Mwakyembe ndani ya kanisa la Gwajima; ashukuru kwa maombi akiri kulishwa sumu!

HATIMAYE Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe,kwa mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu atoke India kwa ajili ya matibabu.
Dk. Mwakyembe alionekana jana kwenye Kanisa la Ufufuo naUzima la jijini Dar es Salaam,linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, katika ibada maalum ya kumshukuruMungu kwa muujiza wa kupona ugonjwa uliokuwa unamsumbua.
Kiongozi huyo alisema kuwa nguvu za mafisadi zimeshindwakummaliza.
Alisema kuwa hivi sasa anatarajia kuzunguka kwenyemakanisa mbalimbali nchini kutangaza kushindwa kwa wabaya wake ambao walipangakummaliza.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na madai kuwa Dk. Mwakyembeamelishwa sumu, lakini jana hakuweka bayana ni ugonjwa gani unaomsumbua naumesababishwa na nini
“Sikuwahi kuvaa viatu tangu nilazwe nchini India, lakini kwa mara ya kwanzaleo nimevaa, shetani alipanga kunimaliza lakini ameshindwa.

Nimepanga kuzunguka kwenye makanisa kumzomea shetani(mafisadi) kwamba ameshindwa na kuwashukuru watu wa Mungu kwa maombi yao,” alisema.
Kikosi cha wapambanaji wa ufisadi
Katika ibada hiyo, Dk. Mwakyembe alisindikizwa na Waziriwa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; mbunge wa Kahama JamesLembeli (CCM); mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM); na Aloyce Kimaro,aliyekuwa mbunge wa Vunjo.
Makada hao waliojipambanua kuwa ni wapambanaji wa ufisadiwalisema kuwa kamwe hawataogopa chochote katika mapambano dhidi ya ufisadi kwakuwa neema inakuja siku za usoni.
Sitta alisema machozi ya Watanzania hayawezi kupotea buredhidi ya mafisadi ambao wameamua kuzitumia rasilimali za taifa kujinufaisha.
“Neema inakuja na nchi itarudi kwenye mstari ambaoMwalimu Julius Nyerere alitamani taifa liwe, hakutaka liwe hivi leo ambapobaadhi ya watu wanatumia migongo ya wenzao kupata mafanikio.
Nchi leo imejaa magenge ya waovu ambao wamejipangakuitafuna bila kujua Tanzaniani ya Mungu, mimi pamoja na kundi langu la kupambana na ufisadi hatuogopichochote,” alisema Sitta.
Sitta alitumia muda mwingi kuzungumzia unyonywajiunaofanywa na waovu (mafisadi) ambao wamewaacha wananchi wakiishi maisha magumubila msaada wowote.
Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wauminiwaliohudhuria kanisani hapo, Sitta alisema viongozi wengi wanatumia dhamanawaliyopewa kwa ajili ya kuliibia taifa kitendo kisichokubalika mbele ya Mungu.
Akitumia kifungu cha Biblia (Habakuki 1:2-4) alisemakilio cha Watanzania juu ya maovu na kutotendewa haki kitafutwa hivi punde.
“Hata kwenye nchi yetu wananchi wanalia juu ya shidawalizonazo, huku uovu na udhalimu ukiendelea; hakuna pa kukimbilia, haki hakunakama ipo imelegea na inawanufaisha mafisadi.
Mikopo ya wanafunzi inacheleweshwa makusudi kwa lengo lawanafunzi hao kufukuzwa kwa kukosa ada, nchi inanyonywa, lakini Mungu anaona naiko siku ataingilia kati, hawezi kukubali watu wake wateseke,” alisema.
Alienda mbali zaidi na kusema nchi itapona na uongoziutabadilika.
Ugonjwa wa Mwakyembe
Waziri Sitta amesisitiza kwa mara nyingine kuwa NaibuWaziri wa Ujenzi, Harrison Mwakyembe, alilishwa sumu.
“Nilishasema na narudia tena alilishwa sumu; miminimekuwa naye muda mrefu akiwa Indiana madaktari wa kule wanasema alilishwa sumu, kamawanabisha vyombo vya uchunguzi vitoe majibu haraka,” alifafanua.
Alisema miguu ya Mwakyembe ilikuwa kamaya tembo na ngozi yake ilikuwa inatoa unga.
Anne Kilango atema cheche
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, alisemaataendelea kupambana na kamwe hatachoka, kwani amevumilia mengi katikakuwawakilisha wanyonge.
“Naipenda nchi yangu na napenda haki, kiongozi bora niyule anayetenda haki kwa wananchi wake, nitaendelea kusimamia na kusema kweli,”alisema.
Alisema amezaliwa kwa ajili hiyo na ataendelea kupiganiahaki ya wanyonge.
James Lembeli anena
Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), amesema licha yaBunge kuwa ni mhimili wa nchi lakini ndiko kwenye ufisadi mkubwa.
“Wachungaji na viongozi wa dini liombeeni Bunge kwaniwatenda maovu wako huko, kwani wabunge wengi husimama kwa ajili ya kuteteanafsi zao na kamwe Askofu Josephat Gwajima usikubali mafisadi kuathiri kanisalako,” alisema.
Kauli ya Aloyce Kimaro
Kimaro naye alisema yote yanawezekana kamaMungu alivyosema na siku zote ukweli unahitajika.
Kimaro aliongeza kuwa ukweli hauchagui mtoto au mkubwa navigumu kwao kutendewa baya kwa vile Mungu mara nyingi hupenda mkweli.
“Mkiona wala rushwa semeni ukweli, hakuna watakalowafanya;Mungu atawalinda kutokana na kumpenda mtu wa namna hiyo,” alisema.
WAKATI huo huo, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa,amechangisha zaidi ya sh milioni 204 katika harambee ya Kanisa la Kiinjili laKilutheri Tanzania(KKKT), lililoko mjini Shinyanga, hivyo kuvuka lengo halisi.
Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi jana katika harambeehiyo iliyolenga kukusanya sh milioni 115, kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo hatua ya kuezeka,alikuwa kivutio kikubwa kwa waumini ambao wakati mwingi walikuwawakimshangilia.
Akizungumza katika harambee hiyo, iliyochangisha shmilioni 136 zilipatikana taslimu na ahadi ya sh milioni 68, Lowassa ambaye piani mbunge wa Monduli (CCM), alitoa wito kwa Watanzania kujenga milango mipanaya ushirikiano wa kimaendeleo.
Alisema, Watanzania wanao wajibu mkubwa kuhakikishakwamba wanadumisha maradufu ushirikiano, ikiwa ni pamoja na kushirikikikamilifu kuchangia shughuli mbalimbali za madhehebu ya dini badala yakutegemea msaada kutoka kwa wahisani.
“Zamani tulikuwa tukitegemea sana Wazungu watusaidie, lakini kwa sasatunashukuru hali hiyo imeenda inatoweka,” alisema Lowassa ambaye alitumia mudausiozidi dakika nne kuhutubia kwenye harambee hiyo.

