Mwakyembe, Sitta 'walisafisha' nini Bandarini?

Unamw?gelea Mwakyembe huyu huyu aliyetuonyesha selfie za Masogange! Na Sitta yupi? Aliyesema ataenda mahakamani jina likikatwa?
 
Hao mawaziri wali play part yao na sasa ni zamu ya ngazi ya juu kabisa kufanya yao
 
Tulikuwa tunampa hongera na sifa nyingi humu Mwakyembe tukisema 'aliisafisha bandari' na ni 'mchapakazi' na wengine wakiomba ateuliwe kuwa Waziri mkuu ili alete Hiyo kasi na uchapakazi lakini tunakumbuka Sitta alipom replace na yeye Sitta akala 'ujiko' wa kuisafisha bandari na kuondoa madudu.

Kumbe in reality hakuna walichokifanya au walichokifanya hakikuwa na manufaa sasa tena sasa tunashingilia Magufuli na Majaliwa 'kuisafisha 'bandari na kuondoa madudu....

Maswali ya kujiuliza Sitta na Mwakyembe 'tuliwasifia' kwa nini hasa? Na kinachofanyika sasa tuna uhakika ndo soluhisho la kudumu? Kama sifa tulizowapa Mwakyembe na Sitta huko nyuma zilikuwa za makosa na hizi sifa tunazo mwaga sasa je? Hivi haiwezekani nchi hii mambo yakaenda bila kiongozi 'kutikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' na 'akamwagiwa' sifa tele?

Nchi zote zenye efficiency viongozi wao huwa 'wanatikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' Kama hapa kwetu?......

Duh mpaka sasahivi watu hawajaelewa. Hivi hao mawaziri wanahusika je na ushuru wa makontena? Je mmeambiwa bandari haikukusanya pesa za uingizaji wa hayo makontena? Ukweli ni kuwa walfage imelipwa na makontena yako kwenye records ya bandari ILA kule TRA hayoko, ndio maana suala hapa hakuna mfanyabiashara aliyelalamika kuibiwa kontena. Kuendelea kutoa hoja za kipuuzi hapa tutakuwa hatuitendei Haji nchi yetu na wala JF.
 
Mizigo yote ukiondoa ile ya jeshi lazima ipitie geti no. 5 kwa uhakiki wa maafisa wa TRA ambao ofisi yao iko mita chache kutoka geti no. 5 ambalo hulindwa na walinzi wa TPA. Kiutaratibu kabla mlinzi hajaruhusu kontena kutoka lazima ajiridhishe kwa kukagua uhalali wa nyaraka huzika ikiwemo utambulisho wa gari na dereva alibeba mzigo. Pale kibanda cha TRA zipo cctv camera pia. Hata hivyo mfumo uliotengenezwa pale TPA ni wa kupiga dili tu kuna uozo kupindukia!!!
 
Kama hamkubali kamishna utendaji angemuondoa tu na kumbadilisha
ila kusema kafukuzwa kazi kisa wizi wa kontena huoni kama
kamdhalilisha mtu? ulinzi wa kontena sio direct responsibility ya kamishna wa TRA...

Hivi wakati mwinyi anajiuzuru uwaziri wa mambo ya ndani kwa sakata la watu kukatwa mapanga kule shinyanga,alikuwa na direct responsible ya kuwalinda hao waliokatwa mapanga?,just thinking loud!!!
 
The Boss: Wizara ya Uchukuzi ina mipaka yake kama ilivyo kwenye shamba au kiwanja chako. Pia hata ukitoka kuoga, ukijifuta na taulo jeupe lazima taulo litaonyesha uchafu uliobaki mwilini. Tusiziondoe sifa tulizowapa ila ni muhimu kujiongeza. Watakaoingia sasa wafanye zaidi ya Mwakyembe na Sitta
 
Mbona unataka kufanya mambo yawe magumu bila ya sababu? Kwani ni nani amekwambia nchi yetu ina hiyo uliyoiita ,,effieciency ya Uongozi"? Ingekuwepo tungekuwa third world?

Acha kupoteza muda wako kwa kuanza kuchimba na kupekenyua mambo ili mradi tu upate cha kumkosoa Raisi Magufuli kwa ayafanyayo!
Kuna jambo unapaswa ulitambue kama bado haujalitambua kila kitu hapa Duniani ni relative hivyo muache Raisi Magufuli atumikie Uraisi wake ndiyo kwanza ana wiki tatu hivyo siyo fair Duniani hata kwa Mungu kuanza kumuhukumu Kiongozi aliyeko madarakani kwa muda wa wiki tatu, hakuna mtu mwenye akili ambaye atakuelewa Dunia hii kwamba yote haya na shutuma zote hizi ni Raisi aliyeko madarakani kwa wiki tatu tu!

