Mwalimu Nyerere na ukabila

na asisahau vitabi hivi pia

the dark side of jk nyerere
life and times of abdulwahid sykes

sikumbuki waandishi
Ninavyo vyote. Cha Dark side kimeandikwa na Ludovick Mwijage na cha Abdulwahid kimeandikwa na Mohammed Said.
 
Mkuu Bukuku, nakubaliana nawewe kabisa kuwa mwalimu kama binadamu alikuwa na mapungufu yake. Katika moja ya hotuba zake za mwisho alisema, 'mchukue yale mazuri yetu na muache yale mabaya'. Amekiiri hadharani kwa kinywa chake. Mimi mara zote nimekuwa nikiyasema yale ambayo sikuridhika na utendaji au utekelezwaji wake.

Tatizo linakuja pale kunapokuwepo na chuki, ima ya kuzaliwa au ya kujifunza dhidi ya Nyerere. Fikiria mtu anaposema Nyerere alikuwa mkabila, hiyo ni sawa kwa maoni yake, lakini aende mbali nakututhibitishia kuwa alikuwa mkabila kwa ABCD.

Mtu anaposema alikuwa mdini, fair! lakini athibitishe bila shaka udini wa Nyerere. Tena hili la udini hata mwandishi Mohamed Said tumejadiliana naye mwezi mzima hapa JF hakuweza kuthibitisha kisomi udini wa Nyerere zaidi ya hisia na hadithi za kusikia. Sasa limejirudia ndio maana tunauliza na si kutetea historia ya Nyerere; 1) Tuthibitishiwe ukabila wake. Hadi sasa hakuna aliyethibitisha.
2) Tuthibitishiwe udini wake, hakuna aliyejitokeza n.k.

Hii maana yake ni nini! tutaambiwa siku moja Nyerere alikuwa Mchina, tunakubali. Siku nyingine alikuwa mdogo wake Dikteta Ngweso, tunakubali. Mama yake alizaliwa ukoo wa Hitler, tunakubali. Yote haya yatajumuishwa na mwendesha mashitaka ili aorodhesha makosa 100 ya Nyerere na kutaka hakimu atoe hukumu bila ya uthibitisho. Hapa ndipo wengine tunasema hapana, tuna akili zetu, tumeishi nyakati za mwlm tunamjua tupeni uthibitisho. Kabla ya hukumu tuthibitishiwe madai dhidi yake.
Kwa vile mara nyingi huwa hawana uthibitisho ya mabaya yake basi sisi tuna uthibitisho wa mema yake ndio linapokuja suala kutaja mazuri yake.

Bukuku inapotokea mtu akasema Nyerere alikuwa mbaya sana kwasababu alikataa kuleta TV, hivi kuna njia gani rahisi ya kumsaidia mtu huyu kama si kumweleza uzuri wa mambo mengi aliyoyafanya kuliko TV.
Siwezi kusema tu hapana ulikuwa uamuzi mzuri kutokuwa na TV nakaishia hapo, nitakuwa nimetumbukia katika mtego wa kudhani bila ushahidi, nitaeleza kwanini TV haikuwa muhimu kuliko elimu na afya na hapa ndipo nalazimika kutaja mema ya Nyerere.

Tufanye hivi: Maswali ni mengi hebu tuanze na haya mawili kwanza, tuelezwe ukabila na udini wa Nyerere.
Mkuu Bukuku fungua pazia ili wenye hoja wakuunge mkono nasi tuelimike.Hakuna sababu ya kutaja mazuri tuanze na haya mawaili tu. Ukabila na Udini wa Nyerere kwa vithibitisho!
 
Mtemi,
Nadhani swali lako unaweza kupata majibu katika kitabu cha Godfrey Mwakikagile. Amegusia attempts zote.
 
Nakumbuka mwl ktk hotuba zake alikuwa very open.........kuhusu kuchagua kiongozi alisisitiza sana yafuatayo na kwa uchungu mkubwa.........alisema"...hatutachagua mtu kwa sababu ya dini yake, hatutachagua mtu kwa sababu ya kabila lake na wala hatutachagua mtu kwa sbabu ya mkoa/sehemu atokako.................tunataka mtu mwenye sifa za kuwa kiongozi yaani mtu anayeyajua matatizo ya watz na yuko tayari kuwatumikia.......ndiyo maana alikuwa hataki watu km akina kikwete na lowasa kwani alijua ni wasanii tu wa mtaani ambao hawawezi kutembea ktk kile wasemacho.......................hakutaka sentensi za kwamba kwa kuwa mhula huu rais katoka bara basi ujao atoke visiwani, kwa kuwa rais katoka kaskazini basi huu atoke mashariki..................jamani yule mzee alikuwa na vision za ajabu sana km angeungwa mkono tungefika mbali sana ndiyo maana wenye akili timamu wanatamani azimio la arusha lirudishwe na liwekwe kwenye katiba mpya ya watz
 
Wacha, ulikuwa wapi?
Ni kama vile tumekuwa tunarusha makombora kutoka kwenye handaki bila kujua kuwa kuna mwenzetu anakuja kutupa ahueni.
It is good to see you here man, and now I can take a break!