 
Ni lini nayeye atatambua kuwa anapaswa kuwajibika mbele ya Tanzania.

Amebaki kusema anaonewa na anapitia magumu,je yeye hajawa sababu ya watanzania kuwa na hali mbaya?
Ni lazima atumbu mbele ya Mungu na watanzania kisha tusonge mbele.

This is inhuman.
Dr.Slaa alidai anataka kulishwa sumu pia.
Walianza na watu wao wa ccm
ngoja wamfikie mmeo tuone kama utayasema haya.
 
Hawa watu kumbe ni wapuuzi hivi.
Yaani kanisani siku hizi ndo uwanja wa siasa?
Sitta ni hovyo kabisa,sijui wachungaji wanao tumiwa hivi na binadamu watajibu nini kwa Mungu.
 
Mimi awa watu wanaojiita wapiganaji wa ufisadi hawana jipya,ni midomo tu subiri 2014 watakavyoanza kubwabwaja mpaka mapovu yanavyowatoka,sitta ndiye mnafiki mkuu kwa jinsi alivyomaliza suala la richmond ni sawa na picha/filamu za kibongo ambapo mwisho wake uwa ni upupu mtupu,mwakyembe aliamua kuficha sehemu ya taarifa ili kuilinda serikali,kilango kwa sasa hata kumsikiliza bungeni unapata kichefuchefu!namkumbuka anna abdallah kwenye bunge lililopita aliwai kusema si kwamba hao watu wana uchungu na nchi zaidi yao bali wanajua kupiga kelele,ukweli sasa unajidhihirisha na kamwe siwezi kuwaamini tena.

