Mwalimu Nyerere na ukabila


Zomba Nyerere alikuwa akipendwa na watu wengi. Nadhani ulishuhudia mazishi yake. Kama hakupendwa na hao unaowasema basoi hao ni wachache tu. Hata kama ni waislamu sio wengi ni wachache kaka. huwezi kusema kwa kuwa aliwafunga baadhi ya mashehe na kumchapa viboko Alhaji Fundikira basi akina Rashidi Kawawa, Salim Ahmed Salim n.k hawakumpenda.
 
Geza Ulole,
I beg to differ. Mwalimu alianza ku "toy" na wazo la ujamaa, au usawa wa binadamu alipokuwa Makerere.Ukisoma makala alizoanzika enzi hizo alikuwa anazungumzia hilo, usawa wa binadamu, na jamii ya kijamaa katika jumuiya ya Waafrika. Kisomo chake Uingereza, hasa pale alipochukua somo la falsafa, kikamwongezea hamasa ya ku 'explore" zaidi ujamaa au socialism. Ngoja nikuchekeshe. Katiba ya KANU, Kenya, ilikuwa inaitisha kujengwa kwa taifa la kijamaa. Katiba ya ANC, Afrika kusini, vivyo hivyo. Kwa hiyo utaona miongoni mwa viongozi ambao walipambana na udhalimu wa kikoloni fikra za kuja na filosofia mbadala ilikuwepo hata kabla ya enzi za uhuru. Mwalimu hakukurupuka tu kwenda China na ghafla akaja na itikadi ya ujamaa.
 
So Muslims were better of during colonial era than after independence? Major religion in what sense-population,political influence, better living conditions?

No. That is not what I meant, nothing about being better-of before or after, it was a matter of lesser and greater evil.
 
Bibi Titi hakumpinga Mwalimu, bali alikuwamo ktk mpango wa kumpindua, na kumpindua Rais ni uhaini. Kitu kizuri ni kwamba hawakunyongwa, hata bibi titi alisamehewa baada ya kutumikia kifungo kwa muda.

Weye, weye, ndio weyee? unanini? Hivi utampindua usiye mpinga kweli? pumba zingine inabidi nkachekee msalani.
 
ina maana unataka kusema ikulu nzima haikuwa na Dish kuangalia newz kama BBC? siamini! alikuwa anapata wapi habari za nje?
Hapana. Haya mambo ya dish labda yalianza enzi za ruksa. Na ile tv/video aliyopewa na Mzee Bomani ilikuwa Msasani. Mwalimu spent his time there more than he did at Ikulu. Habari za nje mwalimu alipenda sana kusikiliza radio. Alipenda sana kusikiliza BBC to Africa. Pia radio Moscow mara kwa mara. Na kama kulikuwepo vipindi maalumu ubalozi wa Tanzania ulikuwa unamrekodia na kumwekea tapes kwenye dipbag.
 

Mkuu hiyo historia ya wapi? Nyerere hajawahi kuwa na Waziri Mkuu toka mkoa wa Mara. Mkuu wa majeshi kweli naye ni Binamu yake Ret. Gen. Musuguri. Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu toka Mkoa wa Mara ni Mzee Joseph Sinde Waryoba chini ya utawala wa Mwinyi. Kawawa, Sokoine, Msuya, Salim Ahmed Salim hawakuwa wanatoka Mara!
 


Halafu hata hizo alizotaifisha zikawa kama mashonde, nyang'a nyang'a baada ya muda si mrefu. Haa jamani tuliosoma zamani tulifaidi shule. Nna uhakika waliosoma kabla ya 1970 wataniunga mkono. Mtu ulikuwa unataka tu uende shule, hakuna kubanana, kila dawati lina draw, wino bure, kalamu bure, rangi bure, lab bure, michezo vifaaa kedekede, brass band hata wapiga brass harusini hawatuingii. Looo alivyokuja mzee wa uhasid! Kila kitu kikafa.
 

And what would that credit be for?
 
That is true only if it were true. Mwalimu alirithi jeshi la ukoloni. Huko ndugu zangu Wakurya walikuwa wameshajazana kwa sababu ya umahiri wao wa kupigana. Vivyo hivyo Wanyakyusa. Enzi za Mwalimu alijitahidi sana n kurecruit wachaga na makabila mengineyo ambayo hayakuwa traditional soldiers. Kwa mfano maafisa wa kikosi cha ndege, navy, intelligence, wote hawa hawakuwa Wakurya. Let us give Mwalimu his due. Alijitahidi kujenga Tanzania isiyo na matabaka ya kikabila.
 


Mazuri yepi? yataje basi, maana mie siyaoni, kumbuka, nilikuwepo sihadithiwi.
 
ukisikia ugonjwa ndo huo
yaani tanzania ilikuwa juu kwa ict wakati computer na tv zilikuwa banned????????
so radio tanzania ndio ilitufanya tuwe juu sio???????/
kipindi cha mikingamo sio?????????

Kulikuwa na vipindi vya ngoma zetu na vipindi fulani hivi vya masomo ya shuleni mwalimu anafundisha redioni huku mnasikiliza; ilikuwa teleconference ya wakati huo!
 

Naona hujaelewa nilicho kiandika, nimesema kama hoja ni makabila basi nyerere alikuwa akiogopa kila kundi kubwa, ama liwe la kikabila au la kidini, na UIslaam kwa kuwa ni kundi mojawapo kubwa kwa wakati huo, nyerere aliuogopa na hakuona haya kuukata mbawa zake. Na kama hapa panajadiliwa ukabila tu, mbona kuna vyama vya ushirika vinajadiliwa?
 
mods please ziunganisheni hizi.kuna mijadala mingi humu kumuhusu Nyerere na kila siku ni hoja zile zile tu hakuna jipya
 


Tena si hivyo tu,

Kandambili anasa,
Jeans anasa,
Lux anasa,
Colgate anasa,
Blue Band anasa,

Dahh, yule jamaa kijiji alichotoka watu wana roho mbaya sana. Kwa kuwa yeye huko alikotoka hajavitumia utotoni akawa ana usongo na wote wanaotumia hivyo vitu. Kweli kabisa maana hata Dar alipokelewa bado anavaa kaptura, duhhh, kina Sykes wakamvua kaptura, wakamwambia hapa pwani kuheshimika lazima uvae suruali, ushike bakora, uvae na kofia ya mkono. Suruali yake ndefu ya kwanza ni ya kuazimwa na kina Sykes.

Hivi jamani hata colgate anasa?
 
I bet u would kill to just achieve 1% of what Nyerere did!

Sijawahi kuona mwenye akili finyu akipewa "standing ovation" na bunge la SA!

Hivi nyerere alifanya kipi kizuri kwa nchi hii?
 

Wewe ulikuwepo wakati wa nyerere? au unabishana mradi ubishe tu? unanchekesha!
 
Mazuri yepi? yataje basi, maana mie siyaoni, kumbuka, nilikuwepo sihadithiwi.
Unajua hapa tusim-crucify Mwalimu sababu ya policy zake..., Socialism does not work sio hapa tu popote pale kwahiyo kwa kufuata policy zake za ujamaa alitaka kila kitu kiwe state owned na distributed equally to the masses.., kwahiyo if at all unaweza kusema njia aliyopitia labda haikuwa nzuri.

Hata dereva mzuri kwa bahati mbaya akipita njia mbaya safari huenda ikawa ngumu lakini hatutalaumu udereva wake bali ubaya wa njia..., therefore maswali yanakuja...
Je Nyerere alikuwa Mzalendo.... Ndio
Je alikuwa Mkabila..... Hapana
Je policies zake zilifanikiwa..... Hapana
Je alikuwa ana good intentions....... Ndio
Was he a good leader.... absolutely
 
duhhh, kina Sykes wakamvua kaptura, wakamwambia hapa pwani kuheshimika lazima uvae suruali, ushike bakora, uvae na kofia ya mkono. Suruali yake ndefu ya kwanza ni ya kuazimwa na kina Sykes.

Hivi jamani hata colgate anasa?
Nadhani hapa tungekuwa tunaongelea utanashati na mavazi nadhani labda angeshindwa..., lakini sidhani kama uongozi bora unaangalia una suruali ngapi au well dressed you are..., In short naona bora huyu aliyeazima suruali kuliko yule kile akienda kuonana na viongozi anavaa armani suit worth millions just to look great. By the way Colgate sio anasa lakini ile dawa ya meno iliyokuwa ikitengenezwa nchini was better kwa uchumi wetu kuliko Colgate, iliyokuwa inakuja kwa magendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…