Mwalimu akiagiza gari atapunguziwa kodi?

Mwalimu akiagiza gari atapunguziwa kodi?

Haya maswali kila siku uwa tunayajibu kuna thread nyingi za nyuma,Punguzo lipo lakini ni dogo na lenye procedure ndefu sana,magari ya biashara kama pick up,hiace n.k na magari yaliyo na CC zaidi ya 2000 hayana sifa ya punguzo,pia gari lililozidi miaka 10 halina sifa ya punguzo.Urefu wa procedure ni pale unapoenda ku sign form zako(kuna form maalumu ya exemption)hapa Bl inaitajika na Bl haipatikani mpaka meli iliyona gari lako iwe imeanza safari ya kuja Tz,sasa mfano Mwalimu hiyo form mpaka ipelekwe Wizarani na mizunguko mingine hivyo meli inawezafika Dar kabda hujamaliza process ukaishia kupigwa storage pale bandarini,nilishaingiza gari kwa Exemption Rav 4 ushuru ukaja 5.5ml utaona punguzo lipo lakini si kubwa kama wengi wanavyofikiri maana utalipa charge zote za bandari,Vat na punguzo dogo kwenye zile kodi nyingine,ukitaka habari zaidi tafuta agent mzuri atakupa maelezo.

Mkuu nakushukuru sana naendelea kujifunza na mchango waka umenijenga sana.haya mambo ukiwa mgeni ni vyema ukapata elimu ya kutosha kabisa kabla ya kufanya maamuzi.nakushukuru sana.
 
Salaam kwa wote!

Naam! Kuna kipindi nilisikia watumishi wa umma hasa walimu wakiagiza gari wanapewa punguzo la kodi, kama kuna mwenye taarifa za uhakika naomba anisaidie ni hatua gani zinatakiwa kufuatwa ili kukamilisha mchakato mzima.

Unaweza kuhudumia familia na gari kwa kiwango cha TZS 350,000 kwa mwezi?
 
Unaweza kuhudumia familia na gari kwa kiwango cha TZS 350,000 kwa mwezi?

Mkuu mwalimu wa shahada ya kwanza ya chuo kikuu anaanza na ngapi? Poa nimekuelewa mkuu ndio maana nataka vitz cc 990 ambayo ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana lakini pia kuniwezesha kuwahi vipindi sehemu mbalimbali maana vijana wanahitaji wapate nondo zangu kwa wakati.

Muda mwingine nashindwa kuwahi vipindi kwa sababu ya usafiri hapa dar.hivyo nimefanya tathmini nikaona hata kipato kitaongezeka mkuu
 
Vitz ni gari nzuri sana tena ukipata kenye cc 990 kama unavyosema katakufaa sana@ Nuruyamnyonge.endelea kupata elimu na agent mzuri mkuu Ujikomboe maana hapa mjini usafiri siyo ni sawa na chakula.
 
Vitz ni gari nzuri sana tena ukipata kenye cc 990 kama unavyosema katakufaa sana@ Nuruyamnyonge.endelea kupata elimu na agent mzuri mkuu Ujikomboe maana hapa mjini usafiri siyo ni sawa na chakula.

Naam mkuu! Tatizo liko kwenye mlolongo wa kupata punguzo la kodi maana mfumo wake umekaa kama haupo vile ili kubinya haki wakati serikali ilikwisha sema. Tunaziomba mamlaka husika wasimamie vizuri hizi taratibu, ili mwalimu nae arudishe heshima kama watumishi wengine na kufanya kuwa sehemu ya kivutio cha wahitimu wa kitato cha sita tena wenye one kujiunga na uwalimu.

Ukienda maofisi mengine hata chama cha walimu peke yake utakuta kila mtu kapaki usafiri wake pembeni sasa ifike wakati walimu tusimame na ikiwezekana tuanzishe chama chetu kipya cha MAAFISA ELIMU TANZANIA maana hiki cha CWT kimekwama kumkomboa mwalimu
 
Kweli kabisa mkuu hayo ndo mambo ya msingi tunapaswa kuyazingatia vinginevyo tutaendelea kuonekana kundi la watu wa chini sana.
 
Mwl. gari la nini ww? we jimwage na kitu TOYO a.k.a BOXER uwahi kupiga chaki. Magari waachie wenye nazo. Yaani eti VITZ unaulizia Exemption? mafuta, service utaweza kweli?

Mwalimu gari la nini wewe? Wewe unalo la nini? Huna adabu kajifunze adabu kwanza.
 
Mkuu mwalimu wa shahada ya kwanza ya chuo kikuu anaanza na ngapi? Poa nimekuelewa mkuu ndio maana nataka vitz cc 990 ambayo ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana lakini pia kuniwezesha kuwahi vipindi sehemu mbalimbali maana vijana wanahitaji wapate nondo zangu kwa wakati.

Muda mwingine nashindwa kuwahi vipindi kwa sababu ya usafiri hapa dar.hivyo nimefanya tathmini nikaona hata kipato kitaongezeka mkuu

Anza na pikipiki hutakaa ulalamike huna pesa ya mafuta
 
Naendelea kuwashukuru nyote kwa michango yenu na nitakuwa natupia jicho kuona nini cha kujifunza kutoka kwenu ahsanteni sana
 
Amina! Ukipata muda utaniambia ukisha agiza likifika bandarini ndio unaanza na mchakato wa msamaha wa kodi au taratibu zinafanyika mapema kitu kikiwa njiani.nitashukuru sana nakutakia majukumu mema na Mungu akubariki ommymbwambo

Ndugu kulingana na maelezo ya wengi humu angalia budget yako kama unaweza kuagiza bila exemption kuepuka usumbufu na kuwa na uhakika zaidi. aprox 805m for a vitz
 
Ndugu kulingana na maelezo ya wengi humu angalia budget yako kama unaweza kuagiza bila exemption kuepuka usumbufu na kuwa na uhakika zaidi. aprox 805m for a vitz

Ni kweli mkuu ikishindikana kupata hiyo exemption nitajikamua tu hii ndio serikali bwana wao wanapeana posho na matibabu nje ya nchi lakini kuweka utaratibu mzuri hasa kwa mwalimu kwa nini iwe tabu? Ushauri wako umetulia nitafanya hivyo baada ya kukata tamaa.
 
Mwl. gari la nini ww? we jimwage na kitu TOYO a.k.a BOXER uwahi kupiga chaki. Magari waachie wenye nazo. Yaani eti VITZ unaulizia Exemption? mafuta, service utaweza kweli?

We ni @$&@&$@¥£€#. kweli sijui unaishi dunia gani!! Kwaiyo unaona gari ni bonge la inshu kiasi kwamba ni ngumu kumiliki mwalimu iyo ni dharau pusi wee.
 
Back
Top Bottom