Hepuka ku generalize mambo na huo msamihati wako wa "relative"
 
Kwa mtazamo mwingine ni kuwa TPA walifanya kazi yao, walifanya records za containers na wenye containers walilipa custom duties kama kawaida ndio maana records zipo wazi TPA...
Shida ipo huko TRA, ICT ya TPA na walinzi wa TPA Gate 5, kuna rushwa zilitembezwa hapo ili containers zipitishwe bila TRA kulipwa kodi stahiki, maana yake inawezekana wafanyakazi wa TRA walikuwa na records zilizotumwa na TPA, lakini wao kwa kupewa rushwa wakatoa release order bila kupokea malipo...
Mchezo ulichezwa na maafisa wa TRA, ICT ya TPA na walinzi...huwezi kuihusisha TPA moja kwa moja coz tayari management ilipokea containers, walitoza custom duties na kurelease docs TRA..ndivyo nilivyoelewa!

Nafikiri hizi containers zilitoka kama zinaenda bandari kavu ndio maana TPA salama. Kwa sababu container zinazokwenda bandari kavu hazihitaji release order ni jukumu la TRA kufanya monitoring kama kweli zimefika huko na ndio sababu ya wao kuingia kwenye swala hili.
 
Sasa walinzi wa TPA ndio kamishna wa TRA afukuzwe?
unaona ni busara?

The Boss

Sasa unadhani wajibu wa kamishna wa kodi Tanzania ni nini?

Yeye alipaswa awe watch dog wa kamishna wa forodha. Awe anapata data zote kutoka TPA na ku cross check kuona mapato yaliyo ingizwa TRA....kama kamishna mkuu wa mapato alipaswa kumsimamia kamishna wa forodha kwa staili hiyo lakini badala yake hakufanya hivyo. Ulitaka rais amchekee tu!?

Sasa kuanza kusema tukomalie walinzi wa magetini sisi wa kazi gani walinzi!? Walinzi watashughulikiwa na mamlaka ya bandari yenyewe...unataka rais afukuze walinzi!? Wewe kweli boya.

Kwanza modes unganisheni huu uzi maana ni sawa na ule mwingine tu.

Moderator, Invisible, Paw
 
Last edited by a moderator:
Kwa mtazamo mwingine ni kuwa TPA walifanya kazi yao, walifanya records za containers na wenye containers walilipa custom duties kama kawaida ndio maana records zipo wazi TPA...
Shida ipo huko TRA, ICT ya TPA na walinzi wa TPA Gate 5, kuna rushwa zilitembezwa hapo ili containers zipitishwe bila TRA kulipwa kodi stahiki, maana yake inawezekana wafanyakazi wa TRA walikuwa na records zilizotumwa na TPA, lakini wao kwa kupewa rushwa wakatoa release order bila kupokea malipo...
Mchezo ulichezwa na maafisa wa TRA, ICT ya TPA na walinzi...huwezi kuihusisha TPA moja kwa moja coz tayari management ilipokea containers, walitoza custom duties na kurelease docs TRA..ndivyo nilivyoelewa!

Unachotaka kujaribu kutenganisha ni kama kujaribu kutenganisha tremi na mataruma, au mtumbwi na bahari wakati unaona kabisa inashindikana. TPA na TRA ni wahusika wakuu katika hili na lipo wazi, sasa ukijaribu kuondoa ICT TPA iliyomo ndani ya TPA unamaanisha nini? Au ni dhana ipi hapa unataka kutuaminishanayo?
 
How I wish Magufuri angefanya kazi kama Sokoine enzi zile za kushughulikia wahujumu uchumi. The present ufisadi has no difference with economic sabotage of Sokoine's time. Aliamuru mawazir wote ku surrender passport zao kwake. Yaani alishughulikia tatizo kutoka kwenye mzizi.

Hivyo basi, Mwakyembe na Sitta walipaswa kuwa behind bars by now kwa kusafisha vibaya bandari! Kwanza huo uwaziri walipewa kama shukrani kwa kuilinda serikali against Richmond scandal.
 
Tulikuwa tunampa hongera na sifa nyingi humu Mwakyembe tukisema 'aliisafisha bandari' na ni 'mchapakazi' na wengine wakiomba ateuliwe kuwa Waziri mkuu ili alete Hiyo kasi na uchapakazi lakini tunakumbuka Sitta alipom replace na yeye Sitta akala 'ujiko' wa kuisafisha bandari na kuondoa madudu.

