Mwakyembe unaua bandari yetu


Nyinyi si ndiyo wale mulioiba mpaka zile computer za bandari ili kupoteza ushahidi? Sasa kama mulikuwa munafanya kazi kisawasawa muliogopa nini mpaka ikabidi kupotezea ushahidi?

Makontena yameshindwa kupotea?
 
Hahaha mpwa watoto wetu watasomaje na tutawekaje heshima bar na gesti?

Mkwe wangu aliibiwa container la maziwa karudi nyuma kimaendeleo sasa namlea na yeye
 

Nimefarijika sana kuona post hii.. Maana yake ni moja tu.. Kwamba malengo ya Dr. Mwakyembe kuisafisha bandari yetu yameanza kuonyesha makali yake..
 
Zamani tuliikuwa tunaimba.. mabepari walia, mabepari walia... sijui tubadili maneno na kuweka "mafisadi walia"...?
 
Mkwe wangu aliibiwa container la maziwa karudi nyuma kimaendeleo sasa namlea na yeye

Hakufuatilia fidia? Uzuri wa bandari yetu ni kuwa wanakwiba wanamtandao wakiwemo wafanyakazi wa bandari na polisi, lakini Bandari inakulipa kama kawa. Kwani nini bana, hela si zetu wote?
 
wakuu sijaelewa,hii kuomba kibali kabla ya kuingiza meli inasaidia vipi vitu vyetu visiendelee kuibwa pale bandarini?
 
wakuu sijaelewa,hii kuomba kibali kabla ya kuingiza meli inasaidia vipi vitu vyetu visiendelee kuibwa pale bandarini?

Sijui taratibu zao bandarini zikoje lakini kwa common sense kama wizara inapata taarifa ya meli kabla ya kuingia na kuwa offloaded ni rahisi kuthibiti wizi. Idadi itahakikiwa na ikija kupotea watafuatilia ni MPAKA NGAZI IPI MZIGO BADO ULIKUWA KAMILI

Labda mkuu, Asprini na Robato wawe na mtazamo tofauti
 
Na mwaka huu mtanuna sana wezi wakubwa nyie! Fagia kabisa panya hao hadi uvunguni Mh Dr Mwakyembe!
 
Bodi Mpya ya Mamlaka ya Bandari: Uteuzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Bandari iliyofanywa na Mhe. Mwakyembe ni tumaini jipya kwa uhai na ufanisi wa Bandari Tanzania. Ninawafahamu vizuri Bw. John Ulanga, Dr. Jabiri Bakari Kuwe na Dr. Shayo. Hongera sana Dr. Mwakyembe kwa uteuzi makini. Kumbe watenda kazi wanajulikana, kwanini wateuliwa wakati jahazi limeshazama?

Bro John hongera sana kwa uteuzi huo. I now see light at the end of tunnel! God bless you and give you strength and courage to deliver to the expectations of all of us who are behind and hand in hand with you.
 
Bado na Waziri wa ardhi na miji nae atusaidie kufanya the same huko wizara yake. Haki ya Mungu hawa majamaa wa ardhi wanatia kinyaa pale wizarani, bado sielewi kama je wana viongozi au wapo wenyewe tu pale maana pananuka uozo wa rushwa. I hate them!!.
 

weee robert leo umetoa hoja kama umebanwa haja kubwa vileee....

yani nyie bandari mnajifanya mnataka kufanya kazi kwa effeciency kama bandari zingine duniani...kwa taarifa yako robert bandari yenu ni chafu na inanuka na haifai hata kidogo...huwezi kutoa conteiner kwa efficiency kisha halimfikii mteja linapotea mikononi mwenu...ni bora likakaa miaka 100 kwenye meli ili limfikie mwenyenalo kwa usalama sahihi

pole sana kwa kukatiwa mirija na mwaka huu mtakufa njaa...mungu ampe maisha marefu dr. Harison mwakyembe awanyooshe mtie adabu na tupate bandari safi kwa matumizi ya tanzania mpya ijayo,.....god bless tanzania.
 
