole,
Katika interview moja na jarida The Internationalist, Mwalimu alikiri kuwa lilikuwa kosa kuua vyama vya ushirika. He admitted to the mistake.
 
Mkuu joka kuu, ngoja namimi niulize hivi serikali ya kikoloni iliyokuwepo ukianza na ya wajerumani halafu waingereza ilijenga shule zipi?
 
Geza Ulole,
Hapana. Wazanaki si sehemu ya Wakurya. Wazanaki walitoka Rwanda/ Burundi wakati Wakurya inasemekana wametokea Ethiopia. Lakini hii ya kuwa na Wakurya wengi jeshini na Wanyakyusa haikutengenezwa na Mwalimu. Ilianzia enzi za KAR.
kuna kitu kinaitwa kinship ni sawa leo hii Mbowe awe Rais halafu jeshini ajaze Wameru, Waarusha na Wamasai halafu aseme hatushaabiani au si jamaa! still utaona kuna sort of nepotism maana hizi jamii ziko karibu zaidi kuanzia kimila hata tamaduni! nathani unapata gist ya nilichomaanisha! Mbona asijaze Wanzanzibari jeshini?
 
Anko Sam,
Bomani alioa Uchagani hata kabla ya uhuru. That is a fact.
 
Hee babu lile, waislaam kawanyanyasa sana, kumbe hata makabila mengine alikuwa anayanyanyasa? ndio maana ile hotuba yake moja anawasannif wakara? mungu amuweke anapostahili.
Na wewe umefunguliwa lini? Nitakata rufaa kwa mods urejeshwe lupango!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…