Kumbe in reality hakuna walichokifanya au walichokifanya hakikuwa na manufaa sasa tena sasa tunashingilia Magufuli na Majaliwa 'kuisafisha 'bandari na kuondoa madudu....

Maswali ya kujiuliza Sitta na Mwakyembe 'tuliwasifia' kwa nini hasa? Na kinachofanyika sasa tuna uhakika ndo soluhisho la kudumu? Kama sifa tulizowapa Mwakyembe na Sitta huko nyuma zilikuwa za makosa na hizi sifa tunazo mwaga sasa je? Hivi haiwezekani nchi hii mambo yakaenda bila kiongozi 'kutikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' na 'akamwagiwa' sifa tele?

Nchi zote zenye efficiency viongozi wao huwa 'wanatikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' Kama hapa kwetu?......

Mabadiliko ya kweli huwa yanakumbana na mtikisiko. Hizo nchi unazosema zimepiga hatua, zilipitia hatua tunayopitia chini ya JPM.

Akina Mwakyembe na Sitta walifanya walichofanya chini ya JK. Sasa ni wakati wa JPM. Either Mwakyembe au Sitta hawawezi wakafanya vile vile. Ni imani yangu kwamba kipindi cha JPM Watafanya vema ziadi.

JPM anaweza kutuvusha kuelekea kwenye suluhu ya kudumu. Tatizo kubwa si ufisadi bandarini au wizara ya mali asili. Tuna tatizo kubwa ambalo ni mmomonyoko wa maadili. Ili kurejesha maadili kwenye reli, lazima uwe na kiongozi mkuu wa nchi wa mfano. JPM ni zawadi kwa mara nyingine tena kwa Watanzania wapenda amani na Maendeleo endelevu.
 
Why Bandari kavu?nani mfaidika?Nani anasafirisha container zenye mizigo toka bandari kuu kwenda bandari za nje...?wizi umefanywa nje ya bandari..zikiwa zinasafirishwa toka bandari kuu kwenda bandari kavu..za ubungo,vingunguti,TRH,AZAM,SDV,TICTS-UBUNGO,GSM....
 
Hapo hilo linawezekana bila kamishna wa TRA kujua
maofisa wa chini waka forge documents...na walinzi wa TRA wakaruhusu kontena zipite
na wenye kontena kama hawajalalamika it means wanahusika...
kamishna kaonewa..yeye kazi yake kuu ni kukusanya mapato nchi nzima
sio kulinda makontena bandarini

na hili ndio tatzo la JPM anavamia watu wa receiving end anaacha root cause hata pale muhimbili alichemsha in this sense tukatoa hela na mashine still zmekufa
 
Hii nchi tunapenda sana kulea upuuzi. Watendaji chini yako wamevurunda wewe upo tu unatazama, mwisho wa siku wewe ndio utawajibika. Hii itafanya watu wawe makini na kusimamia chini yao. Mbona TOKOMEZA mawaziri kama Kagasheki na Nchimbi waliwajibika wakati hawakushika hata fimbo. Haya mambo yakijinga kutetea wezi yakome, kila kiongozi anawajibika kwa utendaji mbovu wa watu wa chini yake
 
The Boss na mimi naomba nichangie kidogo...

1. mwakyembe ana file chafu sana hasa linalohusisha shirika la ndege..kama wataamua kulifanyia kazi atashtakiwa kama wale wafanyakazi wa shirika la ndege walioshitakiwa..wizi alioufanya hapo ATCL ni mkubwa sana na kama haki itatendeka fast jet itakufa maana wengi ndo wamewekeza huko...

2..inaonekana unamtetea huyo bade ...kwa lililotokea amestahili kusimamishwa..kwa uchunguzi uliofanyika ni miongoni mwa watanzania ambao hawaweki hela bank na badla yake wanaweka kwenye sim tank na kutundikwa juu kana kwamba lina maji kumbe limejaa pesa..kuna mwingine yeye nyumbani kwake mahali anapopaki magari kwa chini amezika sim tank mbili na kisha kupaweka level juu zinapaki gari kumbe chini kafukia mabilioni ya hela..mwingine yeye nyumbani kwake ana chumba cha siri (underground room) anatumia chumba hicho kufichia pesa..

mda huwa ni hakimu mzuri sana nyie subirini mbona bado.......
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom