Mwalimu ANGANILE MPETA is no more | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu ANGANILE MPETA is no more

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Lekanjobe Kubinika, Jul 21, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sijui kama hapa ni mahali pake, lakini najua wanajamii forum wengi sana watahusika na habari hizi.

  Mwalimu Anganile Mpeta ametuaga duniani tangu jana kunako saa 12.00 jioni baada ya kubanwa pumzi ghafla akiwa nyumbani kwake Rujewa Mbarali Mbeya. Alipelekwa hospitalini haraka na baada ya kama dakika 15 aliaga dunia. Niandikapo hivi, mwili wa marehemu Anganile Mpeta unafanyiwa taratibu za kuagwa pale Rujewa na kisha kupelekwa IWAMBI SEKONDARI mjini Mbeya ambako alikuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari moja karibu na Ivumwe ili nao wakamuage na kisha apelekwe kijijini alikozaliwa Mbigili Rungwe East kwa maziko kesho.

  Marehemu Anganile Mpeta alisoma Mwakaleli Middle School kunako 1971, akasoma Sekondari hadi Kidato cha Sita ambapo alikwenda Mujibu JKT na kushiriki vita ya Iddi Amin kule Kagera 1979. Kutoka hapo alijiunga na chuo cha Ualimu Chang'ombe DSM miaka 2, akapangiwa kazi Masasi Girls Secondary School Mtwara akiwa na Diploma.

  Baadaye alijiunga Chuo Kikuu cha DSM akapata Degree ya kwanza ya (Uchumi), kisha akapangiwa kazi Minaki Sekondari ambako alifundisha kwa kutoa As nyingi sana za Economics (EGM), akateuliwa kuwa Discipline Master wa Shule na baadaye Mkuu Msaidizi wa Minaki Sekondari kwa miaka kadhaa. Kisha alihamishiwa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kufungua Kyela Secondary School kama Mkuu wa Shule, ambapo baada ya miaka kadhaa alihamishiwa Rujewa Sekondary School kama Mkuu wa Shule wa kwanza kuifungua shule hiyo. Mwaka jana alihamishiwa shule ya mjini Mbeya (IWAMBI) ambako aliendelea kuwa Mkuu wa shule hiyo hadi umauti ulipomfika.

  Marehemu Anganile Mpeta atakumbukwa kwa mambo mengi na wanafunzi wake na wafanyakazi wenzake hata majirani kwa kutokuwa mwongeaji sana na kufuata sana utaratibu uliowekwa. Alikuwa kama hataki kukifanya kitu anakuambia waziwazi pasipo kusubiri.

  Aliaza kusumbuliwa na tatizo la moyo ambalo kidogo limuwahishe miaka michache iliyopita kama daktari maarufu Dr Mabula wa Hospitali ya Rufaa Mbeya asingeingilia kati, akarudi katika afya ya kawaida na kunawiri sana hata kuacha vyote alivyoagizwa kuachana navyo ili kutoathiri matibabu, mtoto wa kwanza kwa baba yake Mchungaji Mstaafu wa KKKKT Dayosisi ya Konde, Mch. Anganile Mwakapola (Mwaipwisi) ameacha mke na watoto wawili.

  Hayo ni maelezo machache sana yamhusuyo mwanataaluma wetu aliyetupotea, ili angalau wawili watatu waweze kukumkuka kwa kuwa picha haijapatikana mara moja. Ni maelezo ambayo huenda yanaweza kusahihishwa kidogo hapa na pale, lakini kimsingi

  Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema sana peponi, Amin.
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,074
  Likes Received: 6,537
  Trophy Points: 280
  RIP Mwalimu.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Rip Anganile Mpeta
   
 4. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  RIP one of our unsung heroes and heroines!
   
 5. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Poleni wafiwa Bwana awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
   
 6. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280

  Asante mkuu,..

  Alikua mwalimu mzuri sana,mimi nilikua mmoja wa wanafunzi wa pili kusajiliwa pale kyela sec.school,..alikua na msimamo mzuri sana kuhusu falsafa ya ualimu na elimu bora na si bora elimu.

  Natumaini watu wengi sana walifaidika na mchango wa huyu mtu.

  Sisi tulikupenda,ila Mungu anakupenda zaidi..............RIP
   
Loading...