Hivi aliekuwa na jukum la kumaliza issue ya Richmond na kutoa uamuzi alikuwa ni sita au wabunge kwa ujumla na baba liz 1
 
Samwel Sitta amefunguka WAPO radio. Anasema Mwakyembe alipewa sumu. Mwakyembe anasema atapita makanisa yote kila Jumapili kumshukuru Mungu kwa kumnusuru.

Sitta amehubiri amesema kuna siku inakuja machozi ya watanzania hatamwagika bure.
 
mi' siongei! namsubiri 2015 jimboni, maana kama waliomchagua wapo kanisani kawe, basi atarudi bungeni 2015. huyu jamaa ni mnafiki kule kwake urambo hakuna hata rami za ndani, shule za advance ni moja tuu jimboni kwake. Wakuu! huyu 6..hatofautiani na seif khatibu ambaye jimbo lake lote mtandao uliopo ni Zantel tuu, huu ni uhuni. wasitufanye watanzania mbumbumbu, sitta hana lolote

ha ha...rami???
 
Ili nirudishe imani yangu kwao hao wanaojiita makamanda wa ufisadi kwanza watoke CCM na kujiuzuru uwaziri!Pili kila unknown waifanye kuwa known to the public.Kuliko kusema tu kila siku kuwa mafisadi wanalitafuna taifa na watashindwa huku nao wakiwa ni sehemu ya serikali ya kifisadi! Anne Kilango huyo yupo kujitafutia umaarufu tu wala hana uthubutu wowote zaidi ya kuongea sana.Hana tofauti na wabunge wengi wa CCM.Kama kweli ni jasiri na hayupo kimaslahi ajiuzuru ubunge na kujitoa CCM vinginevyo simtofautishi na Manyanya.
 
Samwel Sitta amefunguka WAPO radio. Anasema Mwakyembe alipewa sumu. Mwakyembe anasema atapita makanisa yote kila Jumapili kumshukuru Mungu kwa kumnusuru.

Sitta amehubiri amesema kuna siku inakuja machozi ya watanzania hatamwagika bure.

aisee nimeangalia dvd ya church jana baada ya ibada sikuamini bana Kumbe sitta ni mchungaji kabisa
kamwaga neno kama hana akili nzuri ikabidi watu waanze kupiga makofi kama gwajima anaapanda kuhubiri
 
Mwakyembe(20).jpg

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe


Kwa mara ya kwanza tangu augue ugonjwa wa mtawanyiko wa ngozi na kulazwa nchini India mwaka jana, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amehudhuria kanisani na kuwashukuru Watanzania kwa kumwombea kwa Mwenyezi Mungu ambaye amemponya.

Oktoba mwaka jana, Dk. Mwakyembe, alikimbizwa nchini India kwa matibabu zaidi baada ya hali yake ya afya kuzidi kuzorota, huku tetesi kizitolewa kwamba alilishwa sumu na watu wasiojulikana.

Mwishoni mwa Desemba, mwaka jana, Dk. Mwakyembe alizungumza na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya IPP na kukataa kueleza chanzo cha ugonjwa wake na badala yake alisema hatolipa kisasi kwa wabaya wake.

Akizungumza jana kwenye ibada katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo jijini Dar es Salaam kwenye ibada ya kumshukuru Mungu kwa kumponya, alimshukru Mungu pamoja na Watanzania kwa kumwombea katika kipindi chote alichokuwa anaumwa na kulazwa nje ya nchi.

Dk. Mwakyembe ambaye aliingia katika ibada hiyo saa 7:23 mchana, alisema Watanzania wamefanya kazi kubwa kumwombea yeye na kaka yake, Profesa Mark Mwandosya, katika kipindi chote baada ya kupatwa na maradhi.



Aliahidi kuwa kila Jumapili atakuwa anatembelea makanisa mbalimbali kwa ajili ya kutoa shukrani zake baada ya kupona kutokana na nguvu za Mungu.

Aliweka bayana kwamba jana ilikuwa mara yake ya kwanza kuvaa viatu tangu mwaka jana alipopatwa na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua na kukiri kwamba yalikuwa mazito.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye alisoma Neno la Mungu.

Hata hivyo, Sitta alirusha kombora lingine safari hii akisema nchi inayumba, inanyonywa na kuliwa na magenge ya waovu wachache ambao wamejipanga vilivyo huku wakiwa hawana hofu ya Mwenyezi Mungu.