Jasusi

Vipi mkongwe naona hawa kuku wanaleta shida ile misukule imevimbiwa lakini bado inataka kula, wakati wake wa kupasuka matumbo umekaribia.
Hivi hawa kuku aliowaswaga huku ni nani kama sio M k w e r e kwa ushirikiano wake na vifisadi dagaa. Hata aibu halina kibabu kizima akili zake hovyo.
 
Reactions: BAK
Atleast kuna watu mnajaribu kumtetea jk Nyerere na kumake sense katika maelezo yenu. Ngoja nijipe muda zaidi wa kumsoma huyu JK nyerere anayesema amesaidiana kufight uhuru na wazee ila wengi naona wameishia vifo visivyo na majibu mpaka leo. THE DARK SIDE OF NYERERE AND MAISHA SYKES by Mohamedi Saidi vinanipa mwanga kiasi kumfahamu.
 
Ahsate sana Mkuu, nimeupenda mno huu mchango wako.

 
Ahsate sana Mkuu, nimeupenda mno huu mchango wako.


Mkuu za masiku? Naona Internationals karibu zinaisha, Rafa nilitazama mechi zake kule China naona kawashitukia media na aliamua kupumnzika kidogo, hopefully atapumnzika vizuri na baadaye kutinga O2 kwenye funga mwaka. The boy is good. Have a nice day na shukrani za dhati kwa michango yako hapa JF.
 
Reactions: BAK
Nashukuru sana Mkuu nami pia nakupa shukrani za dhati kwa michango yako hapa jamvini kwetu. Mtu wetu Rafa naona labda kachoka lakini kweli performance yake kuanzia spring hadi sasa sikutegemea iwe nzuri kiasi kile hasa ukitilia maanani kwamba alikuwa kaumia na hakucheza kwa kipindi kirefu ili kujitibia goti lake, nahisi kateleza tu baada ya mapumziko mafupi ataendelea kufanya vitu vyake katika mashindano ya kufungia mwaka kabla ya kutinga Australia January, 2014.

 
Hivi nyie mliwai kuangalia tv ya zanzibar. hapakuwaga na kitu isipokuwa jamaa aliyekua anapuliza tarumeta flani hivi zakienyeji. hangalau kilimanjaro milimani KBC ilikuwa na kitu chakuangalia.
 
UKweli ni kwamba Nairobi ni mji wa wamaasai, hata neno Nairobi ni la kimasai. Tatizo, upendeleo uliwafanya wakikuyu kuutawala. Upendeleo ukaongezwa na Kenyatta.
 
Siasa za misikitini zimekupofusha kabisa akili.
 
Hahahah
 
Mpaka sasa mwalimu ndiye aliyefanya makabila mengine wawachukie wahaya kupitiliza. Mwalimu alipandikiza mbegu mbaya kwa watanzania kwamba wahaya wanabaguana, wana ukabila kuliko makabila mengine kitu ambacho sio kweli.

Wahaya ni watu wapole, wasafi, wanyenyekevu na wenye busara sana. Kitu pekee ambacho wahaya hawakipendi ni kudharauliwa, yaani hata uwe na pesa, nyumba, magari n.k yeye kwake anaona ni kitu cha kawaida hatishiki wala kubabaika. Utakuta hajajenga, ila akija kwako hata uwe umejenga kiasi gani, yeye atasema ni kanyumba.

Wahaya ndiyo kabila linalochukiwa Tanzania kuliko yote. Wengi hupenda kumuona Muhaya akiteseka au hata akianguka zaidi, hapo ndipo furaha yao hutimia vizuri. Lakini hii chuki haikuja bure, mwalimu ndiye chanzo aliiharibu image ya wahaya kwa watanzania kwa kuwaita wabaguzi na wakabila, propaganda hii inaenea na kusambaa hadi leo. Inawezekana alifanya hivyo kwa itikadi zake za kisiasa na utawala kwa kuwaogopa wahaya.

Wahaya ni wamoja, wana hadi vyama vya koo zao ili kuhamasisha umoja na mshikamano, wanaishi kijamaa zaidi, sasa sijui huko kubaguana alikokueneza mwalimu alikutoa wapi.

Namchukia sana mwalimu, kila nionapo picha yake, hasira unipanda misri ya cobra. Kwanza ndiye chanzo cha umasikini wa Tanzania kutokana na sera zake mbovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…