Kuna yule mtoto wa mkuu wa operation cjui yani jitu jingajinga linaleta vx v8 hela katoa wapi
 
Tulijua tu mtapiga mayowe ..Mwakyembe ongeza dozi baba naona mapepo yameanza kutoka moja baada ya jingine
 
Anaua bandari anawaua wezi?
Na wabinafsi na wanaoona bandari shamba la bibi!
Mnalo mwaka huu lol!

Aisee safi sana Mwakyembe, km hujawahi ingiza mzigo wowote bandarini, utaona km jamaa anacheza lkn bandari imeoza rushwa, mwakyembe safisha hapo, timua wote wala rushwa.
 
... Kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere, hata leo makampuni na mashirika ya umma yanafilisiwa na wafanyakazi wenzetu na hawapigi kelele. Hivi bandari walikuwa wanafanya nini cha maana kabla ya kuja mwakyembe zaidi ya kujilipa vizuri? Tumeshinddwa vip kuwa na ushindani wa maana na bandari ya mombasa?
Hii inanikumbusha wakati wa kubinafsishwa kwa reli ya kati kwa wahindi miaka 2 iliyopita. Wafanyakazi wa reli walikuwa wakali kana kwamba ni wazalendo wa kweli kumbe ni kelele tu za kuzibiwa mirija ya ulaji wa fisi! Wafanyakazi wamelihujumu sana shirika la reli kwa kuiba mizigo, kuiba makontena matupu na kuyauza mtaani, kuangusha injini kwa lengo la kuiba mafuta. Mnakumbuka treni iliyoishiwa mafuta njiani reli ya Tazara? Hata Tazara mambo ni hayo hayo ya kuiba mbao na simenti za wateja, kesho tazara ikifa mtaona wafanyakazi wanavyokuwa wakali balaa-wakati shirika wanalifilisi wenyewe.

Watu wa bandari mmetuangusha sana kiasi kwamba hamna moral authority ya kupiga mikwara watu wanaojaribu kurekebisha mambo. Mpo kila siku kazini lakini hatuoni ubunifu wowote wa maana ili angalau tuone tuna vichwa vinavyofanya kazi. Binafsi naamini Mwakyeme anaweza sana kubadilisha sekta ya bandari, unless watu kama mtoa mada wamhujumu!
 
Kwa nini kuingia kwa meli bandarini kuhitaji kibali cha Wizara? Ina maana Mwakyembe hana imani na uongozi mpya aliouweka mwenyewe baada ya kumtimua Mgawe?

Nilikuwa nasikiliza BBC jana, wanaongelea jinsi Ethiopia Airlines ilivyokuwa an outlier success story. Mtu wa Ethiopia Airlines akaulizwa hivi kuwa shirika la umma kunasaidia sana kwa maana ya kwamba serikali inaweza ku pick up some slack mkishindwa, akasema to the contrary. Kuwa shirika la umma kunasababisha mikono mingi kwenye chungu, na ukiritimba. Kwamba kinachowasaidia wao ni serikali ya Ethiopia kutoingilia management ya Ethiopian Airlines katika maamuzi ya kibiashara.

Nilimuunga mkono Mwakyembe ku shake things up bandarini na kumtumia Mbakileki vilivyo.

Lakini huu ukiritimba una msaada gani? Ni kweli bandari inakuwa under utilized wakati meli zimejazana zikisubiri pwani ya Dar?
 

Pole sana Robato japo nashindwa kuacha kuamini kuwa wewe ni muathirika wa mabadiliko ya Mwakyembe.

 

Tatizo kwenye miti mingi hakuna wajenzi.
 
kaka wewe ndo mbumbumbu na sidhani kama hapa ni sehemu sahihi kwako. Mwache mh afanye kazi, aondoe wajinga wajinga kama wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…