Kadhalika, Sitta amesema nchi imefika mahalia pabaya ambapo kuna kundi la watu wachache wenye fedha chafu ambao wanatoa ufadhili ili kuwadhuru wenzao.

Sitta alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akimshukuru Mungu kwa kuweza kumponya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe katika viwanja vya Tanganyika Packers.

Alisema wakati wananchi wengi wanalalamikia kupanda kwa gharama za maisha na kukabiliwa na mahangaiko makubwa, lakini kuna kundi la waovu wachache wanaoendelea kuitafuna nchi.

Bila kuwataja majina ya watu hao, Sitta alisema siku inakuja ambapo machozi ya Watanzania yatafutwa na kwamba kundi hilo la waovu limewafanya wenzao kama daraja la kupandia wanakotaka kwenda.

Alisema hivi sasa haki imelegea na mtu anapoipata inakuwa imepindishwa na kwamba hali hiyo inatokana na vitendo vya rushwa na udhalimu uliokithiri hapa nchini.

Sitta alisema huko tuendako nchi itapona na uongozi wa nchi utabadilika na kwamba mafisadi wanaotumia mamilioni ya fedha kuwaondoa viongozi makini madarakani watashindwa.

"Mtu akilipwa fidia kiasi anachopata kinakuwa nusu ya kile anachotakiwa kupewa kama haki yake na hii imetokana na watu kutokuwa na hofu ya Mungu,' alisema.

Kuhusu suala la kundi la watu kutoa ufadhili ili kuwadhuru wenzao, Sitta aliweka bayana kwamba watu hao wapo na wamehusika kumnywesha sumu, Dk. Mwakyembe.

Alisema hila na mbinu chafu za kumdhuru, Dk. Mwakyembe zimeshindwa na kuahidi kwamba yeye na wapambanaji wenzake wa vitendo vya rushwa hawatarudi nyuma na wala hawatishiki na mipango hiyo aliyoiita miovu.

Alitolea mfano, Nabii wa Mungu aitwaye Habakuki ambaye alimwambia Mungu kwamba " nilie hadi lini Bwana ili upate kunisikia."

Alisema madaktari bingwa wa ngozi hapa nchini walishindwa kujua ugonjwa uliokuwa ukimsumbua, Dk. Mwakyembe lakini Mungu aliweza kusimama naye na kumponya.

Alibainisha kuwa sumu aliyonyeshwa Dk. Mwakyembe kutokana na nguvu za Mungu ilishindwa kumdhuru sehemu mbaya na badala yake ilitoka nje kupitia kwenye ngozi ndiyo maana nywele zote zilinyonyoka kichwani.

"Ngozi nne zimetoka katika mwili wa Dk. Mwakyembe na sasa hiyo aliyonayo ndiyo inarudi kama ilivyokuwa na huo ndiyo uponyaji wa Mungu," alisema.

Wengine walioungana na Dk. Mwakyembe katika viwanja hivyo ni pamoja na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli, Mbunge wa Viti Maalum, Hilda Ngowi na Mbunge wa zamani wa Vunjo mkoani Kilimanjaro, Aloyce Kimaro.

Jana ilikuwa mara ya kwanza kwa Dk. Mwakyembe kutoka nyumbani na kuzungumza akiwa na wapambanaji wenzake wa masuala ya ufisadi hapa nchini tangu augue ugonjwa wa mtawanyiko wa ngozi mwaka jana na kualazwa nchini India.



CHANZO: NIPASHE
 
Nimeiona post yako kwa kuchelewa,je wameonge nn hasa?.Vp sura ya Mwakyembe is he recovering?

He is, but nadhani aliathirika sana. Nimemuona jana, ngozi yake imepauka sana nadhani hata mafuta yanadunda, halaf nahisi hata nywele zimenyonyoka zote kwa sababu muda wote anavaa kofia na mikononi hakosi gloves...!
 
Asante MUNGU kwa uponyaji ,hakika wewe ni MUNGU ! Ole wao wanaoendelea kula na MAFISADI wakati wanafanya kazi ya MUNGU,acheni harambee za kuwasafisha mafisadi.....MUNGU atawaumbua na kuwaangamiza!!!!!!!!!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA...
 
Back
Top Bottom